Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Hawa ndio mkuu wao wa kanisa kasema ruksa jinsia moja kutinduana?.Wapo pia mapadre wa kanisa katoliki na maaskofu walio wazuri sana katika kufundisha neno la Mungu ila kwa vile sio popular hawawezi kutajwa hapa .
Huyo tapeli la kutupwaVp Kiboko ya wachawi ,mwenye kanisa Buza
Jamaa namskilizaga Furaha FM 90.9
Baba wa kiroho wa Makandiwa sio huyo yuko Ghana na mwanzo walipoanza huduma walikuwa wanashare ila baadae mambo yaka badilika juu kwa juu...Ukiwa unawafuatilia utawaelewa tu.Pastor Chris ndio Baba wa kiroho wa huyu tapeli na gold smuggler. Yeye nae akawa na kina Bushiri, makandiwa, mtalemwa, tonny na wengine kibao. Huyo jamaa ni charlatan wa kutupwa.
Wa Kimataifa/ toka Mataifa mengine ni hawa:
1. Kenneth Hagin
2. Kenneth Copeland
3. Smith Wigglesworth
4. Dr. David Oyedepo
5. Pastor Chris Oyakilome
6. Uebert Angel
7. T. L. Osborn
8. Gloria Copeland
9. F. F. Bosworth
10. Charles Capps
11. Norvel Hayes
12. Andrew Wommack
13. E. W. Kenyon
14. Jerry Savelle
Kwa Tanzania, ni hawa wafuatao:
1. Aaron B. C. Mabondo
Kwa sasa ni marehemu. Alikuwa katibu Mkuu wa Kanisa la Pentekoste Tanzania. Nilimfahamu kwa mara ya kwanza mwaka 2003, mwezi June, nilipohudhuria Camp iliyoandaliwa na NEW LIFE BAND ya jijini Arusha na kufanyikia katika shule ya Sekondari Moshi mkoani Kilimanjaro.
Nilibarikiwa na masomo yake ya Imani na jinsi alivyokuwa akiishi Imani yake. Baada ya kuaga dunia, nilifanikiwa kukisoma kitabu cha Historia ya maisha yake. Nimevutiwa na misimamo yake ya kiimani, kiasi cha kutokukubali kuwekewa mipaka ya kidhehebu.
Inasemekana, kupitia mafundisho yake, alichochea "uamsho" kwenye Makanisa yasiyokuwa ya Kipentekoste, kama Moravian, Anglikana, n.k. Huwa ninabarikiwa sana na wahubiri wanaolisambaza Neno la Mungu bila kuzingatia mipaka ya madhehebu yao. Msimamo wa Mabondo ulikuwa kwamba hakutumwa kuyahubiria madhehebu, bali kila kiumbe. Kwa hiyo alikuwa yupo tayari kuhubiri popote, bila kujali dhehebu litakalomwalika.
2. Dr. Mosses Kulola
Aliifanya huduma yake kwa uaminifu mkubwa sana. Hakuwa akitafuta maslahi yake binafsi. Alikuwa tayari kuhubiri hata katika mazingira magumu. Alikuwa ni mtu wa lengo moja tu maishani mwake, KUHUBIRI INJILI.
3. Mwl Christopher Mwakasege
Tokea aanze huduma, amekuwa "focused" kwenye hiyo huduma. Angeweza kufanya shughuli zingine za kiuchumi, hasa ukizingatia kuwa ni msomi wa Uchumi, lakini kwa kuwa ameukubali wito wa KULIFUNDISHA Neno la Mungu, ameamua kuachana na vingine vyote na kubaki na kimoja tu, huduma aliyoitiwa.
Kingine ninachompendea, ni tabia yake ya kutokuendekeza "udini". Timu ya huduma yake inadhihirisha hilo. Ina wahudumu kutoka madhehebu mablimbali yaliyopo Tanzania.
Kwa ufahamu wangu, yeye ni miongoni mwa wahubiri wachache walioweza kukivuka kiunzi cha udhehebu nchini Tanzania.
4. Mch. Elyona Kimaro
Japo sijamfuatilia sana, lakini kwa vipindi vyake vichache nilivyovitazama kupitia Upendo TV, amenibariki kwa kweli. Ni kiongozi mzuri. Kiongozi huona hitaji na kutafuta kulitimiza kabla ya kuambiwa. Ndivyo alivyofanya Kimaro kwenye Kanisa analoliongoza, ametafuta jinsi ya kukata kiu ya kiroho ya watu wake.
5. Dr. Augustine Mpemba
Ni Mtanzania anayeishi Marekani. Alikuwa Askofu wa Kanisa la TFE Jijini Mwanza, lakini sijui kama angali kiongozi wa hilo Kanisa kwa sasa. Nilishakisoma kitabu chake kimoja, na nilishasikiliza mtandaoni mafundisho yake kadhaa. Ana uelewa mpana wa mambo ya kiroho na kijamii. Madhalani, yupo vizuri sana kwenye masomo ya IMANI, masomo ambayo ni adimu sana katika Makanisa mengi ya Tanzania.
6. Prosper Ntepa
Sijawahi kusikiliza mahubiri yake, lakini nimevisoma vitabu kadhaa alivyoviandika. Kuna kimoja kinachohusiana na uponyaji, nilikipenda sana. Ni Mwalimu mzuri sana kwenye somo la Imani. Na kama ilivyo kwa tabia ya walimu wengi, yeye naye ni msomaji mzuri sana wa Vitabu.
7. Pastor Famous
Huyu ni Mchungaji wa Winners Chapel Jijini Mwanza. Nafikiri ni Mnigeria, alikuwa akiliongoza Kanisa la Winners Chapel lililopo Pasiansi jijini Mwanza. Sijui kama bado yupo pale au la.
8. Dr. Barnaba Mtokambali
Ni Askofu Mkuu wa TAG na pia ni Rais wa Makanisa ya Assemblies barani Afrika. Kama hiyo haitoshi, ni Mwenyekiti wa Makanisa ya Kipentekoste Tanzania.
Ana maono ya kiuongozi. Si bure CPCT wamempa Uenyekiti.
NB. Naweza nisiwe nakubaliana na kila kitu kwa baadhi ya hao watumishi wa Mungu, lakini kwa kuamua kuwataja kama miongoni mwa wahubiri wangu wa mfano, ni kwa sababu kuna maeneo wamenibariki.
Na, katika wahubiri woote, "my favourite" ni KENNETH HAGIN. Japo alishaaga dunia tokea mwaka 2003, vitabu vyake vimenisaidia sana , hasa katika eneo la IMANI.
Hatujawahi kukutana ana kwa ana, lakini kupitia vitabu vyake, amekuwa kama baba kwangu. Nimeshavisoma zaidi ya vitabu vyake hamsini. Nimeshavisoma karibia vitabu vyote alivyoviandika. Ni vichache sana ndiyo bado.
Tuwekee na wewe watumishi au viongozi wa dini unaowachukulia kama watumishi wa Mungu au viongozi wa mfano kwako.
Karibu!!!
Matapeli yamekuwa mengi sana. Waumini maamuma lazima wanaswe kwenye hizo vilinge vyao. Shetani naye anayo Mazingaombwe yake wengi wamekufa kwa kutafuta miujiza fake.hakuna kupepesa macho kwa matapeli, wenyewe wanajijua. injili yao hata kwenye Biblia haipo. huyo kuhani mtoto wa yesu wa mkombo aliyefukuziwa congo huyo, na mwamposa anajua alikotoka. washindwe kwa Jina la Yesu.
Oh its true, anaitwa prophet Victor kussi Boateng nimekumbuka.Hizi ni nyakati za mwisho. Bibilia inasema nyakati za mwisho zitakuwa za hatari, maana watu watayakataa mafundisho yenye uzima na kugeukia mafundisho ya mashetani na maagizo ya kibinadamu nao watajipatia waalimu makundi makundi kwa kuwa wana masikio ya utafiti. Siku hizo ndo siku hizi sasaBaba wa kiroho wa Makandiwa sio huyo yuko Ghana
Aisee!Tapeli , baba wa manabii feki
Mimi nimewaweka wa kwangu, na wewe waweke wa kwako.Dkt Mwampo... Sijamuona kwenye list
Umenena vyema✅🙏Japo mie sio mfuasi wao, ila Hukumu ni ya Mungu peke yake ,
Sent from my HUAWEI KII-L22 using JamiiForums mobile app
Nini kilichokuvutia kwake?Mchg Hananja naye yumo.
Kwa sababu hujamwekaMbin kweli list hayupo?
😃😃😃Nilisema hvo bse Aligawa pesa kwa waumini walouzuria crusade leaders akisema zinatoka Baharini... Na sote tunajua ufalme wa giza unamakao huko Baharini... Ila kibaya zaidi injili anayohubiri haiko balanced... Mafanikio kwa Sana ila swala la utakatifu hamna au kidogo.
4. Mch. Elyona Kimaro
Japo sijamfuatilia sana, lakini kwa vipindi vyake vichache nilivyovitazama kupitia Upendo TV, amenibariki kwa kweli. Ni kiongozi mzuri. Kiongozi huona hitaji na kutafuta kulitimiza kabla ya kuambiwa. Ndivyo alivyofanya Kimaro kwenye Kanisa analoliongoza, ametafuta jinsi ya kukata kiu ya kiroho ya watu wake.
Z. KakobeKwangu mimi mpaka sasa kwa hapa Tanzania ni hawa.
1. Mwalimu Christopher Mwakasege
2. Pastor Carlos Kirimbai
Jamaa wanaijua bible fresh, wanaisoma kila siku, na wanatamani kila mtu aisome Bible fresh na kuitambua. Yote kwa yote wanakufanya umjue Yesu at personal level bila kubabaishwa na chochote au yoyote.
Naambiwa walifanikiwa kuukwepa upepo wa kidini (kidhehebu) uliokuwa ukivuma vilivyo miaka ya 90, na wamefanikiwa pia kuuvuka huu upepo wa sasa wa tamaa za mali na umungu mtu unaotikisa kanisa la Tz kwa zaidi ya 80%.
Yote kwa yote jamaa wanaweza kukushawishi umjue Yesu na kuijua Bible fresh hata kama wewe sio mkristo au wewe ni mpagani.
Pastor Carlos Kirimbai wa Tanzania, yuko hapo Dar, miaka mingi ya nyuma alikuwa akifanya kazi ya ukalimani katika mikutano ya Injili iliyokuwa inawaleta wahubiri mbali mbali wa kimaitafa hapa Tanzania mfano akina Bhonke. Kwa sasa muda mwingi anakuwa anafundisha na kuhubiri hapo Dar akitumia madarasa ya shule ya sekondari ya Kisutu, mjini kati na akishare free mafundisho yake kupitia mitandao ya kijamii ikiwemo whatsapp. Ni jamaa fulani hivi hana makuu lakini anapeo fresh wa bible na jamii.Pastor Carlos Kirimbai ni wa wapi?
Uebert Angel
Mwamba huyu mchambuzi wa Bible na misimamo mikaliWa Kimataifa/ toka Mataifa mengine ni hawa:
1. Kenneth Hagin
2. Kenneth Copeland
3. Smith Wigglesworth
4. Dr. David Oyedepo
5. Pastor Chris Oyakilome
6. Uebert Angel
7. T. L. Osborn
8. Gloria Copeland
9. F. F. Bosworth
10. Charles Capps
11. Norvel Hayes
12. Andrew Wommack
13. E. W. Kenyon
14. Jerry Savelle
Kwa Tanzania, ni hawa wafuatao:
1. Aaron B. C. Mabondo
Kwa sasa ni marehemu. Alikuwa katibu Mkuu wa Kanisa la Pentekoste Tanzania. Nilimfahamu kwa mara ya kwanza mwaka 2003, mwezi June, nilipohudhuria Camp iliyoandaliwa na NEW LIFE BAND ya jijini Arusha na kufanyikia katika shule ya Sekondari Moshi mkoani Kilimanjaro.
Nilibarikiwa na masomo yake ya Imani na jinsi alivyokuwa akiishi Imani yake. Baada ya kuaga dunia, nilifanikiwa kukisoma kitabu cha Historia ya maisha yake. Nimevutiwa na misimamo yake ya kiimani, kiasi cha kutokukubali kuwekewa mipaka ya kidhehebu.
Inasemekana, kupitia mafundisho yake, alichochea "uamsho" kwenye Makanisa yasiyokuwa ya Kipentekoste, kama Moravian, Anglikana, n.k. Huwa ninabarikiwa sana na wahubiri wanaolisambaza Neno la Mungu bila kuzingatia mipaka ya madhehebu yao. Msimamo wa Mabondo ulikuwa kwamba hakutumwa kuyahubiria madhehebu, bali kila kiumbe. Kwa hiyo alikuwa yupo tayari kuhubiri popote, bila kujali dhehebu litakalomwalika.
2. Dr. Mosses Kulola
Aliifanya huduma yake kwa uaminifu mkubwa sana. Hakuwa akitafuta maslahi yake binafsi. Alikuwa tayari kuhubiri hata katika mazingira magumu. Alikuwa ni mtu wa lengo moja tu maishani mwake, KUHUBIRI INJILI.
3. Mwl Christopher Mwakasege
Tokea aanze huduma, amekuwa "focused" kwenye hiyo huduma. Angeweza kufanya shughuli zingine za kiuchumi, hasa ukizingatia kuwa ni msomi wa Uchumi, lakini kwa kuwa ameukubali wito wa KULIFUNDISHA Neno la Mungu, ameamua kuachana na vingine vyote na kubaki na kimoja tu, huduma aliyoitiwa.
Kingine ninachompendea, ni tabia yake ya kutokuendekeza "udini". Timu ya huduma yake inadhihirisha hilo. Ina wahudumu kutoka madhehebu mablimbali yaliyopo Tanzania.
Kwa ufahamu wangu, yeye ni miongoni mwa wahubiri wachache walioweza kukivuka kiunzi cha udhehebu nchini Tanzania.
4. Mch. Elyona Kimaro
Japo sijamfuatilia sana, lakini kwa vipindi vyake vichache nilivyovitazama kupitia Upendo TV, amenibariki kwa kweli. Ni kiongozi mzuri. Kiongozi huona hitaji na kutafuta kulitimiza kabla ya kuambiwa. Ndivyo alivyofanya Kimaro kwenye Kanisa analoliongoza, ametafuta jinsi ya kukata kiu ya kiroho ya watu wake.
5. Dr. Augustine Mpemba
Ni Mtanzania anayeishi Marekani. Alikuwa Askofu wa Kanisa la TFE Jijini Mwanza, lakini sijui kama angali kiongozi wa hilo Kanisa kwa sasa. Nilishakisoma kitabu chake kimoja, na nilishasikiliza mtandaoni mafundisho yake kadhaa. Ana uelewa mpana wa mambo ya kiroho na kijamii. Madhalani, yupo vizuri sana kwenye masomo ya IMANI, masomo ambayo ni adimu sana katika Makanisa mengi ya Tanzania.
6. Prosper Ntepa
Sijawahi kusikiliza mahubiri yake, lakini nimevisoma vitabu kadhaa alivyoviandika. Kuna kimoja kinachohusiana na uponyaji, nilikipenda sana. Ni Mwalimu mzuri sana kwenye somo la Imani. Na kama ilivyo kwa tabia ya walimu wengi, yeye naye ni msomaji mzuri sana wa Vitabu.
7. Pastor Famous
Huyu ni Mchungaji wa Winners Chapel Jijini Mwanza. Nafikiri ni Mnigeria, alikuwa akiliongoza Kanisa la Winners Chapel lililopo Pasiansi jijini Mwanza. Sijui kama bado yupo pale au la.
8. Dr. Barnaba Mtokambali
Ni Askofu Mkuu wa TAG na pia ni Rais wa Makanisa ya Assemblies barani Afrika. Kama hiyo haitoshi, ni Mwenyekiti wa Makanisa ya Kipentekoste Tanzania.
Ana maono ya kiuongozi. Si bure CPCT wamempa Uenyekiti.
NB. Naweza nisiwe nakubaliana na kila kitu kwa baadhi ya hao watumishi wa Mungu, lakini kwa kuamua kuwataja kama miongoni mwa wahubiri wangu wa mfano, ni kwa sababu kuna maeneo wamenibariki.
Na, katika wahubiri woote, "my favourite" ni KENNETH HAGIN. Japo alishaaga dunia tokea mwaka 2003, vitabu vyake vimenisaidia sana , hasa katika eneo la IMANI.
Hatujawahi kukutana ana kwa ana, lakini kupitia vitabu vyake, amekuwa kama baba kwangu. Nimeshavisoma zaidi ya vitabu vyake hamsini. Nimeshavisoma karibia vitabu vyote alivyoviandika. Ni vichache sana ndiyo bado.
Tuwekee na wewe watumishi au viongozi wa dini unaowachukulia kama watumishi wa Mungu au viongozi wa mfano kwako.
Karibu!!!
Unamfahamu Aaron B. C. Mabondo? Hebu dadavua kidogo mkuu! Ni kati ya watumishi wa Mungu niliowakubali sana.Mzee Mabondo umenikumbusha mbali sana mkuu, Mungu ampumzishe salama. [emoji120]