EINSTEIN112
JF-Expert Member
- Oct 26, 2018
- 21,711
- 35,644
Waingereza wawili na mwanamume mmoja wa Morocco waliokamatwa na vikosi vya Urusi nchini Ukraine wamehukumiwa kifo, shirika la habari linalomilikiwa na Urusi RIA Novosti linaripoti.
Aiden Aslin, 28, kutoka Nottinghamshire, Shaun Pinner, 48, kutoka Bedfordshire, na mtu wa tatu, raia wa Morocco Saaudun Brahim, walifikishwa katika mahakama ya Jamhuri ya Watu wa Donetsk, ambayo inashikiliwa na waasi wanaoiunga mkono Urusi.
Mahakama hiyo haitambuliki kimataifa.
Wanaripotiwa kushtakiwa kwa kuwa mamluki.
Lakini familia za wanaume wa Uingereza wanasema walikuwa katika jeshi la Ukraine.
Wanaume wote wa Uingereza wanahudumia wanajeshi wa Ukraine na Uingereza imeweka wazi kuwa ni wafungwa wa vita wanaostahili kinga na hawapaswi kufunguliwa mashtaka kwa kushiriki katika mapigano.
Telegram RIA News ilisema: ‘’Mahakama Kuu ya DPR ilitoa hukumu ya kwanza kwa mamluki- Mwingereza Aiden Aslin na Sean Pinner na Mmorocco Saadun Brahim walihukumiwa kifo, mwandishi wa RIA Novosti anaripoti kutoka chumba cha mahakama.’’