Salaam wadau na wapendamaendeleo.
Wahusika wafuatao wawajibike au kushtakiwa kwa kuhujumu ujenzi wa barabara ya kutoka Bunju B kwenda Mabwepande kwa aina ya ujenzi huu.
Hawa ni; mkandarasi, mjenzi, mshauri, mkurugenzi wa manispaa, meya,diwani, mbunge na waziri wa ujenzi.
Barabara haina mtaro hata mmoja na wanaikwangua bila kuongeza kifusi chochote.
Wananchi wanaopita barabara hiyo iliyojaa vumbi ni wagonjwa wa tb watarajiwa.
Takukuru hebu mulikeni huu mradi unaotia aibu Dar yote.
Mgeni mimi nashangaa kwani hata huko nitokako ujenzi wa barabara ni wa kiwango kizuri tu kulinganisha na huku kwenu mabwepande.
Hebu waokoeni basi watoto wadogo ambao wanaathirika na vumbi hilo la masaa 24/7 angalau kwa kumwagia maji.
Songoro unafeli sana siku hizi.