Wahitimu Wasiohudhuria Mahafali Wanatozwa hela ya joho mda wa kufuta cheti .je hii ni sawa

Wahitimu Wasiohudhuria Mahafali Wanatozwa hela ya joho mda wa kufuta cheti .je hii ni sawa

Dalton Elijah

JF-Expert Member
Joined
Jul 19, 2022
Posts
968
Reaction score
1,978
Sio jambo geni wala la kushangaza kwa baadhi ya wahitimu wa vyuo vikuu nchini Tanzania kukutana na changamoto mbalimbali baada ya kumaliza masomo yao. Kwa kawaida, kumaliza shahada au stashahada ni hatua ya furaha na fahari kwa mhitimu na familia yake. Hata hivyo, baadhi ya vyuo vikuu nchini vimeweka utaratibu wa kuwauzia wahitimu majoho kama sehemu ya kumbukumbu ya mahafali.

Kwa mfano, Moja ya chuo kikuu jijini mwanza , gharama ya joho ni takribani Tsh 52,000. Changamoto hujitokeza pale ambapo mwanafunzi anashindwa kushiriki mahafali kwa sababu mbalimbali.

Kando na taarifa hiyo Pindi anapokwenda kuchukua cheti chake, uongozi wa chuo humtaka alipe gharama ya joho Tsh 52,000—hata kama hakuhudhuria mahafali.

Hapa ndipo swali muhimu linapozuka: Hela ya joho inayolipwa na mhitimu ambaye hakuhudhuria mahafali inaenda wapi, ilhali mahafali yalishafanyika? Je, huu ni utaratibu wa baadhi ya vyuo kutengeneza fedha kwa kuwatoza wanafunzi ambao hawakushiriki mahafali? Zaidi ya hapo, kwa nini mhitimu anayelipa gharama ya joho wakati wa kuchukua cheti asipewe joho lake ili aweze kupiga picha au kufanya sherehe binafsi?

Ushauri kwa Vyuo Vikuu

Ni vyema vyuo vikuu nchini Tanzania kuangalia upya utaratibu huu, kwani unaonekana kuongeza mzigo kwa wahitimu na unaweza kutafsiriwa kama njia ya kukusanya fedha kimya kimya. Ushauri ni kwamba:
  • Ada ya joho itozwe kwa wanafunzi wanaoshiriki mahafali pekee.
  • Wahitimu ambao hawakuhudhuria mahafali wasitozwe gharama ya joho wanapokwenda kuchukua vyeti vyao.
Utaratibu huu utapunguza malalamiko, kuongeza uwazi, na kuondoa hisia za kudhulumiwa kwa wahitimu.
 
Back
Top Bottom