Wahitimu wa Vyuo mnakwama wapi? Kina Millard Ayo, MC Garab, Babu Tale, Hamissa Mobetto wanakimbiza kutawala fursa za social media

Wahitimu wa Vyuo mnakwama wapi? Kina Millard Ayo, MC Garab, Babu Tale, Hamissa Mobetto wanakimbiza kutawala fursa za social media

Wewe Binafsi umefanikiwaje huko?

Mimi sijasomea taaluma za kutawala mtandaoni. Ndio maana nimeuliza graduates wenye taaluma ama tabia zinazoruhusu kutawala mitandaoni nilizozitaja kwenye uzi.

Pia maendeleo yangu sio haba kwa mtu mwenye age yangu.

Mimi ninamiliki rums za kupangisha zaidi ya 30. Plus Viwanja kazaa

Na safari bado inaendelea..
 
Mimi sijasomea taaluma za kutawala mtandaoni. Ndio maana nimeuliza graduates wenye taaluma ama tabia zinazoruhusu kutawala mitandaoni nilizozitaja kwenye uzi.

Pia maendeleo yangu sio haba kwa mtu mwenye age yangu.

Mimi ninamiliki rums za kupangisha zaidi ya 30. Plus Viwanja kazaa

Na safari bado inaendelea..
Okay, vizuri.

Ila kwani hao graduate wamesomea hizo taaluma za kutawala mitandaoni Kweli?

Je hizo taaluma za kutawala mitandaoni zinafundishwa huko vyuoni?
 
habari wadau.

kila mwaka udsm inamwaga vijana graduates wenye degree mbali mbali.

Mzumbe na udom hivyo hivyo.

Ajira ni ngumu wote tunajua, graduates karibu wote wa vyuo hivyo vikuu huwa wanatumia social media mbali mbali.

kizazi cha internet kinatambua kwamba kuna fursa nyingi za kupiga hela na ajira zinapatikana ukiweza kutawala ama kujibrand kwenye mtandao.

1.vyuoni kuna wadada kibao wana tabia kama za Hamisa mobetto, najiuliza wanakwama wapi kutumia tabia zao hizo hizo Kujibrand na kupiga hela za mtandaoni. Hamisa mobetto form 4 failure anawazidi vipi ujanja dada zetu wenye tabia kama zake waliojaa vyuo vikuu vyetu.

2. Mc garab ni mwalimu level ya diploma kasoma zake kigurunyembe teachers college.. kajiongeza kwa kujibrand mtandaoni.. kawa MC mkubwa anapiga hela harusi moja anachaji milioni 4. kwenda kuongea masaa kazaa ukumbini. wasomi wa vyuo vikuu na degree zetu tunakwama wapi kujibrand kwa kutumia elimu zetu tuwe zaidi yake

3. Millard ayo na yeye hivyo hivyo. form 4 failure kasoma zake certificate ya journalism tu vyuo vya kienyeji. ila ndie amedominate soko la habari. sababu kuu kajua kujibrand mtandaoni.. udsm inamwaga graduates wenye degree za uandishi wa habari kila mwaka,, wanakwama wapi kujibrand kwa kutumia elimu zao wamkimbize millard ayo. maana internet unajibeba mwenyewe kwa content zako

Babu tale na yeye kajiongeza kadandia umeneja WCB, umembeba mpaka kaenda bungeni, wasomi wa managemet degrees wanamwagwa kila siku na vyuo vikuu vyetu, why hawajiongezi kwenye fursa za ku manage wasanii

wasomi tunakwama wapi kutawala ajira za mitandaoni
Ni wenzetu, wanatuwakilisha, kwa pamoja tunasema, fani inalipa
 
Okay, vizuri.

Ila kwani hao graduate wamesomea hizo taaluma za kutawala mitandaoni Kweli?he hizo taaluma za kutawala mitandaoni zinafundishwa huko vyuoni?

Journalism ni mojawapo lazima iende mtandaoni ili kusambaza habari.

Taaluma za creative arts department. Sanaa yoyote lazima iende mtandaoni ili ifikie audience.
 
Hao wameweza kwa sababu kuna watu wamewabeba
Vile vile wapo ktk industry muda mrefu.
Baba levo ni mwanamuziki muda mrefu hivyo anajua anachokifanya.
Bsba levo ma mwijaku ni kama wanatumiwa na media hawana chanel za maana ispkuwa Milard.
 
Usikalili

Twenda taratibu

Umesema Mc garab kasoma kigurunyembe si ndio. Naamini kwenye darasa lao hakumaliza pekee yake, swali kwako aliomaliza nao nao ni maMC wakubwa?

Turudi kwa Ayo.

Watu wote walioishia elimu ya cheti kwenye uandishi wa habari je wote wanamablog na social media kubwa kubwa?
 
Kudharau elimu kwa sababu wewe imeshindwa kukusaidia ni kosa moja kubwa sana.
Hata hao mnaowaita form four failures kuna mahali wanaufyata mdomo na kuwaacha wasomi wafanye taaluma yao.
Kama unahisi elimu ni ghali na mzigo basi jaribu ujinga.
 
Mimi sijasomea taaluma za kutawala mtandaoni. Ndio maana nimeuliza graduates wenye taaluma ama tabia zinazoruhusu kutawala mitandaoni nilizozitaja kwenye uzi.

Pia maendeleo yangu sio haba kwa mtu mwenye age yangu.

Mimi ninamiliki rums za kupangisha zaidi ya 30. Plus Viwanja kazaa

Na safari bado inaendelea..

Nadhani influencers wengi waliosoma wapo Twitter na linkedin kwa sababu huko kuna audience ambayo ipo serious zaidi

Lakini ukiangalia watu maarufu au influencers waliopo katika siasa au corporate world kama zitto au kelvin twissa ni wasomi wazuri sanaa

Lakini hata katika entertainment watu maarufu waliofika hata chuo wapo wengi ila hawaweki sana elimu mbele maana kipaji ndio kimewafikisha hapo mfano Mimi Mars, Nikki wa pili, Jokate, Faraja Kotta, Nancy Sumari, Mwana Fa, Zuchu, Maua Sama, deo etc
 
Mwenye kudharau ilmu binfsi huwa namuonea tu huruma!

Msisahau huyo Millard pamoja na hapo alipofika ni wasomi kawaajili wanamfanyia kazi

Anao content developers
Anao graphics designers
Anao sound editors
Anao video producers and video editors

In short anamiliki kampuni iliyokamilika na inayoendeshwa kama inavyotakiwa

Yeye alipata wazo + capital mengine mengi sasa yanayaendelea sio mawazo yake tena Bali ya watu tena wenye taaluma zao walioajiliwa na kampuni.

Sent from my phone

Na watu wakubwa ambao wamefikisha sanaa au kuwapush hao tunaowaona kama successful stories ni wasomi kiasi pia mfano Ruge na Seven Mosha, wote shule zipo

Kiufupi elimu haikupi mafanikio ila inarahisisha kuyapata

Na kingine wasanii wengi sana kama diamond au ali kiba kufeli kwao kunawasaidia muda wa kupambania kipaji.
Imagine mtu ni form four failure, ananda kupambana mara THT au studios kwa miaka hata mitano ndo anakuja kutoka, sasa graduate unamaliza hata na 23 or 24 ndio uanze kupambana kwenye entertainment 🤦🏽‍♂️🤦🏽‍♂️🤦🏽‍♂️

Itahitajika bahati kufika pakubwa, naamini hata Idris asingefika hapo alipo kama angeendelea na degree ya udaktari. Aliishia form six, akaanza kupambana
 
Back
Top Bottom