Wahubiri wangu wa mfano Tanzania

Wahubiri wangu wa mfano Tanzania

Uebert Angel alinijibu swali ambalo niliwauliza watalaamu wa theologia wakatoa majibu ambayo sijawahi kuridhika ,huyu mwamba alifundisha "the origin of God ".Toka nikiwa mdogo nilikuwa nauliza Mungu alitoka wapi na anakaa wapi.Huyu mwamba alijibu haya maswali mawili nikanyanyua mikono juu .
Alikujibuje huyo mwamba? Tuwekee jibu na sisi tunufaike.
 
Wa Kimataifa/ toka Mataifa mengine ni hawa:
1. Kenneth Hagin
2. Kenneth Copeland
3. Smith Wigglesworth
4. Dr. David Oyedepo
5. Pastor Chris Oyakilome
6. Uebert Angel
7. T. L. Osborn
8. Gloria Copeland
9. F. F. Bosworth
10. Charles Capps
11. Norvel Hayes
12. Andrew Wommack
13. E. W. Kenyon
14. Jerry Savelle

Kwa Tanzania, ni hawa wafuatao:
1. Aaron B. C. Mabondo
Kwa sasa ni marehemu. Alikuwa katibu Mkuu wa Kanisa la Pentekoste Tanzania. Nilimfahamu kwa mara ya kwanza mwaka 2003, mwezi June, nilipohudhuria Camp iliyoandaliwa na NEW LIFE BAND ya jijini Arusha na kufanyikia katika shule ya Sekondari Moshi mkoani Kilimanjaro.

Nilibarikiwa na masomo yake ya Imani na jinsi alivyokuwa akiishi Imani yake. Baada ya kuaga dunia, nilifanikiwa kukisoma kitabu cha Historia ya maisha yake. Nimevutiwa na misimamo yake ya kiimani, kiasi cha kutokukubali kuwekewa mipaka ya kidhehebu.

Inasemekana, kupitia mafundisho yake, alichochea "uamsho" kwenye Makanisa yasiyokuwa ya Kipentekoste, kama Moravian, Anglikana, n.k. Huwa ninabarikiwa sana na wahubiri wanaolisambaza Neno la Mungu bila kuzingatia mipaka ya madhehebu yao. Msimamo wa Mabondo ulikuwa kwamba hakutumwa kuyahubiria madhehebu, bali kila kiumbe. Kwa hiyo alikuwa yupo tayari kuhubiri popote, bila kujali dhehebu litakalomwalika.

2. Dr. Mosses Kulola
Aliifanya huduma yake kwa uaminifu mkubwa sana. Hakuwa akitafuta maslahi yake binafsi. Alikuwa tayari kuhubiri hata katika mazingira magumu. Alikuwa ni mtu wa lengo moja tu maishani mwake, KUHUBIRI INJILI.

3. Mwl Christopher Mwakasege
Tokea aanze huduma, amekuwa "focused" kwenye hiyo huduma. Angeweza kufanya shughuli zingine za kiuchumi, hasa ukizingatia kuwa ni msomi wa Uchumi, lakini kwa kuwa ameukubali wito wa KULIFUNDISHA Neno la Mungu, ameamua kuachana na vingine vyote na kubaki na kimoja tu, huduma aliyoitiwa.

Kingine ninachompendea, ni tabia yake ya kutokuendekeza "udini". Timu ya huduma yake inadhihirisha hilo. Ina wahudumu kutoka madhehebu mablimbali yaliyopo Tanzania.

Kwa ufahamu wangu, yeye ni miongoni mwa wahubiri wachache walioweza kukivuka kiunzi cha udhehebu nchini Tanzania.

4. Mch. Elyona Kimaro
Japo sijamfuatilia sana, lakini kwa vipindi vyake vichache nilivyovitazama kupitia Upendo TV, amenibariki kwa kweli. Ni kiongozi mzuri. Kiongozi huona hitaji na kutafuta kulitimiza kabla ya kuambiwa. Ndivyo alivyofanya Kimaro kwenye Kanisa analoliongoza, ametafuta jinsi ya kukata kiu ya kiroho ya watu wake.

5. Dr. Augustine Mpemba
Ni Mtanzania anayeishi Marekani. Alikuwa Askofu wa Kanisa la TFE Jijini Mwanza, lakini sijui kama angali kiongozi wa hilo Kanisa kwa sasa. Nilishakisoma kitabu chake kimoja, na nilishasikiliza mtandaoni mafundisho yake kadhaa. Ana uelewa mpana wa mambo ya kiroho na kijamii. Madhalani, yupo vizuri sana kwenye masomo ya IMANI, masomo ambayo ni adimu sana katika Makanisa mengi ya Tanzania.

6. Prosper Ntepa
Sijawahi kusikiliza mahubiri yake, lakini nimevisoma vitabu kadhaa alivyoviandika. Kuna kimoja kinachohusiana na uponyaji, nilikipenda sana. Ni Mwalimu mzuri sana kwenye somo la Imani. Na kama ilivyo kwa tabia ya walimu wengi, yeye naye ni msomaji mzuri sana wa Vitabu.

7. Pastor Famous
Huyu ni Mchungaji wa Winners Chapel Jijini Mwanza. Nafikiri ni Mnigeria, alikuwa akiliongoza Kanisa la Winners Chapel lililopo Pasiansi jijini Mwanza. Sijui kama bado yupo pale au la.

8. Dr. Barnaba Mtokambali
Ni Askofu Mkuu wa TAG na pia ni Rais wa Makanisa ya Assemblies barani Afrika. Kama hiyo haitoshi, ni Mwenyekiti wa Makanisa ya Kipentekoste Tanzania.

Ana maono ya kiuongozi. Si bure CPCT wamempa Uenyekiti.

NB. Naweza nisiwe nakubaliana na kila kitu kwa baadhi ya hao watumishi wa Mungu, lakini kwa kuamua kuwataja kama miongoni mwa wahubiri wangu wa mfano, ni kwa sababu kuna maeneo wamenibariki.

Na, katika wahubiri woote, "my favourite" ni KENNETH HAGIN. Japo alishaaga dunia tokea mwaka 2003, vitabu vyake vimenisaidia sana , hasa katika eneo la IMANI.

Hatujawahi kukutana ana kwa ana, lakini kupitia vitabu vyake, amekuwa kama baba kwangu. Nimeshavisoma zaidi ya vitabu vyake hamsini. Nimeshavisoma karibia vitabu vyote alivyoviandika. Ni vichache sana ndiyo bado.

Tuwekee na wewe watumishi au viongozi wa dini unaowachukulia kama watumishi wa Mungu au viongozi wa mfano kwako.

Karibu!!!
Wakusanya sadaka tu
 
Kwangu mimi mpaka sasa kwa hapa Tanzania ni hawa.
1. Mwalimu Christopher Mwakasege
2. Pastor Carlos Kirimbai

Jamaa wanaijua bible fresh, wanaisoma kila siku, na wanatamani kila mtu aisome Bible fresh na kuitambua. Yote kwa yote wanakufanya umjue Yesu at personal level bila kubabaishwa na chochote au yoyote.

Naambiwa walifanikiwa kuukwepa upepo wa kidini (kidhehebu) uliokuwa ukivuma vilivyo miaka ya 90, na wamefanikiwa pia kuuvuka huu upepo wa sasa wa tamaa za mali na umungu mtu unaotikisa kanisa la Tz kwa zaidi ya 80%.

Yote kwa yote jamaa wanaweza kukushawishi umjue Yesu na kuijua Bible fresh hata kama wewe sio mkristo au wewe ni mpagani.
Mwakasege ni msanii tu na amewashika wengi wasiojielewa
 
Uebert Angel alinijibu swali ambalo niliwauliza watalaamu wa theologia wakatoa majibu ambayo sijawahi kuridhika ,huyu mwamba alifundisha "the origin of God ".Toka nikiwa mdogo nilikuwa nauliza Mungu alitoka wapi na anakaa wapi.Huyu mwamba alijibu haya maswali mawili nikanyanyua mikono juu .
Badala utoe majibu uliyopewa umeona ni vema kuandika maelezo marefu kuliko majibu mafupi uliyopewa na sisi tukanufaika?

Hao Gold Smaglers wana kupotosha kwa maneno na lugha fasaha.
 
3 &4 ndotop kwenye list yangu kwa hapa tanzania ila nimejipa homework ya kuwapitia mafundisho yao hao waliobaki nami nipate kitu
 
Uebert Angel alinijibu swali ambalo niliwauliza watalaamu wa theologia wakatoa majibu ambayo sijawahi kuridhika ,huyu mwamba alifundisha "the origin of God ".Toka nikiwa mdogo nilikuwa nauliza Mungu alitoka wapi na anakaa wapi.Huyu mwamba alijibu haya maswali mawili nikanyanyua mikono juu .
hiyo ilikuokoa roho yako? knowing the origin of God, si ungesoma tu Biblia, hadi ukasikie kwa nabii, Mungu si amesema yeye ni NIKO AMBAYE NIKO, yaani NI ALFA NA OMEGA, MWANZO NA MWISHO, ulihitaji nini sasa zaidi ya haya? au alikujibuje?

kwa kukusaidia, kuna cults za kikristo zimeibuka siku hizi, wanajifanya wanakutabiria maisha yako, nabii anasimama anaanza kueleza maisha yako, ndugu zako n.k, na wewe unaitikia sema nabii. mambo kama haya sio mageni, waganga wa kienyeji wamekuwa wakifanya tangu enzi, hauhitaji mtu akutabirie ulivyo ili ujue ni mtu wa Mungu, unahitaji ukutane na mguso wa Mungu moyoni mwako akubadilishe moyo wako mazima. mtu akitabiri kwamba mimi naitwa sulemani, natoka arusha, nina mke anaitwa sara, nina watoto fulani na fulani, kwenye wokovu wangu inanisaidia nini? au mimi kujua yeye ni mtu wa Mungu inanisaidia nini? kitakachonisaidia ni pale yeye atakaposimama mbele yangu kama chombo/instrument/zana ya Mungu,Mungu akamtumia, haongei yeye ila Mungu aliyepo ndani yake anaongea maneno ya uzima, sio ya uaguzi. hao wote wanaoagua, kuanzia huyo wa malawi mwenye kijana wake kule makongo juu, wale walioko south africa, wale wa zimbabwe, nigeria na wengine wooote, ni manabii wa uongo, na wanajitahidi sana kuuaminisha umma kwamba wao ni watu wa Mungu kwa kutumia miujiza bila kujua kwamba miujiza sio kipimo cha utauwa, hata shetani ana miujiza. watu kama hawa wamejaa DSM, arusha, mbeya everywhere.
 
Japo mie sio mfuasi wao, ila Hukumu ni ya Mungu peke yake ,

Sent from my HUAWEI KII-L22 using JamiiForums mobile app
umwonapo mtu mbaya anafanya ubaya usimuonye, siku ya mwisho damu yake itadaiwa. haujui hata maana ya mstari huo unaosema usihukumu usije kuhukumiwa wewe. watu kama wewe ndio mnaishi tu mkisubiria siku ya mwisho ifike, unatakiwa kumjua Mungu uponye roho yako.
 
Pastor Joel Senny, Infinity Glory Church, Arusha. Unaweza kufuatilia mafundisho yake YouTube na Facebook
 
Uebert Angel alinijibu swali ambalo niliwauliza watalaamu wa theologia wakatoa majibu ambayo sijawahi kuridhika ,huyu mwamba alifundisha "the origin of God ".Toka nikiwa mdogo nilikuwa nauliza Mungu alitoka wapi na anakaa wapi.Huyu mwamba alijibu haya maswali mawili nikanyanyua mikono juu .
🙏🙏🙏
 
Back
Top Bottom