Wahudumu ndani ya ndege Kenya Airways ni homa ya uchaguzi au mmenyimwa mishahara yenu? Mmenitisha

API Gravity

JF-Expert Member
Joined
Mar 15, 2016
Posts
658
Reaction score
765
Habari wakuu,

Mwishoni mwa wiki jana nimesafili kutoka Guangzhou hadi Nairobi kwa ndege ya shirika la China Southern Airways na kumalizia safari yangu Dar es salaam kwa Kenya Airways. Ndani China Southern wahudumu walikuwa wenye bashasha, furaha na tabasamu la hali ya juu mda wote wanapopitapita au hata pale wanapokusemesha, ukimwangalia tu anatabasamu. Kipindi nilikohoa kidogo mmoja alikuwa karibu akanipa pole na kuniuliza kama nahitaji msaada.

Sasa kivumbi ndani ya KQ, wahudumu wamenuna sijapata kuona kwenye maisha yangu ya usafiri wa anga, mhudumu anaandaa abiria kwa ajili ya ndege kuruka kakunja sura halafu anatowa maelekezo kwa ishara kama bubu vile. Ilifika mahali nikajikoholesha makusudi na mhudumu akiwa karibu yangu ili nione response kulinganisha na ndege ya wachina, cha ajabu mhudumu hata hakugeuka kuniangalia.

Lingine nililoliona ni wahudumu kuanza kuzurura ndani ya ndege mda kidogo tu baada ya kuruka na pia karibia kabisa na mda wa ndege kutua. Sasa hili sijui kiusalama liko vipi, nikilinganisha na China Southern niliotoka nao huko uchororoni mwa China hadi Guangzhou na Guangzhou Nairobi mambo hayakuwa namna hiyo.

Wito kwa wahudumu wa KQ, hebu badilikeni jamani huduma nzuri kwa abiria wenu ni mhimu kwa ustawi wa shirika lenu. Na nyie KQ wenyewe walipeni vizuri basi hawa watu wawe na furaha, haiwezekeni mhudumu tena wa kike ndani ya ndege kukunja sura kama Tyson anaingia ulingoni.

Ni hayo tu kwa leo.
 
ila wenzetu wanajua biashara sana, yani ukikohoa au kujikuna kama yupo karibu huyo keshafika, kwa ndege zetu sijaona hata shirika 1 likifanya hivyo wakishamaliza kutoa tahadhari huwasikii tena labda wapitishe vinywaji,
 
Habari wakuu
Mwishoni mwa wiki jana nimesafili kutoka Guangzhou hadi Nairobi kwa ndege ya shirika la China Southern Airways na kumalizia safari yangu Dar es salaam kwa Kenya Airways.
Ndani China Southern wahudumu walikuwa wenye bashasha, furaha na tabasamu la hali ya juu mda wote wanapopitapita au hata pale wanapokusemesha, ukimwangalia tu anatabasamu. Kipindi nilikohoa kidogo mmoja alikuwa karibu akanipa pole na kuniuliza kama nahitaji msaada.

Sasa kivumbi ndani ya KQ, wahudumu wamenuna sijapata kuona kwenye maisha yangu ya usafiri wa anga, mhudumu anaandaa abiria kwa ajili ya ndege kuruka kakunja sura halafu anatowa maelekezo kwa ishara kama bubu vile. Ilifika mahali nikajikoholesha makusudi na mhudumu akiwa karibu yangu ili nione response kulinganisha na ndege ya wachina, cha ajabu mhudumu hata hakugeuka kuniangalia.

Lingine nililoliona ni wahudumu kuanza kuzurura ndani ya ndege mda kidogo tu baada ya kuruka na pia karibia kabisa na mda wa ndege kutua. Sasa hili sijui kiusalama liko vipi, nikilinganisha na China Southern niliotoka nao huko uchororoni mwa China hadi Guangzhou na Guangzhou Nairobi mambo hayakuwa namna hiyo.

Wito kwa wahudumu wa KQ, hebu badilikeni jamani huduma nzuri kwa abiria wenu ni mhimu kwa ustawi wa shirika lenu. Na nyie KQ wenyewe walipeni vizuri basi hawa watu wawe na furaha, haiwezekeni mhudumu tena wa kike ndani ya ndege kukunja sura kama Tyson anaingia ulingoni.

Ni hayo tu kwa leo.
alikudharau kwasababu ya tabia mbovu ya rais wako. Sizonje ni janga he should grow up
 
Ukute hawajalipwa pia wanalipwa hela ndogo sana wale watu
Zaidi wanafaidi kuruka kila siku na kulala hotel nzuri
Kubeba simu na hela mliziacha
 
Habari wakuu
Mwishoni mwa wiki jana nimesafili kutoka Guangzhou hadi Nairobi kwa ndege ya shirika la China Southern Airways na kumalizia safari yangu Dar es salaam kwa Kenya Airways.
Ndani China Southern wahudumu walikuwa wenye bashasha, furaha na tabasamu la hali ya juu mda wote wanapopitapita au hata pale wanapokusemesha, ukimwangalia tu anatabasamu. Kipindi nilikohoa kidogo mmoja alikuwa karibu akanipa pole na kuniuliza kama nahitaji msaada.

Sasa kivumbi ndani ya KQ, wahudumu wamenuna sijapata kuona kwenye maisha yangu ya usafiri wa anga, mhudumu anaandaa abiria kwa ajili ya ndege kuruka kakunja sura halafu anatowa maelekezo kwa ishara kama bubu vile. Ilifika mahali nikajikoholesha makusudi na mhudumu akiwa karibu yangu ili nione response kulinganisha na ndege ya wachina, cha ajabu mhudumu hata hakugeuka kuniangalia.

Lingine nililoliona ni wahudumu kuanza kuzurura ndani ya ndege mda kidogo tu baada ya kuruka na pia karibia kabisa na mda wa ndege kutua. Sasa hili sijui kiusalama liko vipi, nikilinganisha na China Southern niliotoka nao huko uchororoni mwa China hadi Guangzhou na Guangzhou Nairobi mambo hayakuwa namna hiyo.

Wito kwa wahudumu wa KQ, hebu badilikeni jamani huduma nzuri kwa abiria wenu ni mhimu kwa ustawi wa shirika lenu. Na nyie KQ wenyewe walipeni vizuri basi hawa watu wawe na furaha, haiwezekeni mhudumu tena wa kike ndani ya ndege kukunja sura kama Tyson anaingia ulingoni.

Ni hayo tu kwa leo.
Duh!hongera yako mwayebo umepanda ndege kipindi hiki wenzio mpaka tukafanyiwe upasuaji India tena kwa michango ya watanzania

Sent from my SM-J700H using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom