SoC01 Wahitimu wa Vyuo na Maisha ya utafutaji Mtaani

SoC01 Wahitimu wa Vyuo na Maisha ya utafutaji Mtaani

Stories of Change - 2021 Competition

Theb

JF-Expert Member
Joined
Jan 25, 2019
Posts
3,927
Reaction score
7,276
Habari zenu wana Jamii Forums, hususani jukwaa hili la "Stories of Change". Ni tumaini langu wote ni wazima.

Andiko hili litaangazia maisha ya vijana wahitimu wa vyuo waliotegemea kuajiriwa na hali imekua tofauti na matarajio yao. Mwanzo, nitaelezea maisha ya mtaani, changamoto zinazo wakabili na vipi watatue hizo changamoto, Pili, nitaelezea fursa zisizohitaji mitaji na zenye kuhitaji mitaji. Tatu, nitaelezea mchango wa serikali na sekta binafsi katika kuwasaidia vijana kupata ajira na kujiajiri. Mwisho, nitamalizia kwa kutoa ushauri wangu katika kuwawezesha vijana wahitimu kujikwamua.

Maisha ya mtaani katika jamii zetu karibia kote yana mfanano kwa asilimia kubwa. Kuanzia ngazi ya familia za wahitimu walio wengi zinafanana kiuchumi, kitamaduni na hata kimalengo. Familia nyingi katika jamii zetu Tanzania tunasoma ili tuajiriwe na sio kujiajiri kwa waliowengi, hali iliyopo kwa sasa imeenda kinyume na malengo na matarijio ya vijana waliokuwa wanasoma na wanaoendelea kusoma mashuleni mpaka vyuoni.

CHANGAMOTO ZINAZO WAKABILI VIJANA WAHITIMU KATIKA UTAFUTAJI.

1. Kushindwa kujiamini na kushindwa kuikubali hali halisi iliyopo. Wengi wameshindwa kujiamini na kufikiria nje ya kitu walichosomea na kuanza kitu kipya ina wawia ngumu.

2. Mazingira yanayo wazunguka wahitimu, jamii ina wapa wakati mgumu kwa kuwahukumu kuwa wamesoma bure, elimu yao haina faida. Hili sio sawa.

3. Ukosefu wa muunganiko baina ya wahitimu na waliotangulia kwenye utafutaji, hapa unakuta wahitimu hawana muunganiko na waliotangulia kwenye utafutaji mitaani.

4. Ukosefu wa mitaji, hususani kwenye biashara au fursa zinazohitaji mitaji.

5. Kukosa uelewa katika utafutaji wenyewe. Kutozijua fursa au kutozitambua biashara na majira yake. Maana kila biashara ina majira yake.

6. Kuchagua kazi. Baadhi ya wahitimu hii changamoto kubwa kwao. Hawako tayari kubeba hata mizigo wanaona aibu au wanaona haiba yao hawastahili kubeba mizigo.

7. Mfumo na mitaala ya elimu nchini haikidhi dhumuni la kujiajiri kwa sababu imejikita katika nadharia zaidi na sio hali halisi katika kujiajiri.

JINSI YA KUPAMBANA NA HIZO CHANGAMOTO:-

1. Wazazi wasaidie watoto wao kuchagua fani zitakazo wawezesha kujiajiri pindi watakapo hitimu vyuoni.

2. Kujikubali, kujitambua na kujichanganya na watafutaji wengine mitaani bila kuwaza au kujutia muda uliopoteza shuleni na vyuoni.

3. Kukubali hali halisi hususani kuwa tayari kwa kazi yoyote bila kuchagua kazi. Mfano baadhi ya wahitimu ni ngumu kufanya kazi kama kuuza mkaa au kununua chupa za plastiki zilizotumika kwa kuhofia taaluma yake au watu watamuonaje.

4. Kuzitambua fursa na kuwa tayari kupambana nazo maana utafutaji mtaani ni ushindani.

5. Kufanya uchunguzi wa biashara unayotaka kwenda kuanzisha, hapa itahitaji kutafiti kwa kile unachotaka kufanya mtaani.

6. Kupunguza matumizi yale yasiyo muhimu. Kuwa na matumizi sahihi ya fedha. Mfano waache unywaji wa pombe, kubet, uvutaji wa sigara au ulevi wowote na anasa zingine zinazo hitaji pesa.

7. Kufanya uchaguzi sahihi wa kile unachoweza kukifanya mtaani na sio kufuata mkumbo. Fanya unachokipenda na unachokiweza

8. Usisahau kutunza kile unachokipata hata kama kidogo. (Bandu bandu humaliza gogo)

FURSA ZINAZOWEZA KUSAIDIA WAHITIMU KATIKA UTAFUTAJI MTAANI

1. Fursa zisizo hitaji mitaji na zisizo hitaji mitaji mikubwa sana. (Hizi kwa ajili ya kuanza kujipatia mitaji kidogo kidogo)

(i) Vibarua viwandani
Kwa wale wahitimu waliopo mijini kuna viwanda, vipo vibarua vya kutwa na wale wanaolipwa kwa wiki viwandani. Kuna kubeba mizigo viwandani kupakia na kupakua mizigo inayoingia na inayotoka na kazi zingine kulingana na kiwanda husika.

(ii) Fursa kwenye standi za mabasi ya abiria
Pia kwenye standi za mabasi kuna baadhi ya fursa zisizohitaji mitaji au zinazohitaji mitaji midogo. Mfano kubeba mizigo ya abiria kuwa wakala wa kukata tiketi na kuunza bidhaa ndogo ndogo kama karanga maji, juisi na matunda.

(iii) Kununua plastiki na kwenda kuziuza
Hapa kuna hii fursa ya kununua plastiki na kwenda kuuza mfano kilo moja unanunua kuanzia 300 hadi 400 na kuuza iliyosagwa ni kuanzia 800 hadi 1200 isiyo sagwa ni 800 bei ya kuuza. Hii ni fursa japo inadharauliwa.

(iv) Kuwa dalali wa mazao shambani au magari ya kusafirisha mizigo au dalali wa nyumba na viwanja
Haihitaji mtaji kwenye kuanza uaminifu wako na kujua chimbo za unachofanya ndio mtaji wako.

(v) Kuanzisha twisheni (tuition) mtaani kwenu
Hii pia saa zingine haihitaji mtaji itahitaji tu utayari wako na uwepo wa wanafunzi wanaosoma na kuitangaza. Japo maeneo mengine hii haina nafasi maana muitiko unakua mdogo hasa vijijini.

(vi) Kubeba mizigo kwenye masoko kupakua na kupakia mazao na bidhaa mbalimbali
Tunaweza kuidharau lakini ni fursa ukibeba mizigo 25 yenye kulipwa 1000 kila mzigo kwa siku una shilingi 25000. Haitaki mtu mwenye aibu na usharobaro.

(v). Kipaji kiwe cha uandishi, uimbaji, ususi, uchoraji, na michezo
Kipaji pia ni fursa kubwa tena isiyo hitaji mtaji ila inahitaji utayari wako kujituma na ubunifu zaidi na uvumilivu uliomithilika.

(vi). Kuwa saidia fundi ujenzi, fundi wa kuchomelea dirisha na mageti, fundi randa nk,

Kusaidia fundi atakulipa kidogo itategemea na kazi iliyopo hapo unajifunza ufundi, kujiandaa kuwa fundi ili ujitegemee. Mfano saidia fundi ujenzi hulipwa sio chini ya 10,000/= kwa siku.

(vii). Kuuza mahindi ya kuchoma na ya kuchemsha.
Hii hususani sehemu zenye mikusanyiko, stand za mabasi, barabarani na kwenye vyombo vya usafiri hususani mabasi.

2. Fursa zinazohitaji mitaji mikubwa au ya kiasi. Nitataja baadhi na ambazo ni rahisi kuzitambua kama ifuatavyo:-

(i). Kununua mazao mashambani na kuleta mjini kwenye masoko
Hapa kuna mahindi, viazi aina zote, mchele mboga mboga kutoka mashambani kuleta mijini. Kikubwa kufanya tathmini vizuri.

(ii). Umachinga wa kuuza vitu mtaani kando ya barabara au kutembeza au kutengeneza banda lako sehemu inayoonekana kwa wateja

(iii). Kilimo, uvuvi na ufugaji

Kilimo kinahitaji uwe na shamba, mbegu, pembejeo za kilimo mbolea na dawa za kupulizia kuua vijidudu hatarishi kwa mazao nacho kilimo kitategemea na aina ya mazao unayolima.

Ufugaji
Mfano wa kuku lazima uwe na mtaji wa kununua kuku, pumba, uduvi na mifupa.

(iv). Udereva boda boda au bajaji
Huu nao utahitaji uwe na mtaji au upate ya mtu. Mfano bado boda hakosi kupata 25000 hadi 30000 kwa siku.

(v). Kuanzisha saloon zote za kunyoa nywele na kusuka nywele
Hapa kwa wanaume na kwa wanawake kuna kunyoa na kusuka hivyo sehemu uliyopo ikiwa na uhitaji hii ni fursa.

(vi). Huduma ya kutuma pesa kwa njia za simu.
Kuanzisha M pesa, airtel money, tigo pesa na halopesa.

(vii). Kuanzisha mgahawa, mama ntilie au ukaangaji wa chipsi na kuchoma mishkaki.

(viii). Kununua na kuuza vyuma chakavu. Hii pia ni fursa inayolipa vizuri ni jambo la kufanya uchunguzi na kuthubutu.

MCHANGO WA SERIKALI PAMOJA NA SEKTA BINAFSI KATIKA KUWASAIDIA WAHITIMU.

1. Kuwapa motisha, semina na muongozo wa namna ya kuanza ujasiriamali.

2. Kuwapatia mikopo yenye riba nafuu au isiyo na riba kabisa.(walemavu wapewe kipaumbele).
Serikali na sekta binafsi kupitia benki na taasisi zingine za kifedha watoe mikopo kwa wahitimu. Pia familia zenye uwezo ziwawezeshe vijana wao waliohitimu.

3. Mazingira wezeshi kwa watafutaji wanaoanza kutafuta mtaani. Hapa kuwaondolea kodi kandamizi. Kuboresha miundo mbinu zaidi mijini na vijijini itasaidia usafirishaji wa bidhaa.

4. Serikali itengeneze mahusiano mazuri na mataifa mengine. Itasaidi kutanua soko la nje kwenye ajira na bidhaa au mazao yatakayo zalishwa nchini.

5. Serikali na sekta binafsi zinapaswa kwa pamoja kuwaamini vijana na kuondoa kigezo cha uzoefu katika kuwapatia kazi/ajira.

6. Serikali na sekta binafsi ziwashirikishe vijana katika juhudi za kuwainua iwe mikopo au semina za kiujasiriamali.

7. Mfumo wa elimu uboreshwe hususani mitaala. Elimu itolewe kwa vitendo na ijikite katika kuwaandaa kujitegemea/kujiajiri.

8. Wazazi, jamii, serikali na mashirika binafsi kwa pamoja watambue na kudhamini karama au vipaji vya wanafunzi toka wakiwa wadogo na kuvisimamia kwa lengo la kujiajiri baadae.

9. Wahitimu wote wenye ulemavu wapatiwe kazi serikalini na mashirika binafsi moja kwa moja. Mfano ajira za mwaka 2021 ualimu na afya serikali haikuwaacha nyuma hili liendelee kila wakati.

10.Kuwe na uwazi katika masuala ya ajira. Iwe za serikali mpaka mashirika binafsi.

11. Ukabila, rushwa, umaeneo na udini viepukwe katika kuwapatia vijana ajira.

12. Waliofikia umri wa kustaafu wasiruhusiwe kuendelea kufanya kazi.

13. Uwepo mgawanyo wa kazi.
Ili mtu mmoja asifanye kazi zaidi ya kituo kimoja.

USHAURI WANGU KWA VIJANA WAHITIMU KATIKA UTAFUTAJI
Ushauri wangu kwa vijana wasaka tonge wahanga wa ajira na vijana woote watafutaji kwa ujumla napenda kutoa ushauri kama ifuatavyo:-

(i). Uvumilivu kwenye hizo fursa tunazoenda kuanzisha maana nako pia tutakutana na changamoto ila tusivunjike moyo na tusikate tamaa mapambano yaendelee.

(ii). Tuzijue hizo fursa na kutambua majira ya hizo fursa itasaidia kutambua muda gani muafaka wa kuanza tusikurupuke kuna kuanguka pia.

(iii). Kama unamtaji usianze na pesa yote ya mtaji maana hauna uhakika 100% kuwa itaenda sawa hivyo kujipanga kwa hilo ni muhimu.

(iv). Kupata ushauri kwa waliofanikiwa ni muhimu itakuongezea maarifa kwa yale usiyo yajua.

(v). Usimuamini kila mtu katika utafutaji wako wengine watakukwamisha. Mfano wanao kopa ni sumu kwako unaeanza utafutaji.

(vi). Tambua hitaji la jamii ikizungukayo. Kama jamii inataka mahindi wapelekee mahindi na sio mchele.

(vii). Ishi vizuri na watu na waheshimu watu kwa imani zao makabila yao na rangi zao. Kuwa na lugha nzuri.

(viii). Zingatia usafi kwenye ofisi yako kuwa na mpangilio mzuri pia toa huduma iliyo bora sio bora huduma.

(ix). Muhimu na la kukumbukwa kila unapopata kidogo kitunze kadri kinavyo kua kiwekeze kitaleta zaidi.

(X). Fanya shughuli halali, kuwa muaminifu, uadilifu ni muhimu na kufuata sheria za nchi yetu katika utafutaji.
 
Upvote 1.6K
Shukran mkuu na Amina kubwa. Vijana mkuje fursa imejileta yenyewe. Na vipi mkuu unaweza waambia sifa za unaohitaji na umri, elimu, nk ili wajue wapi pakuanzia.
Nashukuru sana!

Kwa upande wa hii biashara yetu kimsingi tunahitaji mambo machache sana, na vigezo vyake ni rahisi kama muhusika ana nia ya kweli.

1. Kujitambua
Katika hili tunahitaji mtu ambaye anajitambua na anatambua ni kwanini yupo mahala fulani ili aweze kujisimamia mwenyewe katika utekelezaji wake wa majukumu.

2. Kujitoa/Commitment
Hapa ni vile atakavyojitoa katika utafutaji/utendaji wake kwani biashara hii itampa nafasi ya kubuni njia zake za kuwafikia wadau/wateja baada ya kupatiwa mwongozo wa mahitaji ya Mradi kwa watendaji/mawakala.

3. Elimu na Umri
Kutokana na wimbi la ukosefu wa ajira na asili ya biashara yetu hii, Elimu ni ya ngazi yeyote na fani yeyote (kikubwa ni kujua kusoma, kuandika na kujieleza kiasi). Umri angalau uwe zaidi ya miaka 18.

NB: Ushawishi na lugha nzuri mkwa wateja ni nguzo bora sana katika biashara hii, lakini pia kuwa na nidhamu ya kile unachokifanya kwani jinsi utakavyojiweka wewe ndivyo wadau/ wateja watakavyokupokea.

Nadhani nitakuwa nimejibu au angalau nimeongeza kitu, naomba niwakaribishe ndugu zangu.
 
Shukran mkuu. Nikuulize jambo lingine kwa upande wangu. Je mnawapatia mkataba ai inakua ni makubaliano ya mdomoni tu kawaida.
 
Shukran mkuu. Nikuulize jambo lingine kwa upande wangu. Je mnawapatia mkataba ai inakua ni makubaliano ya mdomoni tu kawaida.
Nashukuru sana kwa swali!

Mikataba kama mikataba ya makubaliano ipo, na mara zote kabla ya kuafikiana jambo lazima kuna mawasiliano ambayo kwayo mnakubaliana ni namna gani mtaiendea kazi husika hasa ikiwa ya maandishi mfano sms, emails, nk. Nayo ni sehemu ya Mkataba

Ila kwa asili ya biashara ilivyo, Kuna njia kadhaa rafiki ambazo kwa namna moja ama nyingine itakubidi ufike kwenye mradi na mteja wako, au kama ukiwa huna nafasi kuna njia ya kutrack na kupata mrejesho kamili kupitia Sisi wenye mradi, na mteja wako kama mnufaika.

Na kikubwa ni Uaminifu tuu, maana sote tunatafuta Na ndio maana tunatafuta watu wa kufanya nao kazi ili tufanikiwe kama timu.

Ila kama inaafikiwa na wakala, anapendekezwa atembelee mradi na kuona ni namna gani miradi inaendeshwa ili kujiridhisha na baada ya hapo ndio tunakubaliana kufanya kazi.
 
Vzr. Nimependa maelezo yako yapo wazi na hayana ukakasi ikiwa kila kitu kipo kama unavyosema basi nawashauri vijana wakufwate PM kwa mengi zaidi japo hata hapa wanaweza kukuuuliza chochote kwa faida ya wengi wenye kutaka kujua.
 
Salaam mkuu tunaomba tujuzwe na sie huenda tukaunga timu liwe kubwa. [emoji1][emoji120][emoji120]
 
Nashukuru sana
 
Nashukuru sana
Shukran saana kwa mchango wako uliohalisi na fursa kwa vijana watafutaji. Na wakiuliza hapa mkuu usisite kuwapa kinaubaga juu ya jambo lako hilo [emoji1317][emoji1317][emoji1303]
 
Nashukuru sana!

Kwa upande wa hii biashara yetu kimsingi tunahitaji mambo machache sana, na vigezo vyake ni rahisi kama muhusika ana nia ya kweli.

1. Kujitambua
Katika hili tunahitaji mtu ambaye anajitambua na anatambua ni kwanini yupo mahala fulani ili aweze kujisimamia mwenyewe katika utekelezaji wake wa majukumu.

2. Kujitoa/Commitment
Hapa ni vile atakavyojitoa katika utafutaji/utendaji wake kwani biashara hii itampa nafasi ya kubuni njia zake za kuwafikia wadau/wateja baada ya kupatiwa mwongozo wa mahitaji ya Mradi kwa watendaji/mawakala.

3. Elimu na Umri
Kutokana na wimbi la ukosefu wa ajira na asili ya biashara yetu hii, Elimu ni ya ngazi yeyote na fani yeyote (kikubwa ni kujua kusoma, kuandika na kujieleza kiasi). Umri angalau uwe zaidi ya miaka 18.

NB: Ushawishi na lugha nzuri mkwa wateja ni nguzo bora sana katika biashara hii, lakini pia kuwa na nidhamu ya kile unachokifanya kwani jinsi utakavyojiweka wewe ndivyo wadau/ wateja watakavyokupokea.

Nadhani nitakuwa nimejibu au angalau nimeongeza kitu, naomba niwakaribishe ndugu zangu.
Mkuu kuna mtu kana PM anatafuta kazi sasa namleta kwako huyu hapa kama mtaelewana na mtafikia makubaliano na kazi akiielewa itapendeza Donkiwango
Mkuu Donkiwango kutana na ndugu huyu mwenye mchongo na kauelezea hapa zaidi unaweza kumfuata PM mkawasiliana vzr zaidi[emoji1317][emoji1317]
 
Salaam mkuu tunaomba tujuzwe na sie huenda tukaunga timu liwe kubwa. [emoji1][emoji120][emoji120]
Ushajuzwa hapo juu ndugu ni.wewe sasa ukaribie kama umemuelewa na upo tayri
 
Vipi andiko ni special kwa wahitimu tu.?
Andiko nimeweka kuwakazia wahitimu lakini maelezo ukiyasoma yanaweza kutumika na mtu yeyote awe muhitimu awe mtu yeyote ili mradi tu awe mtafutaji hususani anae anza kutafuta.

Hata alietafuta akadondoka ni wazi huu uzi unaweza kumsaidia kwa kuwa unaelezea zaidi kuhusu fursa ambazo tunaseza kuzipata ndani ya maisha tunayoishi na mitaa yetu.. [emoji1317][emoji1317]
 
Sawa. Maisha ni magumu hasa kwa vijana wasio na ajira kwa sasa. Lakini vijana wenyewe pia ni changamoto hawataki kuelekezwa kwa wasicho kijua, wasichokuwa na uelewa nacho hawapendi kuonekana hawajui wanajikweza. Hili tuliongelee nalo nadhani lina umuhimu kwa hao wahitimu
 
Jambo zuri kuonesha changamoto waliyonayo wahitimu kwaza shukrani mkuu[emoji1317]

Katika ushauri juu kwenye andiko nadhani niliandika vijana wakubaki kupewa ushauri na kwenye utatuzi wa changamoto nakumbuka hili nako nimelipa maelezo kiasi. Ila acha niliweke tena sawa hapa.

Kwa vijana wahitimu mnaoanza utafutaji msijikweze maana hata vitabu vya dini vimesema ajikwezae atashushwa. Na pia kukishusha kutakufaidisha katika kuyajua mengi zaidi kwenye utafutaji. Tena ikiwezekana km ni.ugenini kijana muhitimu wasijue kuwa wewe ni mhitimu mwenye degree hii itakusaidia kuwa sawa nao bila wao kuwa na reaction yoyote hasi kwako.
 
Habari zenu wana Jamii Forums, hususani jukwaa hili la stories of change. Ni tumaini langu nyote ni wazima.

Andiko hili litaangazia maisha ya vijana wahitimu wa vyuo waliotegemea kuajiriwa na hali imekua tofauti na matarajio yao.

Naanza kwa kuelezea maisha ya mtaani na baadhi ya fursa zenye kuhitaji mitaji na zisizohitaji mitaji na changamoto zake na vipi tunaweza kuzikabili changamoto na kutuwezesha kupita katika baadhi ya hizo fursa na tuweze kujikwamua.

Maisha ya mtaani katika jamii zetu karibia kote yana mfanano kwa asilimia kubwa. Kuanzia ngazi ya familia za wahitimu walio wengi zinafanana kichumi kitamaduni na hata kimalengo. Familia nyingi za jamii zetu Tanzania tunasoma ili tuajiriwe na sio kujiajiri kwa waliowengi, hali iliyopo kwa sasa sio siri imeenda kinyume na malengo na matarijio ya vijana waliokuwa wanasoma na wanaoendelea kusoma mashuleni mpaka vyuoni.

NITAANZA KUELEZEA CHANGAMOTO ZINAZO WAKABILI VIJANA WAHITIMU KATIKA UTAFUTAJI.

1. Kutokujiamini na kutokubaliana na hali halisi iliyopo. Wengi hawa jiamini na wanashindwa kufikiria nje ya kitu walichosomea na kukianza kitu kipya ina wawia ngumu.

2. Mazingira yanoyowazunguka wahitimu, jamii ina wapa wakati mgumu kwa kuwahukumu kuwa wamesoma bure, elimu yao haina faida. Hili sio sawa.

3. Kukosa kampani au muunganiko na watu waliotangulia kwenye mitaa, hapa unakuta wahitimu hawana muunganiko na waliotangulia kwenye mitaa kiutaftaji. Japo hio sio sana.(lack of support)

4. Kutokua na mitaji, hususani kwenye biashara au fursa zinazohitaji mitaji.

5. Kutokua na uelewa wa mitaa na utaftaji wenyewe. Yaani kutozijua fursa au kutozitambua biashara na majira yake. Maana kila biashara ina majira yake.

6. Kuchagua kazi. Hii inahusika saana baadhi ya wahitimu hii changamoto kubwa kwao. Hawako tayari kubeba hata gunia wanaona aibu au wanaona haiba yao hawastahili kubeba gunia.

JINSI GANI WANAWEZA KUPAMBANA NA HIZI CHANGAMOTO:-

1. Kujikubali na kujichanganya na watafutaji wengine mitaani bila kuwaza au kujutia muda uliopoteza shuleni na vyuoni.

2. Kukubali hali halisi hususani kuwa tayari kwa kazi yoyote bila kuchagua kazi. Mfano baadhi ya wahitimu ina muwia ngumu kufanya kazi kama kuuza mkaa au kununua chupa za plastiki zilizotumika kwa kuhofia taaluma yake au watu watamuonaje.

3. Kuzitambua fursa na kuwa tayari kupambana nazo maana utaftaji mtaani ni ushindani.

4. Kuyajua mazingira ya biashara unayotaka kwenda kuanzisha, hapa itahitaji muunganiko na wanaoitambua biashara husika unayotaka kuanzisha kwenye mazingira unayopanga.

5. Kupunguza matumizi yale yasiyo muhimu, hapa matumizi yale yasiyomuhimu ambayo yanafuja pesa hainabudi kuyaacha. Mfano unywaji wa pombe, kubet, uvutaji wa sigara au ulevi wowote na anasa zingine zinazo hitaji pesa.

6. Kufanya uchaguzi sahihi wa kile unachoweza kukifanya mtaani na sio kufwata mkumbo. Je mhitimu unaweza kitu gani kama ni kilimo basi fanya kilimo kama ni ufundi fanya ufundi.

7. Usisahau kutunza kile unachokipata hata kama kidogo. (Bandu bandu humaliza gogo)

FURSA ZILIZOPO KATIKA JAMII ZETU AMBAZO WAHITIMU AU MTAFUTAJI YEYOTE ANAWEZA KUZITAZAMA NA KUANZA KUJIPATIA KIPATO KUPITIA HIZO FURSA

1. Fursa zisizo hitaji mitaji na zisizo hitaji mitaji mikubwa sana. (Hizi kwa ajili ya kuanza kujipatia mitaji kidogo kidogo)

(i) Vibarua viwandani
Kwa wale wahitimu waliopo mijini kuliko na viwanda kuna upatikanaji wa vibarua wa kutwa na wale wanaolipwa kwa wiki kwenye viwanda. Kuna kubeba mizigo viwandani kupakia na kupakua mizigo inayoingia na inayotoka na kazi zingine kulingana na kiwanda husika.

(ii) Fursa kwenye standi za mabasi ya abiria
Pia kwenye standi za mabasi kuna baadhi ya fursa zisizohitaji mitaji au zinazohitaji mitaji midogo, mfano kubeba mizigo ya abiria kuwa wakala wa kukata tiketi na kuunza bidhaa ndogo ndogo kama karanga maji, juisi na matunda.

(iii) Kununua plastiki na kwenda kuziuza
Hapa kuna hii fursa ya kununua plastiki na kwenda kuuza mfano kilo moja unanunua kuanzia 300 hadi mia 400 na kuuza iliyosagwa ni kuanzia 800 hadi 1200 isiyo sagwa ni 800 bei ya kuuza. Hii ni fursa japo inadharauliwa.

(iv) Kuwa dalali wa mazao shambani au magari ya kusafirisha mizigo au dalali wa nyumba viwanja nk
Hii nayo haihitaji mtaji kwenye kuanza uaminifu wako na kujua chimbo za unachofanya ndio mtaji wako.

(v) Kuanzisha twisheni (tuition) mtaani kwenu
Hii pia saa zingine haihitaji mtaji itahitaji tu utayari wako na uwepo wa wanafunzi wanaosoma na kuitangaza. Japo maeneo mengine hii haina nafasi maana muitiko unakua mdogo hasa vijijini.

(vi) Kubeba mizigo kwenye masoko kupakua na kupakia mazao na bidhaa mbalimbali
Tunaweza kuidharau lakini ni fursa ukibeba mizigo 25 yenye kulipwa 1000 kila mzigo kwa siku una shilingi 25000. Inafaa japo haitaki mtu mwenye aibu na usharobaro.

(v). Kipaji kiwe cha uandishi, uimbaji, ususi, uchoraji, na michezo
Kipaji pia ni fursa kubwa tena isiyo hitaji mtaji ila itataka utayari wako kujituma na ubunifu zaidi na uvumilivu uliomithilika.

(vi). Kuwa saidia fundi ujenzi, fundi wa kuchomelea dirisha na mageti, fundi randa nk, (Ufundi wa aina yoyote).

Kusaidia fundi atakulipa kidogo itategemea na kazi iliyopo hapo hapo unajifunza ufundi, kujiandaa kuwa fundi ili ujitegemee. Mfano saidia fundi ujenzi hulipwa sio chini ya 10,000/= kwa siku.

(vii). Kuuza mahindi ya kuchoma na ya kuchemsha.

Hii hususani sehemu zenye mikusanyiko, stand za mabasi barabarani na kwenye vyombo vya usafiri hususani mabasi.

2. Fursa zinazohitaji mitaji mikubwa au ya kiasi. Nitataja baadhi na ambazo ni rahisi kujichanganya kama ifuatavyo:-

(i). Kununua mazao mashambani na kuleta mjini kwenye masoko
Hapa kuna mahindi, viazi aina zote, mchele mboga mboga kutoka mashambani kuleta mijini. Kikubwa kufanya tathmini vizuri.

(ii). Umachinga wa kuuza vitu mtaani kando ya barabara au kutembeza au kutengeneza banda lako sehemu inayoonekana kwa wateja

(iii). Kilimo, uvuvi na ufugaji

Kilimo kinahitaji uwe na shamba, mbegu, pembejeo za kilimo kama mbolea na dawa za kupulizia kuua vijidudu hatarishi kwa mazao nacho kilimo kitategemea na aina ya mazao unayolima. Uvuvi pia utahitaji mtaji kununua nyavu nk.

Ufugaji
Mfano wa kuku lazima uwe na mtaji wa kununua kuku, pumba, uduvi na mifupa. Hii ni baadhi ya mifano.

(iv). Udereva boda boda au bajaji
Huu nao utahitaji uwe na mtaji au upate ya mtu. Mfano bado boda hakosi kupata 25000 hadi 30000 kwa siku.

(v). Kuanzisha saloon zote za kunyoa nywele na kusuka nywele
Hapa kwa wanaume na kwa wanawake kuna kunyoa na kusuka hivyo sehemu uliyopo kama pana uhitaji hii ni fursa.

(vi). Huduma ya kutuma pesa kwa njia za simu.
Kuanzisha M pesa, airtel money, tigo pesa na halopesa.

(vii). Kuanzisha mgahawa, mama ntilie au ukaangaji wa chipsi na kuchoma mishkaki.

(viii). Kununua na kuuza vyuma chakavu. Hii pia ni fursa inayolipa vizuri ni jambo la kufanya uchunguzi na kuthubutu.

MAMBO YANAYO WEZA KUTEKELEZWA NA SERIKALI PAMOJA NA SEKTA BINAFSI KUWASAIDIA VIJANA WAHITIMU.

1. Kuwapa motisha na muongozo wa kuanzisha vikundi vya ujasiriamali. Hapa serikali inapaswa kuwa mhusika mkuu wakuwapa vijana wasio na kazi usaidizi.

2. Kuwapatia mikopo yenye riba nafuu au isiyo na riba kabisa. (Bajeti ya kila mwaka iwepo kiasi cha kuwasaidia)

Serikali na sekta binafsi kupitia benki na taasisi zingine za kifedha wanaowajibu wakuwawezesha kwa mikopo isiyo na riba

3. Mazingira wezeshi kwa watafutaji wanaoanza kutafuta mtaani. Serikali inapaswa kuwawekea mazingira mazuri vijana wanaoanza utafutaji kwa maana itasaidia kuwa inua. Hapa kuwaondolea kodi kandamizi.

4. Kuwapatia semina mbali mbali za kiujasirimali. Hapa lazima kuwapa semina juu ya fursa zilizopo na vipi wataweza kukabiliana na changamoto katika utafutaji.

5. Serikali na sekta binafsi zinapaswa kwa pamoja kuwaamini vijana na kuondoa kigezo cha uzoefu katika kuwapatia kazi.

6. Serikali na sekta binafsi kuwa husisha vijana katika juhudi za kuwainua iwe mikopo au semina za kiujasiriamali.

7. Mfumo wa elimu uboreshwe hususani mitaala iwe rahisi kuwa andaa vijana kujitegemea kulingana na elimu waipatayo.

8.Kuwe na uwazi katika masuala ya ajira. Iwe za serikali mpaka mashirika binafsi uwazi uwepo.

9. Ukabila, rushwa, umaeneo na udini viepukwe katika kuwapatia vijana ajira.

10. Waliofikia umri wa kustaafu wasiruhusiwe kuendelea kufanya kazi.

11. Uwepo mgawanyo wa kazi.

Ili mtu mmoja asifanye kazi zaidi ya kituo kimoja.

Hitimisho
Ushauri wangu kwa vijana wasaka tonge wahanga wa ajira na vijana woote watafutaji kwa ujumla napenda kutoa ushauri kama ufuatao:-

(i). Uvumilivu kwenye hizo fursa tunazoenda kuanzisha maana nako pia tutakutana na changamoto ila tusivunjike moyo na tusikate tamaa mapambano yaendelee.

(ii). Tuzijue hizo fursa na kutambua majira ya hizo fursa itasaidia kutambua muda gani muafaka wa kuanza tusikurupuke kuna kuanguka pia.

(iii). Kama unamtaji usianze na pesa yote ya mtaji maana hauna uhakika 100% kuwa itaenda sawa hivyo kujipanga kwa hilo ni muhimu.

(iv). Kupata ushauri kwa waliofanikiwa ni muhimu itakuongezea maarifa kwa yale usiyo yajua.

(v). Usimwamini kila mtu katika kufanya utafutaji wako wengine watakukwamisha. Mfano wanao kopa hawa ni sumu kwako unaeanza utafutaji.

(vi). Tambua hitaji la jamii ikizungukayo. Kama jamii inataka mahindi wapelekee mahindi na sio mchele. (Hitaji la wateja).

(vii). Ishi vizuri na watu na waheshimu watu kwa imani zao makabila yao na rangi zao.

(viii). Kuwa msafi au zingatia usafi kwenye ofisi yako kuwa na mpangilio mzuri na boresha mazingira ya ofisi yako.

(ix). Muhimu na la kukumbukwa kila unapopata kidogo kitunze kadri kinavyo kua kiwekeze kitaleta zaidi.

Hapa nimefikia mwisho wa andiko langu. Natumaini kidogo kitaeleweka kwa wengi haijaelezea kila.kitu ila nimeelezea kwa uchache kwa yale niliyojionea na kujifunza mtaani.

MUHIMU:
Msisahau kupigia kura andiko hili [emoji1317].
 
Kutokana na andiko lako lina mlengo wa kuonyesha kuwa hakuna umuhimu wa kusoma. Mimi naona ajira zipo nyingi Sana sema tatizo ni sera mbovu za ajira ie kulazimisha uzoefu pia kukosekana msukumo wa ajira za mpito/internship kumjengea uwezo muhitimu,sera la mbovu za kustaafu ie Kuna sababu gani mtu kustaafu miaka 60 kwanini isipunguzwe ili kuongeza nafasi za ajira, sera ya kujengea uwezo mahitimu ie kutoa elimu mbadala na kutoa mikopo yeye riba nafuu.
 
No. Sina maana ya kusema elimu haina maana. Nadhani haija nielewa vzr katika uwasilishaji wangu wa makala hii nimeorothesha njia baadhi za kumsaidia mhitimu anaetafuta kazi au mtaji ndio maana ukisoma sehemu niliyoielezea serikali kuhusu hii changamoto nimetoa maoni na kusema ikiwezekana kuwe na mgawanyo wa kazi, uwazi uwepo katika kupeana kazi/ajira, udini, ukabila, rushwa nk nimevikataa katika kuwapatia vijana wa kitanzania kazi/ajira. Nadhani labda kuna sehemu hujaisoma. Elimu ina umuhimu mkubwa katika maendeleo ya taifa lolote na pia nikasema mfumo wa elimu ufanyiwe maboresho ili uweze kuwaandaa vijana katika kile tunasema kujiajiri na kujitegemea.

Rudia kulisoma tena andiko utaona nilipoelezea mpaka hayo ya kustaafu nimeyaelezea. Yote kwa yote nashukuru kwa mchango wako mkuu [emoji1317][emoji1317]
 
Kutokana na andiko lako lina mlengo wa kuonyesha kuwa hakuna umuhimu wa kusoma. Mimi naona ajira zipo nyingi Sana sema tatizo ni sera mbovu za ajira ie kulazimisha uzoefu pia kukosekana msukumo wa ajira za mpito/internship kumjengea uwezo muhitimu,sera la mbovu za kustaafu ie Kuna sababu gani mtu kustaafu miaka 60 kwanini isipunguzwe ili kuongeza nafasi za ajira, sera ya kujengea uwezo mahitimu ie kutoa elimu mbadala na kutoa mikopo yeye riba nafuu.
Nimeona nikuletee hii niliyoelezea kidogo inayokuja kukujibu mawazo yako mkuu nimeyandika haya sehemu ya mambo serikali inaweza kuyafanya na yameongozana [emoji1313][emoji1313]

"7. Mfumo wa elimu uboreshwe hususani mitaala iwe rahisi kuwa andaa vijana kujitegemea kulingana na elimu waipatayo.

8.Kuwe na uwazi katika masuala ya ajira. Iwe za serikali mpaka mashirika binafsi uwazi uwepo.

9. Ukabila, rushwa, umaeneo na udini viepukwe katika kuwapatia vijana ajira.

10. Waliofikia umri wa kustaafu wasiruhusiwe kuendelea kufanya kazi.

11. Uwepo mgawanyo wa kazi.

Ili mtu mmoja asifanye kazi zaidi ya kituo kimoja."
[emoji1312] nadhani hapo kidogo umeona nilichokisema[emoji1317][emoji1317]
 
Jambo zuri kuonesha changamoto waliyonayo wahitimu kwaza shukrani mkuu[emoji1317]

Katika ushauri juu kwenye andiko nadhani niliandika vijana wakubaki kupewa ushauri na kwenye utatuzi wa changamoto nakumbuka hili nako nimelipa maelezo kiasi. Ila acha niliweke tena sawa hapa.

Kwa vijana wahitimu mnaoanza utafutaji msijikweze maana hata vitabu vya dini vimesema ajikwezae atashushwa. Na pia kukishusha kutakufaidisha katika kuyajua mengi zaidi kwenye utafutaji. Tena ikiwezekana km ni.ugenini kijana muhitimu wasijue kuwa wewe ni mhitimu mwenye degree hii itakusaidia kuwa sawa nao bila wao kuwa na reaction yoyote hasi kwako.
Vijana wetu nawaonea huruma maana wamepoteza muda mwingi kwenye madaftari na mavuno hakuna ni machache ningependekeza serikali kama ilivyowapatia wengi wao mikopo pia iwakopeshe na kuwapa elimu ya ujasiriamali.
 
Back
Top Bottom