GoldDhahabu
JF-Expert Member
- Apr 29, 2023
- 7,189
- 10,375
- Thread starter
- #81
Ingekuwa vizuri kama ungewataja unaoamini ni real.Kwenye list yako, wa kimataifa 90% ni fake. Local 70% fake.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Ingekuwa vizuri kama ungewataja unaoamini ni real.Kwenye list yako, wa kimataifa 90% ni fake. Local 70% fake.
You are right sir! Wanasema "like the father like the son". Kama niliona mhubiri ananitia mashaka, namfuatilia mentor/ baba yake wa kiroho. Nitakachobaini kwa hiyo ndicho kitskachonofanya niendelee kumfuatilia huyo au la.Baba wa kiroho wa Makandiwa sio huyo yuko Ghana na mwanzo walipoanza huduma walikuwa wanashare ila baadae mambo yaka badilika juu kwa juu...Ukiwa unawafuatilia utawaelewa tu.
Leo hii issue ya Fatherhood imenikumbusha jambo..Hivi unajia watumishi wengi wanasomeka sana katika ulimwengu wa roho kirahisi depending na Mababa wa Kiroho? Hata kushambiliwa hutegemea weakness za hao Mababa wa Kiroho..Choose your spiritual Father with full directives of Holy Spirit ukichagua kisa anafundisha na anawatu wengi au anawatoto wengi wa Kiroho inaweza kukupa shida mbeleni.
Hongera sana kwa vitabu ulivo visoma mtoa mada.Kuna njia nzuri sana kupitia hivi vitabu na mafundisho eidha ya audio au video vikiwa kwa uthabiti na kweli vimevuviwa na Master(Holy Spirit) kuwa imparted ndani ya spirit yamfuatiliaji ni kwa urahisi sana kama vile mapepo mengine yanavyo attack watu kupitia novels movies hata musics.
Hope namna yako ya kuamini sio ya kawaida maana watumishi hawa uliowataja wako deep mno katika issue za Faith.Hongera sana.
Mukabwa si wa Dar Es Salaam, mmiliki wa Duka la Vitabu liitwalo HOUSE OF WISDOM BOOKSHOP maeneo ya Posta, Samora Avenue? Au nimemfananisha?Yupo huyu Baba wakuitwa George Mukabwa yupo Mwanza tenga Mda wako umsikilize. Hutojutia
🙏🙏🙏Huyu ni mchungaji kweli ila hana Injili, huwezi kumweka kundi moja na Kulola aisee, Huyu, Mitimingi na Toni Kapola hawana tofauti
Pr Mbaga wa Adventista ni far better kuliko huyu
Haya ni maoni Yangu
🙏🙏🙏Fr Titus Amigu, namsikilizaga radio maria Tanzania , jamaa anahubiri na ana logic kubwa sana kwenye mafundisho yake.
Ni nani huyo mkuu? Wengine tupo huku mikoani. Buza "tunapasikiaga" tu.Vp Kiboko ya wachawi ,mwenye kanisa Buza
Jamaa namskilizaga Furaha FM 90.9
Mkuu, binafsi simfahamu Pr Mbaga. Unaweza ukamwelezea kidogo? Huenda kuna mtu anaweza akawa anahitaji "huduma" yake.Huyu ni mchungaji kweli ila hana Injili, huwezi kumweka kundi moja na Kulola aisee, Huyu, Mitimingi na Toni Kapola hawana tofauti
Pr Mbaga wa Adventista ni far better kuliko huyu
Haya ni maoni Yangu
Kwa hiyo sasa muhimbili haina wagonjwa tena?Mwampo sio tapeli watu wanapona wenye matatizo wwngi wamefunguliwa
Nashukuru mkuu🙏Pastor Carlos Kirimbai wa Tanzania, yuko hapo Dar, miaka mingi ya nyuma alikuwa akifanya kazi ya ukalimani katika mikutano ya Injili iliyokuwa inawaleta wahubiri mbali mbali wa kimaitafa hapa Tanzania mfano akina Bhonke. Kwa sasa muda mwingi anakuwa anafundisha na kuhubiri hapo Dar akitumia madarasa ya shule ya sekondari ya Kisutu, mjini kati na akishare free mafundisho yake kupitia mitandao ya kijamii ikiwemo whatsapp. Ni jamaa fulani hivi hana makuu lakini anapeo fresh wa bible na jamii.
Mkuu, nilieleza kuwa hao niliowaweka ni ambao kwa namna Moja ama nyingine nimebarikiwa na huduma zao.Huyu TAPELI nae yumo hivi huwa mmefungwa macho? Aljeeriza wameonyesha utapele wa huyu na nia ya kuhubiri bado umemuweka meza moja na Kulola
✅🙏Mwamba huyu mchambuzi wa Bible na misimamo mikali
Unaitwa FULL GOSPAL
. Z.Kakobe
KUNA KAUKOMAVU FULANI NA KAUTUBUZIMA NIMEKAONA NILIPOKUWA NASOMA LINE TO LINE YA HAYO ULIYOANDOKA.WEWE SIYO WALE WA SURIALI NI DHAMBI AU SIYO DHAMBI .GRAND MALT NI DHAMBI AU SIYO DHAMBI.Wa Kimataifa/ toka Mataifa mengine ni hawa:
1. Kenneth Hagin
2. Kenneth Copeland
3. Smith Wigglesworth
4. Dr. David Oyedepo
5. Pastor Chris Oyakilome
6. Uebert Angel
7. T. L. Osborn
8. Gloria Copeland
9. F. F. Bosworth
10. Charles Capps
11. Norvel Hayes
12. Andrew Wommack
13. E. W. Kenyon
14. Jerry Savelle
Kwa Tanzania, ni hawa wafuatao:
1. Aaron B. C. Mabondo
Kwa sasa ni marehemu. Alikuwa katibu Mkuu wa Kanisa la Pentekoste Tanzania. Nilimfahamu kwa mara ya kwanza mwaka 2003, mwezi June, nilipohudhuria Camp iliyoandaliwa na NEW LIFE BAND ya jijini Arusha na kufanyikia katika shule ya Sekondari Moshi mkoani Kilimanjaro.
Nilibarikiwa na masomo yake ya Imani na jinsi alivyokuwa akiishi Imani yake. Baada ya kuaga dunia, nilifanikiwa kukisoma kitabu cha Historia ya maisha yake. Nimevutiwa na misimamo yake ya kiimani, kiasi cha kutokukubali kuwekewa mipaka ya kidhehebu.
Inasemekana, kupitia mafundisho yake, alichochea "uamsho" kwenye Makanisa yasiyokuwa ya Kipentekoste, kama Moravian, Anglikana, n.k. Huwa ninabarikiwa sana na wahubiri wanaolisambaza Neno la Mungu bila kuzingatia mipaka ya madhehebu yao. Msimamo wa Mabondo ulikuwa kwamba hakutumwa kuyahubiria madhehebu, bali kila kiumbe. Kwa hiyo alikuwa yupo tayari kuhubiri popote, bila kujali dhehebu litakalomwalika.
2. Dr. Mosses Kulola
Aliifanya huduma yake kwa uaminifu mkubwa sana. Hakuwa akitafuta maslahi yake binafsi. Alikuwa tayari kuhubiri hata katika mazingira magumu. Alikuwa ni mtu wa lengo moja tu maishani mwake, KUHUBIRI INJILI.
3. Mwl Christopher Mwakasege
Tokea aanze huduma, amekuwa "focused" kwenye hiyo huduma. Angeweza kufanya shughuli zingine za kiuchumi, hasa ukizingatia kuwa ni msomi wa Uchumi, lakini kwa kuwa ameukubali wito wa KULIFUNDISHA Neno la Mungu, ameamua kuachana na vingine vyote na kubaki na kimoja tu, huduma aliyoitiwa.
Kingine ninachompendea, ni tabia yake ya kutokuendekeza "udini". Timu ya huduma yake inadhihirisha hilo. Ina wahudumu kutoka madhehebu mablimbali yaliyopo Tanzania.
Kwa ufahamu wangu, yeye ni miongoni mwa wahubiri wachache walioweza kukivuka kiunzi cha udhehebu nchini Tanzania.
4. Mch. Elyona Kimaro
Japo sijamfuatilia sana, lakini kwa vipindi vyake vichache nilivyovitazama kupitia Upendo TV, amenibariki kwa kweli. Ni kiongozi mzuri. Kiongozi huona hitaji na kutafuta kulitimiza kabla ya kuambiwa. Ndivyo alivyofanya Kimaro kwenye Kanisa analoliongoza, ametafuta jinsi ya kukata kiu ya kiroho ya watu wake.
5. Dr. Augustine Mpemba
Ni Mtanzania anayeishi Marekani. Alikuwa Askofu wa Kanisa la TFE Jijini Mwanza, lakini sijui kama angali kiongozi wa hilo Kanisa kwa sasa. Nilishakisoma kitabu chake kimoja, na nilishasikiliza mtandaoni mafundisho yake kadhaa. Ana uelewa mpana wa mambo ya kiroho na kijamii. Madhalani, yupo vizuri sana kwenye masomo ya IMANI, masomo ambayo ni adimu sana katika Makanisa mengi ya Tanzania.
6. Prosper Ntepa
Sijawahi kusikiliza mahubiri yake, lakini nimevisoma vitabu kadhaa alivyoviandika. Kuna kimoja kinachohusiana na uponyaji, nilikipenda sana. Ni Mwalimu mzuri sana kwenye somo la Imani. Na kama ilivyo kwa tabia ya walimu wengi, yeye naye ni msomaji mzuri sana wa Vitabu.
7. Pastor Famous
Huyu ni Mchungaji wa Winners Chapel Jijini Mwanza. Nafikiri ni Mnigeria, alikuwa akiliongoza Kanisa la Winners Chapel lililopo Pasiansi jijini Mwanza. Sijui kama bado yupo pale au la.
8. Dr. Barnaba Mtokambali
Ni Askofu Mkuu wa TAG na pia ni Rais wa Makanisa ya Assemblies barani Afrika. Kama hiyo haitoshi, ni Mwenyekiti wa Makanisa ya Kipentekoste Tanzania.
Ana maono ya kiuongozi. Si bure CPCT wamempa Uenyekiti.
NB. Naweza nisiwe nakubaliana na kila kitu kwa baadhi ya hao watumishi wa Mungu, lakini kwa kuamua kuwataja kama miongoni mwa wahubiri wangu wa mfano, ni kwa sababu kuna maeneo wamenibariki.
Na, katika wahubiri woote, "my favourite" ni KENNETH HAGIN. Japo alishaaga dunia tokea mwaka 2003, vitabu vyake vimenisaidia sana , hasa katika eneo la IMANI.
Hatujawahi kukutana ana kwa ana, lakini kupitia vitabu vyake, amekuwa kama baba kwangu. Nimeshavisoma zaidi ya vitabu vyake hamsini. Nimeshavisoma karibia vitabu vyote alivyoviandika. Ni vichache sana ndiyo bado.
Tuwekee na wewe watumishi au viongozi wa dini unaowachukulia kama watumishi wa Mungu au viongozi wa mfano kwako.
Karibu!!!
PAST Elingarami Munishi,namuona yuko objective sana.Wa Kimataifa/ toka Mataifa mengine ni hawa:

Karibu mkuu, lakini mimi si Mchungaji wala kiongozi wa dini. Lakini ukipenda kunitafuta sitakuzuia.KUNA KAUKOMAVU FULANI NA KAUTUBUZIMA NIMEKAONA NILIPOKUWA NASOMA LINE TO LINE YA HAYO ULIYOANDOKA.WEWE SIYO WALE WA SURIALI NI DHAMBI AU SIYO DHAMBI .GRAND MALT NI DHAMBI AU SIYO DHAMBI.
NATAMANI TUNGEKUTANA ANA KWA ANA,NINGETOKA KATIKA MKWAMO.
BE BLESSED.
Pastor Chris oyakilome aliwahi kusema
"kufanya masterbation sio dhambi"
Hii ilinitisha kidogo maana nilikua mfuasi wake mzuri.
Hapana mkuu, hiyo ni dhambi kama dhambi zingine.Ndio sio dhambi,ni kitendo kitakatifu cha kupunguza upwiru na kuacha zinaa.
Ni dhambi kwenu , dhambi ni mtazamo wa mtu tu.Hapana mkuu, hiyo ni dhambi kama dhambi zingine.
Hao wote hapo juu sina shaka nao,hasa pastor Chris oyakhilomeMkuu, nilieleza kuwa hao niliowaweka ni ambao kwa namna Moja ama nyingine nimebarikiwa na huduma zao.
Nilivisoma vitabu kadhaa vya Uebert Angel, japo kuna baadhi ya mambo ambayo mwanzoni vilinitia mashaka kuhusu huduma yake, niliamua kupuuzia baada ya kubaini kuwa mentor wake ni Pastor Chris.
Pastor Chris naye nilikuwa nina mashaka naye, lakini mashaka yaliisha nilipogundua kuwa rafiki yake wa karibu ni Benny Hinn.
Hata Benny Hinn, nilikuja kumkubali vilivyo baada ya kugundua ukaribu alikokuwa nao na Reinhard Bonnke.
Unauona mnyororo ulivyo? Bonnke, Benny Hinn, Pastor Chris, Uebert Angel.
Lakini sivyo tu, huwa nina "falsafa" yangu kwa habari ya watumishi. Kwamba, katika mafundisho yao, nitatofautisha chuya na wali. Nikikutana na chuya, nitatema lakini wali nitaumeza.
"Sibugii" kila kitu kisemwacho na mtumishi. Nikijiridhisha kuwa akisemacho kipo nje ya Biblia, nakiweka kando nasubiria kingine.