Wahusika mko wapi hadi hali imekuwa hivi hapa Mbezi?

Wahusika mko wapi hadi hali imekuwa hivi hapa Mbezi?

Waenda kwa miguu tumekuwa wakimbizi watu hawana pa kupita, eneo LA wazi lipo LA kutosha ila njia za waenda kwa miguu na mitaro imezibwa!! Hujuma ya Dotto James
Mimi jana nilishangaa kuona njia wameziba na barabarani kuna watu wamepanga biashara.
 
Duh! Hakuna bango la kukataza hilo eneo la karibu? Serikali ya mtaa?
Njia ya kwenda goba muuza chips kuweka kiko chini ya Tangazo la kukataza kabisaaaaa!
Tatizo la mbezi ni serikali ya mtaa wa mshikamano.
RC hawezi kuwepo kila sehemu
 
Hali inazidi kuwa mbaya kila siku.
 
Kweli nchi hii haitawaliki, pamoja na kelele zote za serikali ya CCM kuwa kuna njama toka kundi fulani kuwa nchi isitawalike kwa kufumbia macho wanaoshindwa kuheshimu sheria na sheria ndogo, hili la Mbezi Jijini Dar es Salaam ni ishara serikali imeshindwa kuongoza.
Hii ni uasi. Kuasi dira na maagizo ya Mhe. Rais. Usipofanikiwa ama ukugongwa unasema kwasababu ya maisha.

Na wengine serikali imewapa mikopo hapo ili wakaasi maagizo yake vizuri. Kweli haipendezi. Usipo mheshimu Kiongoz Mkuu. Usitegemee upate heri na mafanikio. Trust me. Yeye amebeba moyo wa Taifa.
 
Watumishi wa manispaa ubungo ndiyo wengi zarau serikali ya awamu ya 6,ndiyo chanzo machinga kurudi mbezi.
 
Kweli nchi hii haitawaliki, pamoja na kelele zote za serikali ya CCM kuwa kuna njama toka kundi fulani kuwa nchi isitawalike kwa kufumbia macho wanaoshindwa kuheshimu sheria na sheria ndogo, hili la Mbezi Jijini Dar es Salaam ni ishara serikali imeshindwa kuongoza.

Mbezi sio jijini dar es salaam, Mbezi ipo manispaa ya ubungo
 
Back
Top Bottom