KERO Wahudumu mabasi ya Mwendokasi wanatoza nauli zaidi ya iliyopangwa kwa kisingizio cha kukosa chenji

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Mimi nina kero moja hawa wahudumu wa mabasi ya mwendokasi wanatoza nauli zaidi tofauti na utaratibu wa nauli zilizowekwa kwa kisinginzio cha kukosa chenji.

Kwa mfano nauli ya kutoka Mbezi kwenda Gerezani ni Tsh 1,250 ukitoa noti ya 2,000 unarundishiwa 500 wakisema chenji hamna.

mwendokasi.jpg
 
Sehemu yoyote inayotoa huduma kwa jamii kama kuna vichenji vya coin vinabaki mara chache kurudishiwa kwa kisingizio cha kukosa chenji
 
Mimi nina kero moja hawa wahudumu wa mabasi ya mwendokasi wanatoza nauli zaidi tofauti na utaratibu wa nauli zilizowekwa kwa kisinginzio cha kukosa chenji.

Kwa mfano nauli ya kutoka Mbezi kwenda Gerezani ni Tsh 1,250 ukitoa noti ya 2,000 unarundishiwa 500 wakisema chenji hamna.

Hawo ni wahuni tu kama wahuni wengine. Washughulikiwe kwa mujibu wa taratibu na sheria za nchi.
 
Hili suala linakera mno, tena ubaya we abiria akiwa na upungufu hata wa 50 hakubaliwi na haijalishi hali yake wala umri wake. Huu ni ufedhuli.
Na hizi chenji ambazo hazirudishwi kwa abiria, je! wapi zinaenda au ndio jioni watu wanajilipa posho?
 
Mimi nilidai chenji yang nikapewa. Mdai chenji zenu, kulea hii tabia tunabariki udokozi
 
Yan leo mara ya 3 ndan ya mwezi huu naenda mbezi pale. Naona wanaweka chenji za 500 tu mezan, za mia 2 wanazificha mpaka udai. Usipodai hawakwambii na ukidai mara nyinginr unaambiwa hamna chenji.
 
Mimi nina kero moja hawa wahudumu wa mabasi ya mwendokasi wanatoza nauli zaidi tofauti na utaratibu wa nauli zilizowekwa kwa kisinginzio cha kukosa chenji.

Kwa mfano nauli ya kutoka Mbezi kwenda Gerezani ni Tsh 1,250 ukitoa noti ya 2,000 unarundishiwa 500 wakisema chenji hamna.

Karibu kituo Chao Cha Muhimbili Kila siku Kila saa hawana chenji ya 250 tetesi Kila siku wahudumu hutoka na mafao haramu ya 30000.😡
 
Back
Top Bottom