macho_mdiliko
Platinum Member
- Mar 10, 2008
- 25,191
- 48,765
Watanzania tunaishi dunia yetu. Nadhani elimu yetu duni hasa kutoweza kuelewa kiingereza na kukosa exposure ndiyo kinafanya watu wawe na akili kama zako. Nasema hivi kwa sababu nchi haiwezi kuwa na vijana ambao kila mmoja anafanya biashara. Jaribu kutembea nchi za Ulaya uone wanaomaliza vyuo vikuu ni wangapi wanafanya biashara na ni wangapi wanaajiriwa au kujiajiri wenyewe. Makosa ya CCM na viongozi wake kukosa plan na kutofanya kazi ya uongozi hakuwezi kumalizwa kwa vijana kuwa na ''mitaji ya biashara''. Hata kama ukiwapa wahitimu wote mitaji sasa hivi, bado hali itakuwa mbaya kwa sababu supply itakuwa kubwa kuliko demand. Matatizo ya CCM kufeli hayawezi kumalizwa kwa short-cut za kuwapa vijana mitaji ya kufanya biashara. Tuna tatizo kubwa linalohitaji urgent and aggressive solution, bila huu upumbavu wanaofanya Samia na wenzake. Tukubali kwanza tuna matatizo makubwa na tuungane wote kufumua mfumo wetu wa uongozi uliotufelisha na kuunda upya.Tazama mwenyewe huyu dada graduate anavyoteseka
View attachment 3238169
huu ni Ushuhuda: Tusirudie makosa ya wazazi wetu kukariri elimu ni ufunguo wa maisha
mtoto afundishwe biashara na kuzalisha pesa kwa kujiajiri mapema.
Watoto wa zama hizi wajifunze high income skills mapema, hii itawasaidia sana
No need kuweka pesa nyingi kwenye formal education.
Tatizo la Ajira linaletwa na Wazazi wahuni.
Hujamrithisha mtoto Mali , familia haina family business na wala mtoto hapewi mtaji, sasa ataachaje kukosa Ajira?