SoC01 Wahitimu wa Vyuo na Maisha ya utafutaji Mtaani

SoC01 Wahitimu wa Vyuo na Maisha ya utafutaji Mtaani

Stories of Change - 2021 Competition

Theb

JF-Expert Member
Joined
Jan 25, 2019
Posts
3,927
Reaction score
7,276
Habari zenu wana Jamii Forums, hususani jukwaa hili la "Stories of Change". Ni tumaini langu wote ni wazima.

Andiko hili litaangazia maisha ya vijana wahitimu wa vyuo waliotegemea kuajiriwa na hali imekua tofauti na matarajio yao. Mwanzo, nitaelezea maisha ya mtaani, changamoto zinazo wakabili na vipi watatue hizo changamoto, Pili, nitaelezea fursa zisizohitaji mitaji na zenye kuhitaji mitaji. Tatu, nitaelezea mchango wa serikali na sekta binafsi katika kuwasaidia vijana kupata ajira na kujiajiri. Mwisho, nitamalizia kwa kutoa ushauri wangu katika kuwawezesha vijana wahitimu kujikwamua.

Maisha ya mtaani katika jamii zetu karibia kote yana mfanano kwa asilimia kubwa. Kuanzia ngazi ya familia za wahitimu walio wengi zinafanana kiuchumi, kitamaduni na hata kimalengo. Familia nyingi katika jamii zetu Tanzania tunasoma ili tuajiriwe na sio kujiajiri kwa waliowengi, hali iliyopo kwa sasa imeenda kinyume na malengo na matarijio ya vijana waliokuwa wanasoma na wanaoendelea kusoma mashuleni mpaka vyuoni.

CHANGAMOTO ZINAZO WAKABILI VIJANA WAHITIMU KATIKA UTAFUTAJI.

1. Kushindwa kujiamini na kushindwa kuikubali hali halisi iliyopo. Wengi wameshindwa kujiamini na kufikiria nje ya kitu walichosomea na kuanza kitu kipya ina wawia ngumu.

2. Mazingira yanayo wazunguka wahitimu, jamii ina wapa wakati mgumu kwa kuwahukumu kuwa wamesoma bure, elimu yao haina faida. Hili sio sawa.

3. Ukosefu wa muunganiko baina ya wahitimu na waliotangulia kwenye utafutaji, hapa unakuta wahitimu hawana muunganiko na waliotangulia kwenye utafutaji mitaani.

4. Ukosefu wa mitaji, hususani kwenye biashara au fursa zinazohitaji mitaji.

5. Kukosa uelewa katika utafutaji wenyewe. Kutozijua fursa au kutozitambua biashara na majira yake. Maana kila biashara ina majira yake.

6. Kuchagua kazi. Baadhi ya wahitimu hii changamoto kubwa kwao. Hawako tayari kubeba hata mizigo wanaona aibu au wanaona haiba yao hawastahili kubeba mizigo.

7. Mfumo na mitaala ya elimu nchini haikidhi dhumuni la kujiajiri kwa sababu imejikita katika nadharia zaidi na sio hali halisi katika kujiajiri.

JINSI YA KUPAMBANA NA HIZO CHANGAMOTO:-

1. Wazazi wasaidie watoto wao kuchagua fani zitakazo wawezesha kujiajiri pindi watakapo hitimu vyuoni.

2. Kujikubali, kujitambua na kujichanganya na watafutaji wengine mitaani bila kuwaza au kujutia muda uliopoteza shuleni na vyuoni.

3. Kukubali hali halisi hususani kuwa tayari kwa kazi yoyote bila kuchagua kazi. Mfano baadhi ya wahitimu ni ngumu kufanya kazi kama kuuza mkaa au kununua chupa za plastiki zilizotumika kwa kuhofia taaluma yake au watu watamuonaje.

4. Kuzitambua fursa na kuwa tayari kupambana nazo maana utafutaji mtaani ni ushindani.

5. Kufanya uchunguzi wa biashara unayotaka kwenda kuanzisha, hapa itahitaji kutafiti kwa kile unachotaka kufanya mtaani.

6. Kupunguza matumizi yale yasiyo muhimu. Kuwa na matumizi sahihi ya fedha. Mfano waache unywaji wa pombe, kubet, uvutaji wa sigara au ulevi wowote na anasa zingine zinazo hitaji pesa.

7. Kufanya uchaguzi sahihi wa kile unachoweza kukifanya mtaani na sio kufuata mkumbo. Fanya unachokipenda na unachokiweza

8. Usisahau kutunza kile unachokipata hata kama kidogo. (Bandu bandu humaliza gogo)

FURSA ZINAZOWEZA KUSAIDIA WAHITIMU KATIKA UTAFUTAJI MTAANI

1. Fursa zisizo hitaji mitaji na zisizo hitaji mitaji mikubwa sana. (Hizi kwa ajili ya kuanza kujipatia mitaji kidogo kidogo)

(i) Vibarua viwandani
Kwa wale wahitimu waliopo mijini kuna viwanda, vipo vibarua vya kutwa na wale wanaolipwa kwa wiki viwandani. Kuna kubeba mizigo viwandani kupakia na kupakua mizigo inayoingia na inayotoka na kazi zingine kulingana na kiwanda husika.

(ii) Fursa kwenye standi za mabasi ya abiria
Pia kwenye standi za mabasi kuna baadhi ya fursa zisizohitaji mitaji au zinazohitaji mitaji midogo. Mfano kubeba mizigo ya abiria kuwa wakala wa kukata tiketi na kuunza bidhaa ndogo ndogo kama karanga maji, juisi na matunda.

(iii) Kununua plastiki na kwenda kuziuza
Hapa kuna hii fursa ya kununua plastiki na kwenda kuuza mfano kilo moja unanunua kuanzia 300 hadi 400 na kuuza iliyosagwa ni kuanzia 800 hadi 1200 isiyo sagwa ni 800 bei ya kuuza. Hii ni fursa japo inadharauliwa.

(iv) Kuwa dalali wa mazao shambani au magari ya kusafirisha mizigo au dalali wa nyumba na viwanja
Haihitaji mtaji kwenye kuanza uaminifu wako na kujua chimbo za unachofanya ndio mtaji wako.

(v) Kuanzisha twisheni (tuition) mtaani kwenu
Hii pia saa zingine haihitaji mtaji itahitaji tu utayari wako na uwepo wa wanafunzi wanaosoma na kuitangaza. Japo maeneo mengine hii haina nafasi maana muitiko unakua mdogo hasa vijijini.

(vi) Kubeba mizigo kwenye masoko kupakua na kupakia mazao na bidhaa mbalimbali
Tunaweza kuidharau lakini ni fursa ukibeba mizigo 25 yenye kulipwa 1000 kila mzigo kwa siku una shilingi 25000. Haitaki mtu mwenye aibu na usharobaro.

(v). Kipaji kiwe cha uandishi, uimbaji, ususi, uchoraji, na michezo
Kipaji pia ni fursa kubwa tena isiyo hitaji mtaji ila inahitaji utayari wako kujituma na ubunifu zaidi na uvumilivu uliomithilika.

(vi). Kuwa saidia fundi ujenzi, fundi wa kuchomelea dirisha na mageti, fundi randa nk,

Kusaidia fundi atakulipa kidogo itategemea na kazi iliyopo hapo unajifunza ufundi, kujiandaa kuwa fundi ili ujitegemee. Mfano saidia fundi ujenzi hulipwa sio chini ya 10,000/= kwa siku.

(vii). Kuuza mahindi ya kuchoma na ya kuchemsha.
Hii hususani sehemu zenye mikusanyiko, stand za mabasi, barabarani na kwenye vyombo vya usafiri hususani mabasi.


2. Fursa zinazohitaji mitaji mikubwa au ya kiasi. Nitataja baadhi na ambazo ni rahisi kuzitambua kama ifuatavyo:-

(i). Kununua mazao mashambani na kuleta mjini kwenye masoko
Hapa kuna mahindi, viazi aina zote, mchele mboga mboga kutoka mashambani kuleta mijini. Kikubwa kufanya tathmini vizuri.

(ii). Umachinga wa kuuza vitu mtaani kando ya barabara au kutembeza au kutengeneza banda lako sehemu inayoonekana kwa wateja

(iii). Kilimo, uvuvi na ufugaji

Kilimo kinahitaji uwe na shamba, mbegu, pembejeo za kilimo mbolea na dawa za kupulizia kuua vijidudu hatarishi kwa mazao nacho kilimo kitategemea na aina ya mazao unayolima.

Ufugaji
Mfano wa kuku lazima uwe na mtaji wa kununua kuku, pumba, uduvi na mifupa.

(iv). Udereva boda boda au bajaji
Huu nao utahitaji uwe na mtaji au upate ya mtu. Mfano bado boda hakosi kupata 25000 hadi 30000 kwa siku.

(v). Kuanzisha saloon zote za kunyoa nywele na kusuka nywele
Hapa kwa wanaume na kwa wanawake kuna kunyoa na kusuka hivyo sehemu uliyopo ikiwa na uhitaji hii ni fursa.

(vi). Huduma ya kutuma pesa kwa njia za simu.
Kuanzisha M pesa, airtel money, tigo pesa na halopesa.

(vii). Kuanzisha mgahawa, mama ntilie au ukaangaji wa chipsi na kuchoma mishkaki.

(viii). Kununua na kuuza vyuma chakavu. Hii pia ni fursa inayolipa vizuri ni jambo la kufanya uchunguzi na kuthubutu.


MCHANGO WA SERIKALI PAMOJA NA SEKTA BINAFSI KATIKA KUWASAIDIA WAHITIMU.

1. Kuwapa motisha, semina na muongozo wa namna ya kuanza ujasiriamali.

2. Kuwapatia mikopo yenye riba nafuu au isiyo na riba kabisa.(walemavu wapewe kipaumbele).
Serikali na sekta binafsi kupitia benki na taasisi zingine za kifedha watoe mikopo kwa wahitimu. Pia familia zenye uwezo ziwawezeshe vijana wao waliohitimu.

3. Mazingira wezeshi kwa watafutaji wanaoanza kutafuta mtaani. Hapa kuwaondolea kodi kandamizi. Kuboresha miundo mbinu zaidi mijini na vijijini itasaidia usafirishaji wa bidhaa.

4. Serikali itengeneze mahusiano mazuri na mataifa mengine. Itasaidi kutanua soko la nje kwenye ajira na bidhaa au mazao yatakayo zalishwa nchini.

5. Serikali na sekta binafsi zinapaswa kwa pamoja kuwaamini vijana na kuondoa kigezo cha uzoefu katika kuwapatia kazi/ajira.

6. Serikali na sekta binafsi ziwashirikishe vijana katika juhudi za kuwainua iwe mikopo au semina za kiujasiriamali.

7. Mfumo wa elimu uboreshwe hususani mitaala. Elimu itolewe kwa vitendo na ijikite katika kuwaandaa kujitegemea/kujiajiri.

8. Wazazi, jamii, serikali na mashirika binafsi kwa pamoja watambue na kudhamini karama au vipaji vya wanafunzi toka wakiwa wadogo na kuvisimamia kwa lengo la kujiajiri baadae.

9. Wahitimu wote wenye ulemavu wapatiwe kazi serikalini na mashirika binafsi moja kwa moja. Mfano ajira za mwaka 2021 ualimu na afya serikali haikuwaacha nyuma hili liendelee kila wakati.

10.Kuwe na uwazi katika masuala ya ajira. Iwe za serikali mpaka mashirika binafsi.

11. Ukabila, rushwa, umaeneo na udini viepukwe katika kuwapatia vijana ajira.

12. Waliofikia umri wa kustaafu wasiruhusiwe kuendelea kufanya kazi.

13. Uwepo mgawanyo wa kazi.
Ili mtu mmoja asifanye kazi zaidi ya kituo kimoja.

USHAURI WANGU KWA VIJANA WAHITIMU KATIKA UTAFUTAJI
Ushauri wangu kwa vijana wasaka tonge wahanga wa ajira na vijana woote watafutaji kwa ujumla napenda kutoa ushauri kama ifuatavyo:-

(i). Uvumilivu kwenye hizo fursa tunazoenda kuanzisha maana nako pia tutakutana na changamoto ila tusivunjike moyo na tusikate tamaa mapambano yaendelee.

(ii). Tuzijue hizo fursa na kutambua majira ya hizo fursa itasaidia kutambua muda gani muafaka wa kuanza tusikurupuke kuna kuanguka pia.

(iii). Kama unamtaji usianze na pesa yote ya mtaji maana hauna uhakika 100% kuwa itaenda sawa hivyo kujipanga kwa hilo ni muhimu.

(iv). Kupata ushauri kwa waliofanikiwa ni muhimu itakuongezea maarifa kwa yale usiyo yajua.

(v). Usimuamini kila mtu katika utafutaji wako wengine watakukwamisha. Mfano wanao kopa ni sumu kwako unaeanza utafutaji.

(vi). Tambua hitaji la jamii ikizungukayo. Kama jamii inataka mahindi wapelekee mahindi na sio mchele.

(vii). Ishi vizuri na watu na waheshimu watu kwa imani zao makabila yao na rangi zao. Kuwa na lugha nzuri.

(viii). Zingatia usafi kwenye ofisi yako kuwa na mpangilio mzuri pia toa huduma iliyo bora sio bora huduma.

(ix). Muhimu na la kukumbukwa kila unapopata kidogo kitunze kadri kinavyo kua kiwekeze kitaleta zaidi.

(X). Fanya shughuli halali, kuwa muaminifu, uadilifu ni muhimu na kufuata sheria za nchi yetu katika utafutaji.
 
Upvote 1.6K
Mkuu uliiona..?
Nop. Kila anayeomba kura yangu huwa nashindwa kumpa coz of that, wengine wanasema namba ziko chini mwisho wa makala but nikiangalia mwisho wa makala sioni namba zozote, hapa nadhani jf hawakujipanga vizuri kwenye hili la kupiga kura
 
Nop. Kila anayeomba kura yangu huwa nashindwa kumpa coz of that, wengine wanasema namba ziko chini mwisho wa makala but nikiangalia mwisho wa makala sioni namba zozote, hapa nadhani jf hawakujipanga vizuri kwenye hili la kupiga kura
Itakua unatumia app ya jf kutoka play store haina option hiyo
 
Unayo.yasema hayo.yote ya watu kurudishana wastaafu nimeyakemea kwenye andiko hilo, ukabila, rushwa, mtu mmoja kushika kazi zaidi ya.moja nimekemea, nimeelezea vitu vingi japo kwa uchache kutokana na idadi iliyowekwa maneno.yasizidi. ila kiujumla mimi nimeilaumu serikali kwa maana vipi vipindi.ajira haikuwa changamoto saana mfano kipindi cha Hayari Mwl Nyerere, Mzee Mwinyi, Hayati Benjamin Mkapa, na hata Mzee kikwete awamu zao zilitoa ajira kwa kada nyingi.hususani elimu, ulinzi na afya ajira zilikua lazima ziwepo tena kwa wahitimu wote bila makandokando yoyote.

Ila awamu ya 5 ya Hayati J P Magufuli ndipo suala la ajira kwa vijana lilipo anza kuwa kitendawili kutokana na sera zake kutoweka kipaumbele katika kuwajiri vijana wahitimu.

Ningeweka itikadi hapa wangekuja wajuzi wa mambo.na kuniashushua kuwa je ajira zimekua adimu toka awamu ipi..? Na hizo.awamu zilizotoa ajira kila mwaka tena kwa vijana karibia wengi ya wahitimu ilikua chama gani.


Mkuu nadhani hapo.itakua umenielewa[emoji1317]
Kweli ajira zimepotea awamu ya 5 awamu za nyumba kabla.ya awamu ya mwendazake huu uhaba wa ajira na hiki kilio hakikuwepo. Yote yametokana na mwendazake kutowapa vijana ajira kwa kila mwaka yy aliamini ktk kununua ndege na kujenga madaraja
 
Serikali haiwezi kukwepa jukumu la kuwezesha watu wake. Kinachotakiwa serikali iwe inovative enough inawawezesha kwa namna gani? Hii tabia ya kutoa tujisenti kama mitaji wezeshi ni ujinga na utapeli ulio kubuhu.

Serikali inatakiwa iwekeze mabilioni kwenye miradi ya uzalishaji mali kupitia kilimo, uvuvi mifugo, madini nk halafu iwaite vijana na wasio na ajira kama wabia wenza wa nguvukazi kwenye hiyo miradi.

Lakini hii ya kumpa mtu fukara mwenye njaa 30,000/= kwa mfano. Unafikiri atazipekeka wapi zaidi ya tumboni?

Wazo la kuwashauri kuwaiga wale ambao wamefanikiwa na hawajaenda shule nalo halina afya kihivyo. Wengi wa hawa shuleless waliofanikiwa sehemu kubwa ya mafanikio yao nyuma yake ni nguvu za giza kutoa makafara kwa kwenda mbele. Kafara hizo ni za damu za watoto wao, ndugu, marafiki wa karibu na wafanyakazi walio waajiri. Niishie hapo asante sana.
Tusenti tudogo. Hahahaha hivyo tusenti vinaishia kununua unga basi wa dona na maharage ila sio kujikomboa kwa vijana. Serikali hii ya mama samia nivema angeliona hili. Na bunge hili la ndio mzee sidhani kama linaona huu msoto wa vijana.
 
Kweli ajira zimepotea awamu ya 5 awamu za nyumba kabla.ya awamu ya mwendazake huu uhaba wa ajira na hiki kilio hakikuwepo. Yote yametokana na mwendazake kutowapa vijana ajira kwa kila mwaka yy aliamini ktk kununua ndege na kujenga madaraja
Kwa hela cash. Bila kujali huduma kama za elimu na afya pia ulinzi.zinahitaji watumishi wapya kila mara.

Cha ajabu shuleni waalimu wa kizazi hiki ambao angalau wanajua jua hata maswala.ya kiteknolojia ambao.ni.hawa vijana hawapewi nafasi hivi tutaweza ku shindana na mataifa mengine ikiwa wastaafu ndio tegemeeo.letu. mkuu pitia nina andiko lingine la uwekezaji kwa vijana nilitaka niliungamishe hapa hapa ila idadi ya maneno.imenikamata haiwezekani
 
Ok. Shukran.karibu kwa hoja maoni mkuu hilo la kura itakua ushapiga amini hivyo. Karibu hapa kwa hoja maoni, uzoefu, mapito yako katika utafutaji kwa ujumla tujifunze wote[emoji1317][emoji1317][emoji1303]
 
Ok. Shukran.karibu kwa hoja maoni mkuu hilo la kura itakua ushapiga amini hivyo. Karibu hapa kwa hoja maoni, uzoefu, mapito yako katika utafutaji kwa ujumla tujifunze wote[emoji1317][emoji1317][emoji1303]
nilishachangia sana majuzi kuna comment zangu zaidi ya 10 humu
 
Vzr hivyo bado kura yako.ndio unashindwa kupiga tu..? Unatumia browsers ipi..?
 
Tusenti tudogo. Hahahaha hivyo tusenti vinaishia kununua unga basi wa dona na maharage ila sio kujikomboa kwa vijana. Serikali hii ya mama samia nivema angeliona hili. Na bunge hili la ndio mzee sidhani kama linaona huu msoto wa vijana.

Ndio shida ya kuwa na viongozi wanao jiona ni masuper stars na celebrities flani hivi. Hawajui ni kazi za utumishi wa nchi walizo aminiwa tu kuzifanya na wenzao. Wakishapata fedha za uwizi na rushwa vichwa vikiwavimba basi wanageuka kuwa mabwana na si watumishi wa wenzao tena. Wengine wanafurahia kuitwa jina la hawa waswahili "bwana kuba kesha sema" upuuzi kabisa.
 
Kwa hela cash. Bila kujali huduma kama za elimu na afya pia ulinzi.zinahitaji watumishi wapya kila mara.

Cha ajabu shuleni waalimu wa kizazi hiki ambao angalau wanajua jua hata maswala.ya kiteknolojia ambao.ni.hawa vijana hawapewi nafasi hivi tutaweza ku shindana na mataifa mengine ikiwa wastaafu ndio tegemeeo.letu. mkuu pitia nina andiko lingine la uwekezaji kwa vijana nilitaka niliungamishe hapa hapa ila idadi ya maneno.imenikamata haiwezekani
Elimu ina mchango zaidi katika kuliendeleza taifa lolotelolotewizara zote zinaitegemea wizara ya elimu katika kuandaa wataalamu wote nchini lakini serikali haioni
Ndio shida ya kuwa na viongozi wanao jiona ni masuper stars na celebrities flani hivi. Hawajui ni kazi za utumishi wa nchi walizo aminiwa tu kuzifanya na wenzao. Wakishapata fedha za uwizi na rushwa vichwa vikiwavimba basi wanageuka kuwa mabwana na si watumishi wa wenzao tena. Wengine wanafurahia kuitwa jina la hawa waswahili "bwana kuba kesha sema" upuuzi kabisa.
Siku hizi ukiwa celebrities ongezea na kashahada kokote ni rahisi kuwa na cheo serikalini
 
Ndio shida ya kuwa na viongozi wanao jiona ni masuper stars na celebrities flani hivi. Hawajui ni kazi za utumishi wa nchi walizo aminiwa tu kuzifanya na wenzao. Wakishapata fedha za uwizi na rushwa vichwa vikiwavimba basi wanageuka kuwa mabwana na si watumishi wa wenzao tena. Wengine wanafurahia kuitwa jina la hawa waswahili "bwana kuba kesha sema" upuuzi kabisa.
Tatizo.wanajua hakuna wakuwatoa washajua watz bado hawajaamka na wanatudanganya saana ila kubwa na la.muhimu nadhani hizi awamu za mwanzo.zilijitahidi kuendana na hitaji la.jamii hususani.masuala ya ajira ziliajiri wahitimu haswa kutoka 1 hadi ya 4 hivi vilio havikuepo aisee. Ila ya 5 kuja ya leo ajira hazipewi kipaombele. Wanashindwa kutambua kuwa katika taifa lolote lile vijana ndio uti wa mgongo wa mipango ya kesho. Mkuu nina uzi.mwingine wa kuitwa vijana ndio.uti wa mgongo.taifa liwekeze kwao nalo nimeelezea vema nilitaka niungamishe humu.sema limitation ya maneno.yasiyozid 1500 ikanikamata
 
Elimu ina mchango zaidi katika kuliendeleza taifa lolotelolotewizara zote zinaitegemea wizara ya elimu katika kuandaa wataalamu wote nchini lakini serikali haioni

Siku hizi ukiwa celebrities ongezea na kashahada kokote ni rahisi kuwa na cheo serikalini
Elimu.inahusika katika kutengeneza wizara zote nakubaliana na wewe kwa 100% . Elimu inahusika kuwaandaa viongozi, waalimu, madaktari, wauguzi, wajenzi, wanasheria, maafisa wa jeshi la polisi na wananchi, wahasibu nk lakini tutegemee nini ikiwa mbunge anaingia bungeni kwa kigezo cha kusoma na kuandoka ila mwalimu wa chekechea inabidi awe na ufaulu. Lazima sheria zianze kuithamini kwanza elimu mfano wa bunge hivyo.iwe km hawana level fulan ya elimu wasiruhusiwe kugombea
 
Ndio shida ya kuwa na viongozi wanao jiona ni masuper stars na celebrities flani hivi. Hawajui ni kazi za utumishi wa nchi walizo aminiwa tu kuzifanya na wenzao. Wakishapata fedha za uwizi na rushwa vichwa vikiwavimba basi wanageuka kuwa mabwana na si watumishi wa wenzao tena. Wengine wanafurahia kuitwa jina la hawa waswahili "bwana kuba kesha sema" upuuzi kabisa.
Angalia watoto wao sasa wanalia kama hawa wa wanyonge..?
 
Katika changamoto zinazowakabili hiyo number 6 ndio inasumbua wengi sana, hizi McDonalds tunazoona zilianzishwa na jamaa wa chips mayai wa mtaani kama wa kwetu tuu kwa hiyo tusione aibu na mambo mengi hayahitaji mitaji mikubwa kama wengi tunavyofikiria, issue ni kutafuta tatizo na kulitafutia solution na matatizo yapo mengi sana
 
Back
Top Bottom