Wahubiri wangu wa mfano Tanzania

Wahubiri wangu wa mfano Tanzania

Kama ni msanii na watu wanasaidika kupitia mafundisho yake, basi usanii wake ni mzuri. Hata hivyo, inawezekana sijajua ulichomaanisha kwa neno msanii, labda umemaanisha kinyume cha matumizi ya kawaida ya huo msamiati. Lakini kama ni kinyume chake, utakuwa umekosea.

Mwakasege ni mtumishi wa Mungu anayempenda Mungu.
Hata mwamposa,watu wanapona watu wanataka vitendo sio maneno tu
 
bora hata kuhani musa
Yule kwa mtu mwenye akili timamu hawezi kaa chini na kumsikiloza Kuhani Musa. Ni bora mara sabini nirudi kunuwa ulanzi kuliko kwenda kusali kwa Kuhani Musa,Mwamposa, Sijui shilla au Bashando au Yule mama Shaboka au mtalemwa au Masanja. Bora nirudi kwenye umalaya wangu wa zamani tu kuliko kukaa pale niwasikilize. Eti unamsikiliza Maboya, Mgogo, Kapora, Mashimo, Geordavie, Malisa au mchungaji sijui Mtume au nabii wa namna hii.
FB_IMG_1700393713300.jpg
 
Unamfahamu Aaron B. C. Mabondo? Hebu dadavua kidogo mkuu! Ni kati ya watumishi wa Mungu niliowakubali sana.

~ Alimpenda sana Mungu

~ Aliwaheshimu watumishi wenzake bila kujali utofauti wa madhehebu yao

~ Alikuwa mnyenyekevu sana

~ Alikuwa na imani katika NENO la Mungu. Japo hakuwa mtu wa media na hakupenda kujitangaza, kuna watu wengi walisaidika sana kupitia huduma yake, mfano:
1. Kumfufua Kanali wa JWTZ mkoani Arusha. Siku hiyo alikuwa Arusha katika Kanisa la KLPT Kaloleni alipopigiwa simu na mke wa marehemu ili akamsaidie kuupeleka mwili mochwari. Lakini alipofika, alimwamuru ainuke na ikawa hivyo, tena, akiwa hana hata chembe ya maumivu.

2. Dar Es Salaam nako pia alimfufua mtu.

3. Alipopelekwa hospitalini baada ya kivunjika mguu kwa ajali ya gari, daktari alipomwambia atakaa hospitalini mwezi mmoja alikataa. Alisema ana kazi nyingi hivyo atatoka baada ya siku tatu. Na kweli, siku ya tatu iligundulilka kuwa mguu ulishaunga na akaruhusiwa kwenda nyumbani.

Alikuwa ni mtu wa imani hasa. Alimwombea mwanamke aliyekuwa katolewa kizazi na hatimaye akaweza kubeba mimba, alimwombea muathirika wa VVU akapona, n.k.

Ukiweza, soma kitabu cha Historia yake, kinaitwa A WALK OF FAITH.
Mkuu kitabu chake napata wapi?
 
Wa Kimataifa/ toka Mataifa mengine ni hawa:
1. Kenneth Hagin
2. Kenneth Copeland
3. Smith Wigglesworth
4. Dr. David Oyedepo
5. Pastor Chris Oyakilome
6. Uebert Angel
7. T. L. Osborn
8. Gloria Copeland
9. F. F. Bosworth
10. Charles Capps
11. Norvel Hayes
12. Andrew Wommack
13. E. W. Kenyon
14. Jerry Savelle

Kwa Tanzania, ni hawa wafuatao:
1. Aaron B. C. Mabondo
Kwa sasa ni marehemu. Alikuwa katibu Mkuu wa Kanisa la Pentekoste Tanzania. Nilimfahamu kwa mara ya kwanza mwaka 2003, mwezi June, nilipohudhuria Camp iliyoandaliwa na NEW LIFE BAND ya jijini Arusha na kufanyikia katika shule ya Sekondari Moshi mkoani Kilimanjaro.

Nilibarikiwa na masomo yake ya Imani na jinsi alivyokuwa akiishi Imani yake. Baada ya kuaga dunia, nilifanikiwa kukisoma kitabu cha Historia ya maisha yake. Nimevutiwa na misimamo yake ya kiimani, kiasi cha kutokukubali kuwekewa mipaka ya kidhehebu.

Inasemekana, kupitia mafundisho yake, alichochea "uamsho" kwenye Makanisa yasiyokuwa ya Kipentekoste, kama Moravian, Anglikana, n.k. Huwa ninabarikiwa sana na wahubiri wanaolisambaza Neno la Mungu bila kuzingatia mipaka ya madhehebu yao. Msimamo wa Mabondo ulikuwa kwamba hakutumwa kuyahubiria madhehebu, bali kila kiumbe. Kwa hiyo alikuwa yupo tayari kuhubiri popote, bila kujali dhehebu litakalomwalika.

2. Dr. Mosses Kulola
Aliifanya huduma yake kwa uaminifu mkubwa sana. Hakuwa akitafuta maslahi yake binafsi. Alikuwa tayari kuhubiri hata katika mazingira magumu. Alikuwa ni mtu wa lengo moja tu maishani mwake, KUHUBIRI INJILI.

3. Mwl Christopher Mwakasege
Tokea aanze huduma, amekuwa "focused" kwenye hiyo huduma. Angeweza kufanya shughuli zingine za kiuchumi, hasa ukizingatia kuwa ni msomi wa Uchumi, lakini kwa kuwa ameukubali wito wa KULIFUNDISHA Neno la Mungu, ameamua kuachana na vingine vyote na kubaki na kimoja tu, huduma aliyoitiwa.

Kingine ninachompendea, ni tabia yake ya kutokuendekeza "udini". Timu ya huduma yake inadhihirisha hilo. Ina wahudumu kutoka madhehebu mablimbali yaliyopo Tanzania.

Kwa ufahamu wangu, yeye ni miongoni mwa wahubiri wachache walioweza kukivuka kiunzi cha udhehebu nchini Tanzania.

4. Mch. Elyona Kimaro
Japo sijamfuatilia sana, lakini kwa vipindi vyake vichache nilivyovitazama kupitia Upendo TV, amenibariki kwa kweli. Ni kiongozi mzuri. Kiongozi huona hitaji na kutafuta kulitimiza kabla ya kuambiwa. Ndivyo alivyofanya Kimaro kwenye Kanisa analoliongoza, ametafuta jinsi ya kukata kiu ya kiroho ya watu wake.

5. Dr. Augustine Mpemba
Ni Mtanzania anayeishi Marekani. Alikuwa Askofu wa Kanisa la TFE Jijini Mwanza, lakini sijui kama angali kiongozi wa hilo Kanisa kwa sasa. Nilishakisoma kitabu chake kimoja, na nilishasikiliza mtandaoni mafundisho yake kadhaa. Ana uelewa mpana wa mambo ya kiroho na kijamii. Madhalani, yupo vizuri sana kwenye masomo ya IMANI, masomo ambayo ni adimu sana katika Makanisa mengi ya Tanzania.

6. Prosper Ntepa
Sijawahi kusikiliza mahubiri yake, lakini nimevisoma vitabu kadhaa alivyoviandika. Kuna kimoja kinachohusiana na uponyaji, nilikipenda sana. Ni Mwalimu mzuri sana kwenye somo la Imani. Na kama ilivyo kwa tabia ya walimu wengi, yeye naye ni msomaji mzuri sana wa Vitabu.

7. Pastor Famous
Huyu ni Mchungaji wa Winners Chapel Jijini Mwanza. Nafikiri ni Mnigeria, alikuwa akiliongoza Kanisa la Winners Chapel lililopo Pasiansi jijini Mwanza. Sijui kama bado yupo pale au la.

8. Dr. Barnaba Mtokambali
Ni Askofu Mkuu wa TAG na pia ni Rais wa Makanisa ya Assemblies barani Afrika. Kama hiyo haitoshi, ni Mwenyekiti wa Makanisa ya Kipentekoste Tanzania.

Ana maono ya kiuongozi. Si bure CPCT wamempa Uenyekiti.

NB. Naweza nisiwe nakubaliana na kila kitu kwa baadhi ya hao watumishi wa Mungu, lakini kwa kuamua kuwataja kama miongoni mwa wahubiri wangu wa mfano, ni kwa sababu kuna maeneo wamenibariki.

Na, katika wahubiri woote, "my favourite" ni KENNETH HAGIN. Japo alishaaga dunia tokea mwaka 2003, vitabu vyake vimenisaidia sana , hasa katika eneo la IMANI.

Hatujawahi kukutana ana kwa ana, lakini kupitia vitabu vyake, amekuwa kama baba kwangu. Nimeshavisoma zaidi ya vitabu vyake hamsini. Nimeshavisoma karibia vitabu vyote alivyoviandika. Ni vichache sana ndiyo bado.

Tuwekee na wewe watumishi au viongozi wa dini unaowachukulia kama watumishi wa Mungu au viongozi wa mfano kwako.

Karibu!!!
Hao wote ni matapeli wa kidini wanatumia dini kujinufaisha
 
Kwenye list yako, wa kimataifa 90% ni fake. Local 70% fake.
Tusaidie na majina yao tuwatambue kama walivyoandikwa hapa. Usiishie kuandika %. Hivi hutusaidii tunaofuatilia Kutaka kujua tofauti yao: real&fake.
 
Kwa Mungu hakuna huyu mtumishi ndio Bora kuliko wengine. Mungu amempatia kila mmoja karama yake, na huwezi kushindanisha karama na kuanza kuwashindanisha watumishi.

Na mara nyingi tunapotoka kwa kulazimisha kwamba watumishi maarufu ndio waziri kuliko wengine. Mtumishi akisha kuwa na you tube channel au redio basi ndio anaitwa Bora.

Kuna siku nilikuwa nasikiliza Mwalimu Mwakasege, akasema Kuna siku Mchungaji wa Kanisa alimfuata akamwuliza , Kama Mwakasege akiwa kwenye ibada huwa anafuatilia mahubiri ya watumishi wengine. Mwakasege akamjibu kuwa huwa anafuatilia Sana na Kuna mambo mengi anayapata.

Point ya Mwakasege ni kwamba kila mtumishi kawekewa kitu chake tofauti hivyo huwezi kuanza kuwarank huyu ni Bora huyu sio Bora ( hii happy kwa manabii matapeli).

Mimi miaka ya Nyuma nilikuwa najua Askofu Kulola ndio mwanzilishi wa Upentekoste, ila nilipokuja kusoma historia ya Upentekoste nikagundua kumbe kulikuwa Kuna watumishi wakubwa miaka ya nyuma walioanzisha Upentekoste, tatizo hawakuwa maarufu.

Kwa mfano miaka ya 1935 kipindi Cha ukoloni kulikuwa na mwinjilisti mkubwa Sana alihubiri maeneo mengi Sana alikuwa anaitwa Harris Kapiga. Na wengine wengi akiwemo Mzee Andrea shimba ila hawakuwa maarufu. So nashauri tuachane na roho ya mashindano ndani ya kanisa , na kila mmoja afanye kwa kadri alivyopewa na Mungu.
Uko sahihi sana. Nafkiri mada ilitakiwa kuzitaja kazi za watumishi na si kulinganisha sifa bila vigezo.
Nitatoa mfano, Paulo, mtumwa wa Yesu Kristo anasema yeye ni zaidi ya wale thenashara. Lakini zaidi katika nini? Ni katika kufungwa, katika kufunga, katika dhoruba na katika mapigo. Yaani zaidi katika taabu ya injili. Lakini pia yeye ndiye aliyefanya kazi ya kusambaza injili zaidi kwa mataifa. Lakini pamoja na yote hakuwadharau wenzake, isipokuwa aliwaonya kwa upendo.

Pia, ikumbukwe hizi karama za roho hutolewa na roho kadri apendavyo roho mtakatifu. Mwingine mwalimu, mwinjilisti, utume na unabii.

Neno linatuagiza tuzijaribu kila roho, tupime au tuwatambue watumishi kwa matunda yao na maisha yao kwa ujumla. Na pia tuangalie nani kawaachia joho, yaani tuangalie baba zao wa kiroho.

Paulo aliitwa na Yesu akapewa Philipo, kuna Elisha na Eliya, kuna Musa na Haroun, Joshua na Caleb, kuna Paulo na Timotheo. Watoto wa Kulola na Lazaro unapata TAG / EAGT hapo kwa DSM hapo ma nguli kama Katunzi, Kakobe na wengi ambao wameanzisha huduma na zimesimama imara mpaka sasa.

Hivi ndivyo vipimo vya kibiblia. Ni muhimu kukumbuka kuwa hiyo ni mifano michache. Wapo watumishi wa Mungu wanafanya kazi kubwa hasa vijijini na wanatumika kweli kweli lakini hawaimbwi sana masikioni mwa watu. Ukiwa mfatiliaji wa injili utalielewa hili.
 
Uebert Angel alinijibu swali ambalo niliwauliza watalaamu wa theologia wakatoa majibu ambayo sijawahi kuridhika ,huyu mwamba alifundisha "the origin of God ".Toka nikiwa mdogo nilikuwa nauliza Mungu alitoka wapi na anakaa wapi.Huyu mwamba alijibu haya maswali mawili nikanyanyua mikono juu .
Alikujibuje?
 
Kasikilize mkuu utafaidika zaidi ina part one na two ni kitu kizito kuandika inachukua muda.
Huu ni ujinga wa kiroho. Neno la Mungu halifichwi. Neno ni gharama lakini tunalitoa bure kwa kuwa tumepewa bure na Mungu.
 
Pastor Daniel Mgogo
Yuko vizuri sana ila kuna ujasiliamali wa injili huwa wanaufanya. Yaani wanaangalia watu wanataka kusikia nini. Yaani wanafata masikio ya utafiti ya watu. Wanagusa matatizo ya ndoa na mahusiano kuliko dhambi.
 
Je? Kuna watumishi wa mungu ukifka tu wanataja matatizo yako before ujawaelezea? Hii imekaaje wataalam??

Sent from my SM-A042F using JamiiForums mobile app
Kuna contest.
Mungu akimfunulia hivyo mtumishi lazima utukufu uende kwa Mungu na si kwa Mtumishi. Ukiona hiyo ndiyo inakuwa huduma maalumu tena mathalani ikawa inalipiwa kwa kiasi fulani cha pesa. Ujue kuna hila hata kama kuna injili ya kweli.
 
Lakini nafikiri hakumaanisha hivyo. Alilenga fikra, kwamba kama wazo ovu halipo moyoni mwa mtu, hawezi kufanya uovu. Kwa hiyo, kama mtu hafikirii hicho, kamwe hawezi kufanya.

Nimeitafuta clip yake mtandaoni baada ya kuiona comment yako. Hamaanishi watu wajichue, bali wasiwe na hizo fikra.
Dhambi hata ukimtamani mwanamke hakika umekwisha kuzini nae.
 
Back
Top Bottom