SoC01 Wahitimu wa Vyuo na Maisha ya utafutaji Mtaani

SoC01 Wahitimu wa Vyuo na Maisha ya utafutaji Mtaani

Stories of Change - 2021 Competition

Theb

JF-Expert Member
Joined
Jan 25, 2019
Posts
3,927
Reaction score
7,276
Habari zenu wana Jamii Forums, hususani jukwaa hili la "Stories of Change". Ni tumaini langu wote ni wazima.

Andiko hili litaangazia maisha ya vijana wahitimu wa vyuo waliotegemea kuajiriwa na hali imekua tofauti na matarajio yao. Mwanzo, nitaelezea maisha ya mtaani, changamoto zinazo wakabili na vipi watatue hizo changamoto, Pili, nitaelezea fursa zisizohitaji mitaji na zenye kuhitaji mitaji. Tatu, nitaelezea mchango wa serikali na sekta binafsi katika kuwasaidia vijana kupata ajira na kujiajiri. Mwisho, nitamalizia kwa kutoa ushauri wangu katika kuwawezesha vijana wahitimu kujikwamua.

Maisha ya mtaani katika jamii zetu karibia kote yana mfanano kwa asilimia kubwa. Kuanzia ngazi ya familia za wahitimu walio wengi zinafanana kiuchumi, kitamaduni na hata kimalengo. Familia nyingi katika jamii zetu Tanzania tunasoma ili tuajiriwe na sio kujiajiri kwa waliowengi, hali iliyopo kwa sasa imeenda kinyume na malengo na matarijio ya vijana waliokuwa wanasoma na wanaoendelea kusoma mashuleni mpaka vyuoni.

CHANGAMOTO ZINAZO WAKABILI VIJANA WAHITIMU KATIKA UTAFUTAJI.

1. Kushindwa kujiamini na kushindwa kuikubali hali halisi iliyopo. Wengi wameshindwa kujiamini na kufikiria nje ya kitu walichosomea na kuanza kitu kipya ina wawia ngumu.

2. Mazingira yanayo wazunguka wahitimu, jamii ina wapa wakati mgumu kwa kuwahukumu kuwa wamesoma bure, elimu yao haina faida. Hili sio sawa.

3. Ukosefu wa muunganiko baina ya wahitimu na waliotangulia kwenye utafutaji, hapa unakuta wahitimu hawana muunganiko na waliotangulia kwenye utafutaji mitaani.

4. Ukosefu wa mitaji, hususani kwenye biashara au fursa zinazohitaji mitaji.

5. Kukosa uelewa katika utafutaji wenyewe. Kutozijua fursa au kutozitambua biashara na majira yake. Maana kila biashara ina majira yake.

6. Kuchagua kazi. Baadhi ya wahitimu hii changamoto kubwa kwao. Hawako tayari kubeba hata mizigo wanaona aibu au wanaona haiba yao hawastahili kubeba mizigo.

7. Mfumo na mitaala ya elimu nchini haikidhi dhumuni la kujiajiri kwa sababu imejikita katika nadharia zaidi na sio hali halisi katika kujiajiri.

JINSI YA KUPAMBANA NA HIZO CHANGAMOTO:-

1. Wazazi wasaidie watoto wao kuchagua fani zitakazo wawezesha kujiajiri pindi watakapo hitimu vyuoni.

2. Kujikubali, kujitambua na kujichanganya na watafutaji wengine mitaani bila kuwaza au kujutia muda uliopoteza shuleni na vyuoni.

3. Kukubali hali halisi hususani kuwa tayari kwa kazi yoyote bila kuchagua kazi. Mfano baadhi ya wahitimu ni ngumu kufanya kazi kama kuuza mkaa au kununua chupa za plastiki zilizotumika kwa kuhofia taaluma yake au watu watamuonaje.

4. Kuzitambua fursa na kuwa tayari kupambana nazo maana utafutaji mtaani ni ushindani.

5. Kufanya uchunguzi wa biashara unayotaka kwenda kuanzisha, hapa itahitaji kutafiti kwa kile unachotaka kufanya mtaani.

6. Kupunguza matumizi yale yasiyo muhimu. Kuwa na matumizi sahihi ya fedha. Mfano waache unywaji wa pombe, kubet, uvutaji wa sigara au ulevi wowote na anasa zingine zinazo hitaji pesa.

7. Kufanya uchaguzi sahihi wa kile unachoweza kukifanya mtaani na sio kufuata mkumbo. Fanya unachokipenda na unachokiweza

8. Usisahau kutunza kile unachokipata hata kama kidogo. (Bandu bandu humaliza gogo)

FURSA ZINAZOWEZA KUSAIDIA WAHITIMU KATIKA UTAFUTAJI MTAANI

1. Fursa zisizo hitaji mitaji na zisizo hitaji mitaji mikubwa sana. (Hizi kwa ajili ya kuanza kujipatia mitaji kidogo kidogo)

(i) Vibarua viwandani
Kwa wale wahitimu waliopo mijini kuna viwanda, vipo vibarua vya kutwa na wale wanaolipwa kwa wiki viwandani. Kuna kubeba mizigo viwandani kupakia na kupakua mizigo inayoingia na inayotoka na kazi zingine kulingana na kiwanda husika.

(ii) Fursa kwenye standi za mabasi ya abiria
Pia kwenye standi za mabasi kuna baadhi ya fursa zisizohitaji mitaji au zinazohitaji mitaji midogo. Mfano kubeba mizigo ya abiria kuwa wakala wa kukata tiketi na kuunza bidhaa ndogo ndogo kama karanga maji, juisi na matunda.

(iii) Kununua plastiki na kwenda kuziuza
Hapa kuna hii fursa ya kununua plastiki na kwenda kuuza mfano kilo moja unanunua kuanzia 300 hadi 400 na kuuza iliyosagwa ni kuanzia 800 hadi 1200 isiyo sagwa ni 800 bei ya kuuza. Hii ni fursa japo inadharauliwa.

(iv) Kuwa dalali wa mazao shambani au magari ya kusafirisha mizigo au dalali wa nyumba na viwanja
Haihitaji mtaji kwenye kuanza uaminifu wako na kujua chimbo za unachofanya ndio mtaji wako.

(v) Kuanzisha twisheni (tuition) mtaani kwenu
Hii pia saa zingine haihitaji mtaji itahitaji tu utayari wako na uwepo wa wanafunzi wanaosoma na kuitangaza. Japo maeneo mengine hii haina nafasi maana muitiko unakua mdogo hasa vijijini.

(vi) Kubeba mizigo kwenye masoko kupakua na kupakia mazao na bidhaa mbalimbali
Tunaweza kuidharau lakini ni fursa ukibeba mizigo 25 yenye kulipwa 1000 kila mzigo kwa siku una shilingi 25000. Haitaki mtu mwenye aibu na usharobaro.

(v). Kipaji kiwe cha uandishi, uimbaji, ususi, uchoraji, na michezo
Kipaji pia ni fursa kubwa tena isiyo hitaji mtaji ila inahitaji utayari wako kujituma na ubunifu zaidi na uvumilivu uliomithilika.

(vi). Kuwa saidia fundi ujenzi, fundi wa kuchomelea dirisha na mageti, fundi randa nk,

Kusaidia fundi atakulipa kidogo itategemea na kazi iliyopo hapo unajifunza ufundi, kujiandaa kuwa fundi ili ujitegemee. Mfano saidia fundi ujenzi hulipwa sio chini ya 10,000/= kwa siku.

(vii). Kuuza mahindi ya kuchoma na ya kuchemsha.
Hii hususani sehemu zenye mikusanyiko, stand za mabasi, barabarani na kwenye vyombo vya usafiri hususani mabasi.

2. Fursa zinazohitaji mitaji mikubwa au ya kiasi. Nitataja baadhi na ambazo ni rahisi kuzitambua kama ifuatavyo:-

(i). Kununua mazao mashambani na kuleta mjini kwenye masoko
Hapa kuna mahindi, viazi aina zote, mchele mboga mboga kutoka mashambani kuleta mijini. Kikubwa kufanya tathmini vizuri.

(ii). Umachinga wa kuuza vitu mtaani kando ya barabara au kutembeza au kutengeneza banda lako sehemu inayoonekana kwa wateja

(iii). Kilimo, uvuvi na ufugaji

Kilimo kinahitaji uwe na shamba, mbegu, pembejeo za kilimo mbolea na dawa za kupulizia kuua vijidudu hatarishi kwa mazao nacho kilimo kitategemea na aina ya mazao unayolima.

Ufugaji
Mfano wa kuku lazima uwe na mtaji wa kununua kuku, pumba, uduvi na mifupa.

(iv). Udereva boda boda au bajaji
Huu nao utahitaji uwe na mtaji au upate ya mtu. Mfano bado boda hakosi kupata 25000 hadi 30000 kwa siku.

(v). Kuanzisha saloon zote za kunyoa nywele na kusuka nywele
Hapa kwa wanaume na kwa wanawake kuna kunyoa na kusuka hivyo sehemu uliyopo ikiwa na uhitaji hii ni fursa.

(vi). Huduma ya kutuma pesa kwa njia za simu.
Kuanzisha M pesa, airtel money, tigo pesa na halopesa.

(vii). Kuanzisha mgahawa, mama ntilie au ukaangaji wa chipsi na kuchoma mishkaki.

(viii). Kununua na kuuza vyuma chakavu. Hii pia ni fursa inayolipa vizuri ni jambo la kufanya uchunguzi na kuthubutu.

MCHANGO WA SERIKALI PAMOJA NA SEKTA BINAFSI KATIKA KUWASAIDIA WAHITIMU.

1. Kuwapa motisha, semina na muongozo wa namna ya kuanza ujasiriamali.

2. Kuwapatia mikopo yenye riba nafuu au isiyo na riba kabisa.(walemavu wapewe kipaumbele).
Serikali na sekta binafsi kupitia benki na taasisi zingine za kifedha watoe mikopo kwa wahitimu. Pia familia zenye uwezo ziwawezeshe vijana wao waliohitimu.

3. Mazingira wezeshi kwa watafutaji wanaoanza kutafuta mtaani. Hapa kuwaondolea kodi kandamizi. Kuboresha miundo mbinu zaidi mijini na vijijini itasaidia usafirishaji wa bidhaa.

4. Serikali itengeneze mahusiano mazuri na mataifa mengine. Itasaidi kutanua soko la nje kwenye ajira na bidhaa au mazao yatakayo zalishwa nchini.

5. Serikali na sekta binafsi zinapaswa kwa pamoja kuwaamini vijana na kuondoa kigezo cha uzoefu katika kuwapatia kazi/ajira.

6. Serikali na sekta binafsi ziwashirikishe vijana katika juhudi za kuwainua iwe mikopo au semina za kiujasiriamali.

7. Mfumo wa elimu uboreshwe hususani mitaala. Elimu itolewe kwa vitendo na ijikite katika kuwaandaa kujitegemea/kujiajiri.

8. Wazazi, jamii, serikali na mashirika binafsi kwa pamoja watambue na kudhamini karama au vipaji vya wanafunzi toka wakiwa wadogo na kuvisimamia kwa lengo la kujiajiri baadae.

9. Wahitimu wote wenye ulemavu wapatiwe kazi serikalini na mashirika binafsi moja kwa moja. Mfano ajira za mwaka 2021 ualimu na afya serikali haikuwaacha nyuma hili liendelee kila wakati.

10.Kuwe na uwazi katika masuala ya ajira. Iwe za serikali mpaka mashirika binafsi.

11. Ukabila, rushwa, umaeneo na udini viepukwe katika kuwapatia vijana ajira.

12. Waliofikia umri wa kustaafu wasiruhusiwe kuendelea kufanya kazi.

13. Uwepo mgawanyo wa kazi.
Ili mtu mmoja asifanye kazi zaidi ya kituo kimoja.

USHAURI WANGU KWA VIJANA WAHITIMU KATIKA UTAFUTAJI
Ushauri wangu kwa vijana wasaka tonge wahanga wa ajira na vijana woote watafutaji kwa ujumla napenda kutoa ushauri kama ifuatavyo:-

(i). Uvumilivu kwenye hizo fursa tunazoenda kuanzisha maana nako pia tutakutana na changamoto ila tusivunjike moyo na tusikate tamaa mapambano yaendelee.

(ii). Tuzijue hizo fursa na kutambua majira ya hizo fursa itasaidia kutambua muda gani muafaka wa kuanza tusikurupuke kuna kuanguka pia.

(iii). Kama unamtaji usianze na pesa yote ya mtaji maana hauna uhakika 100% kuwa itaenda sawa hivyo kujipanga kwa hilo ni muhimu.

(iv). Kupata ushauri kwa waliofanikiwa ni muhimu itakuongezea maarifa kwa yale usiyo yajua.

(v). Usimuamini kila mtu katika utafutaji wako wengine watakukwamisha. Mfano wanao kopa ni sumu kwako unaeanza utafutaji.

(vi). Tambua hitaji la jamii ikizungukayo. Kama jamii inataka mahindi wapelekee mahindi na sio mchele.

(vii). Ishi vizuri na watu na waheshimu watu kwa imani zao makabila yao na rangi zao. Kuwa na lugha nzuri.

(viii). Zingatia usafi kwenye ofisi yako kuwa na mpangilio mzuri pia toa huduma iliyo bora sio bora huduma.

(ix). Muhimu na la kukumbukwa kila unapopata kidogo kitunze kadri kinavyo kua kiwekeze kitaleta zaidi.

(X). Fanya shughuli halali, kuwa muaminifu, uadilifu ni muhimu na kufuata sheria za nchi yetu katika utafutaji.
 
Upvote 1.6K
Mr. Mbagga 333:

Uthubutu na kudiriki ingawa matatizo ya vijana wa Tanzania yanatofautiana kutoka sehemu moja kwenda sehemu nyingine.

Matatizo yanaanza kuanzia ngazi ya familia,jamii mpaka kitaifa. Kwamba soma uelimike.

Watu wengi wanafanya vitu kwa mkumbo saaana. Kitu kilichofanikiwa kwako kwa mwingine hakiwezi kufanikiwa.

Hili kwako unalionaje, kama muandishi wa hili andiko upo kwenye kujiajiri au ni mawazo tu ?
 
Mimi ni.muhitimu yaani mhanga wa nilichokiandika na nimeandika mengi nimejionea ndio maana na hapo nimefupisha saana maelezo kutokana na sheria ilivyo sema kuwa ya sizidi 1500.

Nipo napambana na mtaa kama umepitia juu huko utaona kuna sehemu nimeeleza kwamba shughuli moja wapo.ambayo nishawahi kufanya. Ambayo ilikua ni biashara ya mkaa pia na biashara ya viazi nilijihusisha kidogo na ndio naifikiria tena kuirudia. Sina ajira japo nina degree. Hivyo nimeandika kitu halisi ambacho kipo na hata wewe ukiuliza au ukifuatilia una labda wadogo zako, ndugu zako na jamaa ambao ni wahanga.

Umesema sio kila kilichomfanikisha mwingine na wewe kitakufanikisha ni.kweli sikatai ila itategemea mazingira, umejipangaje(mtaji, kulijua soko, na kila hitaji la ujasiriamali unaouwaza), pia fursa zipo nyingi na sio kila fursa inapatikana kila eneo.

Mfano.

1. Fursa ya kununua plastic na kuzipeleka kwa wanunuaji.wakubwa huwezi kuianzisha vijijini ni dhahiri hutapata mzgo wa kutosha kwa wakati katika biashara yako hiyo.

2. Kilimo, kwenye kilimo kila kanda ina hali ya hewa tofauti na sehemu nyingine nidhahiri mazao hayawezi ya kafanana kila kanda au kila mkoa. Hapa namaanisha mazao yanayolimwa mfano Kilimanjaro hayawezi kulimwa yoote mikoa ya pwani. Chukulia zao la viazi mviringo linakulia ukanda wenye baridi na mvua ya kutosha haliwezi kukulia mikoa yenye joto kama pwani, mtwara na dar es salaam pia Tanga kuacha wilaya ya lushoto. Yapo mazao yanaweza kuzalishwa ukanda wenye baridi na wenye joto mfano mahindi na Nyanya. Ila huwezi kupanda mpunga sehemu yenye baridi kama njombe.

Mkuu nimachache nimejaribu kukupa ka mwelekeo juu ya ulichokisema kuwa sio kila kilichomfanikisha mwingine na wewe kitakufanikisha. Hilo kweli ila zipo sababu za kuzingatiwa ili.mtu hata kama unaiga lazima uzifuate na ukubali kujifunza na kupambana na changamoto.
 
Mr. Mbagga 333:

Uthubutu na kudiriki ingawa matatizo ya vijana wa Tanzania yanatofautiana kutoka sehemu moja kwenda sehemu nyingine.

Matatizo yanaanza kuanzia ngazi ya familia,jamii mpaka kitaifa. Kwamba soma uelimike.

Watu wengi wanafanya vitu kwa mkumbo saaana. Kitu kilichofanikiwa kwako kwa mwingine hakiwezi kufanikiwa.

Hili kwako unalionaje, kama muandishi wa hili andiko upo kwenye kujiajiri au ni mawazo tu ?
Niongezee tu kusema kila fursa kabla ya kuikabili lazima kufanya uchuguzi na kuitambua vzr. Km nilivyosema juu kwenye ushauri kule kwenye andiko ya kuwa lazima uijue hiyo fursa kwa maana ujue mtaji unaoweza kutosha, mazingira(soko kununua na kuuza), majira ya hiyo fursa, lazima ujifunze na kuuliza waliokutangulia, lazima ukubali na uwe tayari kuzikali changamoto kwa maana hakuna kitu chepesi hata siku moja.

Kitu chepesi itakua ni kuelezea ya wenzako tu na kuyakosoa au kusifia tu.

Vijana tuthubutu tunaweza
 
Mimi ni.muhitimu yaani mhanga wa nilichokiandika na nimeandika mengi nimejionea ndio maana na hapo nimefupisha saana maelezo kutokana na sheria ilivyo sema kuwa ya sizidi 1500.

Nipo napambana na mtaa kama umepitia juu huko utaona kuna sehemu nimeeleza kwamba shughuli moja wapo.ambayo nishawahi kufanya. Ambayo ilikua ni biashara ya mkaa pia na biashara ya viazi nilijihusisha kidogo na ndio naifikiria tena kuirudia. Sina ajira japo nina degree. Hivyo nimeandika kitu halisi ambacho kipo na hata wewe ukiuliza au ukifuatilia una labda wadogo zako, ndugu zako na jamaa ambao ni wahanga.

Umesema sio kila kilichomfanikisha mwingine na wewe kitakufanikisha ni.kweli sikatai ila itategemea mazingira, umejipangaje(mtaji, kulijua soko, na kila hitaji la ujasiriamali unaouwaza), pia fursa zipo nyingi na sio kila fursa inapatikana kila eneo.

Mfano.

1. Fursa ya kununua plastic na kuzipeleka kwa wanunuaji.wakubwa huwezi kuianzisha vijijini ni dhahiri hutapata mzgo wa kutosha kwa wakati katika biashara yako hiyo.

2. Kilimo, kwenye kilimo kila kanda ina hali ya hewa tofauti na sehemu nyingine nidhahiri mazao hayawezi ya kafanana kila kanda au kila mkoa. Hapa namaanisha mazao yanayolimwa mfano Kilimanjaro hayawezi kulimwa yoote mikoa ya pwani. Chukulia zao la viazi linakulia ukanda wenye baridi na mvua ya kutosha haliwezi kukulia mikoa yenye joto kama pwani, mtwara na dar es salaam pia Tanga kuacha wilaya ya lushoto. Yapo mazao yanaweza kuzalishwa ukanda wenye baridi na wenye joto mfano mahindi na Nyanya. Ila huwezi kupanda mpunga sehemu yenye baridi kama njombe.

Mkuu nimachache nimejaribu kukupa ka mwelekeo juu ya ulichokisema kuwa sio kila kilichomfanikisha mwingine na wewe kitakufanikisha. Hilo kweli ila zipo sababu za kuzingatiwa ili.mtu hata kama unaiga lazima uzifuate na ukubali kujifunza na kupambana na changamoto.
Umethubutu mkuu 🤝
 
Umethubutu mkuu [emoji1666]
Ndio mkuu japo changamoto ni nyingi sio kidogo. Kuanguka na kuanza kawaida ila ndio kujifunza huko. Maana tusipo thubutu hatuwezi kujifunza lolote.
 
Mim Ni mzawa wa njombe na nimekulia huko nikwel fursa zipo Tena nyingi haswa za mazao na misutu Koo na maeneo kwa wale wanaopend kuwekeza kwenye ardhi
Vizuri. Nimechelewa kuiona hii reply yako karibu kwanza. Ndio mbao za huko ni hizo za paini tu au hata za asili
 
Naunga mkono hoja.
Shukran karibu mkuu hapa utupe na wewe nondo za kitaa kama.zipo au km zipo hoja zilete wadau wapo wakipita watasawazisha kila.lenye kuuliza.[emoji1317][emoji1317][emoji1303]
 
Shukran karibu mkuu hapa utupe na wewe nondo za kitaa kama.zipo au km zipo hoja zilete wadau wapo wakipita watasawazisha kila.lenye kuuliza.[emoji1317][emoji1317][emoji1303]
Sawa, ngoja nipige kwanza research ya kutosha kitaa then nilete nondo na mimi kuongezea.
 
Sawa, ngoja nipige kwanza research ya kutosha kitaa then nilete nondo na mimi kuongezea.
Pamoja sana mkuu. Ulipo naimani fursa zipo lete wazo tulichambue moja jumlisha moja zitakua mbili mara mbili zingine zitakua 4. Mawazo.ya wengi ni njia inayoweza kueleweka kwa haraka
 
Kwa watoto wa masikini waliosomeshwa kwa wazazi wao kujinyima ndio wanaoambiwaga wakajiajiri na wakifika mitaani walikoambiwa wakajiajiri wanakuta nafasi zote za kujiajiri zimebanwa na wale wenye vipaji vya kujiajiri,kwani kujiajiri nako ni kipaji,unaweza ukatoka huko na degrees zako ukasema kuwa unakwenda kujiajiri ukajikuta unaambulia patupu pamoja na degrees zako zote kwa kuwa kujiajiri siyo kipaji chako.

Kujiajiri kunakuja pale ambapo serekali ambayo ndiyo yenye wajibu wakuwaajiri vijana inaposhindwa kutimiza wajibu wake wa kutoa ajira kwa vijana iliowasomesha yenyewe,wakati huo haijawaandaa kujiajiri kwa kuwa mafunzo yanayotolewa kwa wakati huwa yanalenga kuajiriwa na siyo kujiajiri.

Kwa upande wa vigogo mbali na watoto wao kuwa wamesoma ki ulayaulaya ki mayaimayai hali ni tofauti kabisa,neno kajiajiri kwao ni msamiati mgumu kwa kuwa wao wanakuwa na uhakika na ajira kwa vile wao wanaandaliwa kuwa watawala wakuwatawala hawa wanaoambiwa wakajiajiri pamoja na kusimamia miradi ya baba zao.
 
Hakika umenena vyema. Wanaoteseka ni hawa hawa wa maisha duni wale wale wakuitwa wanyonge. Ajabu saana viongozi wetu wanawaingiza watoto wao kwenye mfumo wa utawala ili hali wengine hawana hata maarifa na wenye maarifa au karama za uongozi unakuta hawapewi nafasi. Ni suala lisiloepukika la kuufanyia maboresho mfumo wetu wa elimu na mitaala kwa ujumla iweze kuendana na hali halisi ya ukosefu wa ajira na iweze kuwapatia wahitimu maarifa ya namna ya kujiajiri.

Ni ngumu kumkuta mtoto wa kiongozi akiwa anapanga foleni kwenye usaili wowote ule nchini. Wao wapo karibu na keki ya taifa. Yaani nchi moja lakn kuna waliopo mbele ya wenzao hata kama vigezo hawana ila wanabebwa ndio maana tunaona vituko kwenye hizi tawala zetu.

Kwa ujumla hapo juu kwenye uzi kuna sehemu nilisema uwazi uwepo katika masuala ya ajira, rushwa, kujuana, itikadi, ukabila, umaeneo, udini na ungudu viepukwe katika kuwa patia ajira vijana nchini.
 
Kwa watoto wa masikini waliosomeshwa kwa wazazi wao kujinyima ndio wanaoambiwaga wakajiajiri na wakifika mitaani walikoambiwa wakajiajiri wanakuta nafasi zote za kujiajiri zimebanwa na wale wenye vipaji vya kujiajiri,kwani kujiajiri nako ni kipaji,unaweza ukatoka huko na degrees zako ukasema kuwa unakwenda kujiajiri ukajikuta unaambulia patupu pamoja na degrees zako zote kwa kuwa kujiajiri siyo kipaji chako.

Kujiajiri kunakuja pale ambapo serekali ambayo ndiyo yenye wajibu wakuwaajiri vijana inaposhindwa kutimiza wajibu wake wa kutoa ajira kwa vijana iliowasomesha yenyewe,wakati huo haijawaandaa kujiajiri kwa kuwa mafunzo yanayotolewa kwa wakati huwa yanalenga kuajiriwa na siyo kujiajiri.

Kwa upande wa vigogo mbali na watoto wao kuwa wamesoma ki ulayaulaya ki mayaimayai hali ni tofauti kabisa,neno kajiajiri kwao ni msamiati mgumu kwa kuwa wao wanakuwa na uhakika na ajira kwa vile wao wanaandaliwa kuwa watawala wakuwatawala hawa wanaoambiwa wakajiajiri pamoja na kusimamia miradi ya baba zao.
Na pia mkuu watoto wa vigogo au viongozi kwa ujumla wazazi wao washachuma saana kupitia vyeo vyao hivyo kwao suala la mitaji au wapi pakujishikiza sio changamoto hata kidogo. Hili tumuangazie mtoto wa masikini ambaye kwao hazipo pesa na vyeo havipo hana amjuaye ndani ya mfumo hivyo anapitia hizi changamoto zote.
 
Ndio.nadhani nitaliongezea kwenye kilimo kwa maana ya kwamba hii miti inayokatwa na.kuchanwa hizo.mbao ni kilimo pia. Kuna miradi mingi ya hawa wakulima wa miti kwenye hiyo mikoa mimi nilishawahi kupika hiyo mikoa sijabahatika kuishi au hata kushinda siku moja lakini huko njombe, iringa, makambako na mufindi niliona kule miti ni kilimo pia kingine. Kwa kuona kwangu tu ndio nilijua kua ni kilimo.

Ndio.nadhani nitaliongezea kwenye kilimo kwa maana ya kwamba hii miti inayokatwa na.kuchanwa hizo.mbao ni kilimo pia. Kuna miradi mingi ya hawa wakulima wa miti kwenye hiyo mikoa mimi nilishawahi kupika hiyo mikoa sijabahatika kuishi au hata kushinda siku moja lakini huko njombe, iringa, makambako na mufindi niliona kule miti ni kilimo pia kingine. Kwa kuona kwangu tu ndio nilijua kua ni

Ndio.nadhani nitaliongezea kwenye kilimo kwa maana ya kwamba hii miti inayokatwa na.kuchanwa hizo.mbao ni kilimo pia. Kuna miradi mingi ya hawa wakulima wa miti kwenye hiyo mikoa mimi nilishawahi kupika hiyo mikoa sijabahatika kuishi au hata kushinda siku moja lakini huko njombe, iringa, makambako na mufindi niliona kule miti ni kilimo pia kingine. Kwa kuona kwangu tu ndio nilijua kua ni kilimo.

Mim Ni mzawa wa njombe na nimekulia huko nikwel fursa zipo Tena nyingi haswa za mazao na misutu Koo na maeneo kwa wale wanaopend kuwekeza kwenye ardhi
Gud. Mwenyeji vipi kilimo hicho cha miti kinakuaga miaka mingapi mpka mit ikomae iwe tayari kwa uvunwaji..??
 
Mr. Mbagga 333:

Uthubutu na kudiriki ingawa matatizo ya vijana wa Tanzania yanatofautiana kutoka sehemu moja kwenda sehemu nyingine.

Matatizo yanaanza kuanzia ngazi ya familia,jamii mpaka kitaifa. Kwamba soma uelimike.

Watu wengi wanafanya vitu kwa mkumbo saaana. Kitu kilichofanikiwa kwako kwa mwingine hakiwezi kufanikiwa.

Hili kwako unalionaje, kama muandishi wa hili andiko upo kwenye kujiajiri au ni mawazo tu ?
Upo sahihi kiongozi. Fursa hizo alitoorithesha mwenzetu zipo mitaani lakini sio kla fursa inapatikana hapo ulipo. Mahitaji ya sehemu hayafananiii kwa yote japo kwa mijini mahitaji yanaweza kufanana kwa asilimia kubwa. Naona fursa za kwenye miji mikubwa zinafanana na pia za vijijin zinafanana.
 
Ndio.nadhani nitaliongezea kwenye kilimo kwa maana ya kwamba hii miti inayokatwa na.kuchanwa hizo.mbao ni kilimo pia. Kuna miradi mingi ya hawa wakulima wa miti kwenye hiyo mikoa mimi nilishawahi kupika hiyo mikoa sijabahatika kuishi au hata kushinda siku moja lakini huko njombe, iringa, makambako na mufindi niliona kule miti ni kilimo pia kingine. Kwa kuona kwangu tu ndio nilijua kua ni kilimo.
Nimekuelewa kiongozi.
 
Back
Top Bottom