Salaam wadau na wapendq maendeleo.
Wahusika wafuatao wawajibike au kushtakiwa kwa kuhujumu ujenzi wa barabara ya kutoka bunju b kwenda mabwepande kwa aina ya ujenzi huu. Hawa ni; mkandarasi, mjenzi, mshauri, mkurugenzi wa manispaa, meya,diwani, mbunge na waziri wa ujenzi.
Barabara haina mtaro hata mmoja na wanaikwangua bila kuongeza kifusi chochote.
Wananchi wanaopita barabara hiyo iliyojaa vumbi ni wagonjwa wa tb watarajiwa.
Takukuru hebu mulikeni huu mradi unaotia aibu dar yote.
Mgeni mimi nashangaa kwani hata huko nitokako ujenzi wa barabara ni wa kiwango kizuri tu kulinganisha na huku kwenu mabwepande.
Hebu waokoeni basi watoto wadogo ambao wanaathirika na vumbi hilo la masaa 24/7 angalau kwa kumwagia maji!
Songoro unafeli sana siku hizi.
Hakuna cha mtaro wala mfereji kwenye barabara ya mabwepande na mvua zikinyesha maji yanatuama katikati ya barabara na kutengeza mahandaki na mabwawa.Barabara za vumbi mara nyingi huchongwa ili ziwe zinamwaga maji pembeni (camber) kisha maji hayo hutililika kuelekea kwenye mifereji ambayo huyaondoa ili yasituame barabarani na kuyafanya yaharibu barabara (mitre drains) kutegemana na ukubwa wa bajeti kwingine kwenye maji mengi hulazimika kuweka mitaro ya zege/mawe hasa sehemu zenye miinuko na mitelemko. Sasa, ingawa sio msemaji ila kwa maoni yangu ndio hivyo pengine kuna mradi mkubwa wa kuijenga nilisikia kutokea Mbezi/Makabe.
Hawajaongeza chochote zaidi ya kuikwangua na kupitisha kishindilio chao kwa dk. 40 tu na kusepa.Hiyo barabara ilikua mbaya asee....
Wanajenga kwa kiwango cha lami? Au wanakwangua tu na kuweka changarawe?
Hakuna cha mtaro wala mfereji kwenye barabara ya mabwepande na mvua zikinyesha maji yanatuama katikati ya barabara na kutengeza mahandaki na mabwawa.
Ndio maana nimeiamsha takukuru ifanye ziara kwenye barabara hii na kuchukua hatua kwa wahusika wote kwani engineer mhusika anaichafua fani ya ujenzi na kuifanya ibagazwe!
Meya Songoro naufahamu utendaji wako, hebu shughulikia kero hii haraka kwani inakuchafua.Sasa
Hakuna cha mtaro wala mfereji kwenye barabara ya mabwepande na mvua zikinyesha maji yanatuama katikati ya barabara na kutengeza mahandaki na mabwawa.
Ndio maana nimeiamsha takukuru ifanye ziara kwenye barabara hii na kuchukua hatua kwa wahusika wote kwani engineer mhusika anaichafua fani ya ujenzi na kuifanya ibagazwe!
Meya Songoro naufahamu utendaji wako, hebu shughulikia kero hii haraka kwani inakuchafua.
Barabara ni ya vumbi. Huwezi kuja kukwangua vumbi bila kuongeza kifusi juu. Ile barabara ina mashimo balaa. Kilichohitajika ni kumwaga kifusi then kusambaza na kushindilia. Wao wamekwangua barabara ina maana wanaichimba zaidi kuelekea chini.Sasa hapo shida kwa msimamizi/mkaguzi na mkandarasi kwanini maji yatuame katikati ya barabara? Lakini yawezekana pia kama nilivyosema awali maeneo mengine ni korofi pengine huhitaji matengenezo ya kipekee kama vile uwekaji wa culvets, ditch, rigged pavements nk. Sasa kulingana na ufinyu wa bajeti pengine ni marekebisho ya muda tu kwa maoni yangu tu lakini.
Hiyo barabara bado ina vumbi? mbona enzi za Magufuli ilikuwa ishatengewa fedha kwa ujenzi wa lami ,hiyo na ile ya kibaha kwenda baobab? Kama zote hizo bado zina vumbi ni hatari.Salaam wadau na wapendamaendeleo.
Wahusika wafuatao wawajibike au kushtakiwa kwa kuhujumu ujenzi wa barabara ya kutoka Bunju B kwenda Mabwepande kwa aina ya ujenzi huu.
Hawa ni; mkandarasi, mjenzi, mshauri, mkurugenzi wa manispaa, meya,diwani, mbunge na waziri wa ujenzi.
Barabara haina mtaro hata mmoja na wanaikwangua bila kuongeza kifusi chochote.
Wananchi wanaopita barabara hiyo iliyojaa vumbi ni wagonjwa wa tb watarajiwa.
Takukuru hebu mulikeni huu mradi unaotia aibu Dar yote.
Mgeni mimi nashangaa kwani hata huko nitokako ujenzi wa barabara ni wa kiwango kizuri tu kulinganisha na huku kwenu mabwepande.
Hebu waokoeni basi watoto wadogo ambao wanaathirika na vumbi hilo la masaa 24/7 angalau kwa kumwagia maji.
Songoro unafeli sana siku hizi.
Ndicho walichofanya. Catapiller moja na kishindilio kimoja bila kumwaga kifusi wala maji. Na wameenda juu mara mbili tena kwa speed na hawakukaa zaidi ya dk.40.Barabara ni ya vumbi. Huwezi kuja kukwangua vumbi bila kuongeza kifusi juu. Ile barabara ina mashimo balaa. Kilichohitajika ni kumwaga kifusi then kusambaza na kushindilia. Wao wamekwangua barabara ina maana wanaichimba zaidi kuelekea chini.
Hii ni kwa mjibu wa mtoa mada.
Vumbi la hatari kwa maisha ya viumbehai.Hiyo barabara bado ina vumbi? mbona enzi za Magufuli ilikuwa ishatengewa fedha kwa ujenzi wa lami ,hiyo na ile ya kibaha kwenda baobab? Kama zote hizo bado zina vumbi ni hatari.
Sina uhakika labda tumwalike bi Hanifa mkurugenzi wa manispaa atupe jibu.Vipi kuna mpango wowote wa kuunganisha Kwa lami kutoka bunju B Hadi mpiji majohe
Alafu haipo kwenye mpango wa serikali Kwa mwaka huu kwenye budget 2026-27.Inashangaza sana, barabara muhimu kama ya Mbezi luis to Bunju B via (mpiji magohe & mwabwepande) mpaka leo bado imeachwa vile vile, ni 25kilometers tuu, kumbuka kama hii barabara ingekua ishakamilika pasingekua na ulazima wa Gari za mikoa ya kaskazini zinazotokea stand ya magufuli kupita hii njia ya Goba,.zinazunguka sana