Wahitimu wa Vyuo mnakwama wapi? Kina Millard Ayo, MC Garab, Babu Tale, Hamissa Mobetto wanakimbiza kutawala fursa za social media

Wewe Binafsi umefanikiwaje huko?

Mimi sijasomea taaluma za kutawala mtandaoni. Ndio maana nimeuliza graduates wenye taaluma ama tabia zinazoruhusu kutawala mitandaoni nilizozitaja kwenye uzi.

Pia maendeleo yangu sio haba kwa mtu mwenye age yangu.

Mimi ninamiliki rums za kupangisha zaidi ya 30. Plus Viwanja kazaa

Na safari bado inaendelea..
 
Okay, vizuri.

Ila kwani hao graduate wamesomea hizo taaluma za kutawala mitandaoni Kweli?

Je hizo taaluma za kutawala mitandaoni zinafundishwa huko vyuoni?
 
Ni wenzetu, wanatuwakilisha, kwa pamoja tunasema, fani inalipa
 
Okay, vizuri.

Ila kwani hao graduate wamesomea hizo taaluma za kutawala mitandaoni Kweli?he hizo taaluma za kutawala mitandaoni zinafundishwa huko vyuoni?

Journalism ni mojawapo lazima iende mtandaoni ili kusambaza habari.

Taaluma za creative arts department. Sanaa yoyote lazima iende mtandaoni ili ifikie audience.
 
Hao wameweza kwa sababu kuna watu wamewabeba
Vile vile wapo ktk industry muda mrefu.
Baba levo ni mwanamuziki muda mrefu hivyo anajua anachokifanya.
Bsba levo ma mwijaku ni kama wanatumiwa na media hawana chanel za maana ispkuwa Milard.
 
Usikalili

Twenda taratibu

Umesema Mc garab kasoma kigurunyembe si ndio. Naamini kwenye darasa lao hakumaliza pekee yake, swali kwako aliomaliza nao nao ni maMC wakubwa?

Turudi kwa Ayo.

Watu wote walioishia elimu ya cheti kwenye uandishi wa habari je wote wanamablog na social media kubwa kubwa?
 
Unaweza Kuta mtoa mada ni muhitimu wa shahada ya uandishi wa habar ila hana kazi.
 
Kudharau elimu kwa sababu wewe imeshindwa kukusaidia ni kosa moja kubwa sana.
Hata hao mnaowaita form four failures kuna mahali wanaufyata mdomo na kuwaacha wasomi wafanye taaluma yao.
Kama unahisi elimu ni ghali na mzigo basi jaribu ujinga.
 

Nadhani influencers wengi waliosoma wapo Twitter na linkedin kwa sababu huko kuna audience ambayo ipo serious zaidi

Lakini ukiangalia watu maarufu au influencers waliopo katika siasa au corporate world kama zitto au kelvin twissa ni wasomi wazuri sanaa

Lakini hata katika entertainment watu maarufu waliofika hata chuo wapo wengi ila hawaweki sana elimu mbele maana kipaji ndio kimewafikisha hapo mfano Mimi Mars, Nikki wa pili, Jokate, Faraja Kotta, Nancy Sumari, Mwana Fa, Zuchu, Maua Sama, deo etc
 

Na watu wakubwa ambao wamefikisha sanaa au kuwapush hao tunaowaona kama successful stories ni wasomi kiasi pia mfano Ruge na Seven Mosha, wote shule zipo

Kiufupi elimu haikupi mafanikio ila inarahisisha kuyapata

Na kingine wasanii wengi sana kama diamond au ali kiba kufeli kwao kunawasaidia muda wa kupambania kipaji.
Imagine mtu ni form four failure, ananda kupambana mara THT au studios kwa miaka hata mitano ndo anakuja kutoka, sasa graduate unamaliza hata na 23 or 24 ndio uanze kupambana kwenye entertainment πŸ€¦πŸ½β€β™‚οΈπŸ€¦πŸ½β€β™‚οΈπŸ€¦πŸ½β€β™‚οΈ

Itahitajika bahati kufika pakubwa, naamini hata Idris asingefika hapo alipo kama angeendelea na degree ya udaktari. Aliishia form six, akaanza kupambana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…