Wahubiri wangu wa mfano Tanzania

William Marrion Branham ndo no 1 kwangu.
Hata Uebert Angel anakiri kwamba Branham hakua mtu wa kawaida.
Nilikisoma kitabu cha Historia ya maisha na huduma yake. Kina shuhuda za kushangaza sana! Mwacheni Mungu aitwe Mungu!!!
 
Bila kumweka Sheikh Kipozeo mzee wa mizigo hii list ni batili...
 
Wote hawa bado sijaona wa kumzidi yule nimpendae na ninayemkubali kwa 100% kama Daniel Mgogo mwenye Mahubiri ya Kiuhalisia wa Kimaisha na siyo Unafiki kama walio Wengi.
 
πŸ™πŸ™πŸ™
 
Wote hawa bado sijaona wa kumzidi yule nimpendae na ninayemkubali kwa 100% kama Daniel Mgogo mwenye Mahubiri ya Kiuhalisia wa Kimaisha na siyo Unafiki kama walio Wengi.
Kanisa lake linaitwaje?
 
NotedπŸ™πŸ™πŸ™
 
kwamimi,
Kitaifa...Mwakasege,....
Kimkoa....Abiudi Misholi,
Kiwilaya...Mwamba wa Kikosi Kazi (Mungu amfanyie wepesi huko gerezani..atoke alishe kondoo walio wake). Huyu mwamba nyimbo zake haipiti siku bila kusikiliza, lazima niskilize nyimbo zake hata mbili tu ndipo moyo unapata amani kiasi..ila kuwekwa gerezani kunanitesa hata mimi huku nje.

Kimataifa: Hivi yule Peter Yangren bado yupo huko nje?
 
Kama wote hao unawasikiza unatoa wapi muda wa kufanya kazi mkuu? Sina Nia mbaya
Mimi namfahamu mark Finley (Nje)
Mwakasege Tz
David mbaga Tx sda hasa kwenye afya huyu jamaa namkubali sana.
Sijaanza leo, wala mwaka Jana au Juzi. Ni uwekezaji wa miaka mingi, hasa kwa njia ya vitabu.

Audio na video ndiyo ya miaka ya hivi karibuni. Na uzuri mmoja wa audio, unaweza ukatembea nayo kokote uendako, ukaisikiliza uwapo garini au utembeapo kutoka sehemu moja au nyingine.

Hata vitabu, ni kawaida yangu kuwa na kitabu mkononi kokote niendako. Inapotokea nimepata dakika kumi za kuwa free, nasoma kurasa kadhaa au kusikiliza audio n.k.
 
Mwl Mwakasege hajaexperience wokovu, are you kidding?
Hata mimi ninamshangaa sana mtu anayesema hivyo. Sijui ana shida gani!

Mtu ambaye hajaokoka anawezaje kuwasaidia wengine kuokoka?

Hata hivyo simlaumu kwa sababu inawezekana yeye ana tafsiri yake binafsi ya wokovu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…