Kimsingi umewataja wa mtandaoni na wanaosikika sana kwenye media ila bado wapo watumishi wazuri tu humu duniani. Kuna mzee mmoja nilimkuta huko Iringa niliendaga na kuiishi kikazi mwezi mmoja huko Vijijini Dabaga nikawa naabudu kanisa la TAG Kilolo Christian Centre lipo pale Kilolo Wilayani Anaitwa Mzee Lucas Mkuye. Huyo ndio Mtume wa kwanza wa kweli kumuona maishani mwangu.
Mzee alianza huduma 1979 kipindi hiko ukanda wote wa Dabaga hauna kanisa lolote la kipentecoste na alikuwa akitembea kwa miguu hadi Mapanda huko Mufindi na akaanzisha na kusimamisha makanisa ya TAG ukanda huo. Zaidi ya makanisa 60 yametokea mikononi mwake.
Kwa Walutheri tunaoishi au kukulia ulutheri Morogoro au kwa wale tuliosoma Lutheran Junior Seminary miaka ya 1990's tuna mkumbuka Marehemu Mchungaji Hebert Hafferman. Huyu ndio Mtume wa Pili wa kweli kumuona kwa macho yangu achana na akina Bashando na Daudi Mashimo.
Mzee yule alikuwa mzungu na alikuja TZ miaka ya 1950's na alisambaza Ulutheri kwa kiasi kikubwa kwenye jamii ya kimasai. Aliwekeza kwenye huduma ya Neno na masuala ya kijamii ikiwemo kuwasomesha wamasai wengi wa Morogoro. Zao lake mmojawapo ni Richard Mameo Askofu wa Lutheran hapa Morogoro. R.I.P HEBERT HAFFERMAN, tutakutana katika pambazuko lile katika siku ile ya kalamu ya mwanakondoo.
Picha ya Marehemu mzee Hebert Hafferman akiwa na mtoto wa mchungaji mmoja wa Kimasai Marehemu Lucas.
View attachment 2818389