Tuko na safari ndefu sana kama taifa.
Ndiyo maana mataifa mengine yanafaidi sana kwa kuwatumia wahitimu wetu ambao miaka nenda rudi serikali imetumia gharama kubwa kuwasomesha.
Tunataka kila mtu apate elimu, lakini kama hakuna mazingira wezeshi na ya makusudi ili kuwafanya wanufaike na elimu waliyoipata, maarifa yale huleta tija kiduchu.
Kumbuka msomi huwa na matarajio makubwa sana anapokuwa masomoni - ametumia muda, nguvu, pesa na hata wakati mwingine kuhatarisha afya yake.
Hawa wasipopata walichosomea, hii hupelekea msongo mkubwa sana wa mawazo na matokeo yake huweza kuwa mabaya zaidi.