Mimi yalikwishanikuta kama hayo na kilichotokea mpaka leo sitokuja kusahau kwani nilikuja gundua nae anatoka nje tena na rafiki yangu ambaye tulikuwa tunaaminiana sana,siku niliyowakuta live aliniambia kuwa nae anafanya kama nilivyofanya mimi hivyo nimsamehe kama yeye alivyonisamehe na tuendelee kuishi kama kawaida.
Ushauri:Chunga sana mienendo yake na jaribu kutulia maana si rahisi mtu kuchukuliwa chake na akasamehe kirahisi namna hiyo hasa kwa wanawake,mwoneshe unajutia kufanya vile na usijenge mazingira ya kumficha jambo kwake,kuwa wazi muda wote hata kwa jambo dogo na mwisho atakuamini na kusamehe kwa kujua sasa umebadilika na kuwa mtu safi kwake.