Chuo cha Taasisi ya elimu ya watu wazima (IAE) kimekuwa na changamoto ya kuto kutoa AVN Number kwa wahitimu wake toka Mwaka wa masomo 2023/2024 na hakuna majibu mazuri yanayotelewa wakiulizwa.
Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima au Institute of Adult Education (IAE) kwa Wahitimu utaratibu ulikuwa ni wanatoa vyeti Mwezi Juni ila mpaka sasa hakuna dalili yoyote ya kutoa vyeti kwa Wahitimu wa Diploma 2024 ilihali tunahitaji vyeti vitusaidie.
Sisis Wahitimu wa Chuo hichi ngazi ya Diploma tuliohitimu Desemba 2024 tulijulishwa kuwa tutapewa vyeti Juni 2025 lakini kabla ya hapo tuliambiwa kutakuwa na statement ya matokeo ambayo sehemu nyingine wanaitwa result slip au transcript, nayo mpaka sasa ni kimya huu ukiwa ni mwezi wa Tisa sasa.
Hali hiyo imeathiri Watu wengi, kwani waliokuwa na mpango wa kuendelea kwa ajili ya vyuo vingine nikiwemo mimi katika usajili wa Julai 2025 tumekwama kwa kuwa ilikuwa ngumu kwetu kwasababu pia hakukuwa na AVN Number.
Utaratibu ulivyo kama cheti hakijatoka chuo kinakupa AVN Number baada ya kuwa kimewasilisha matokeo yetu Baraza la Elimu ya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi (NACTVET), inavyoonekana hata matokeo yetu hayajawasilishwa NACTVET.
Tukiuliza Chuo hakitoi majibu yanayoeleweka, ajabu ni kuwa hata graduation nayo imesogezwa mbele hadi Desemba 2025, sasa sijui huu utendaji wao upoje.
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.