Kwani kwanini unasoma na kwa faida ya nani?
Unasoma kwa faida yako wewe na wala sio ya mtu yoyote au serikali na kama ulishindwa kujiajiri kwa mkopo wako ulipokuwa chuo unategemea ujiajiri mtaani tena kwa laki mbili?
Kwa akili za graduates wa Tanzania zilivyo (hata humu wapo lakini angalia uwezo wao hata wa kuandika tu).
Walichokuwa kuwa wanakifanya chuo kwa mkopo ndio hicho hicho watakifanya kwa hicho kilaki mbili, yaani kulewa na kufanya anasa (kula bata na maisha according to them).
Hawa graduates ni useless kwa taifa na kwao wenyewe pia, hawana na wala hawajaonyesha uwezo wowote extraordinary kama graduates wa nchi nyingine kwenye utatuzi wa changamoto za kijamii, kimazingira, kiintelligence, kitechnology, kimatibabu, kiinjinia na wala uvumbuzi na ugunduzi zaidi ya kufikiria ngono.
Uwezo extraordinary angalau kuleta hamasa kwa wananchi walipa kodi na serikali kutoa msaada.
Ndio wananchi sababu hizo pesa ni za wananchi walipa kodi na mimi siwezi kulipa kodi yangu alafu akapewe mlevi mmoja akalewe kwa jina la graduate.
Unasaidia mtu mwenye uwezo na anayeonyesha nia ya kujisaidia zaidi ya hapo achana nae utakuwa unamlazimisha na maumivu mtakula wote.
Wewe ni graduate nipinge hapa kwa hoja za kueleweka.