Mister mimi
Member
- Apr 29, 2018
- 89
- 106
Ndio, maana kimaana ya kugha ya kiswahili 'kafiri' ni mtu asiyeamini.
Na hii ipo hasa kwenye hizi dini kubwa mbili duniani.
Eti we muislam,mtu ambaye hakuzuii kujifuza dini yako,hakuzuii kufanya ibada,pengine mtu huyo ni mfanyakazi wako/boss wako/mama/baba yako n.k. je ukafiri wake ni upi ikiwa na yeye anaamini uwepo wa Mungu?
Hivyo hivyo kwa wakristo,mtu asiyeamini ukristo kimaana ya neno kafiri na kiimani ya kikristo kwa mujibu wa maandiko mtu huyo kwa wakristo ni kafiri.wakristo hawawaiti waislam makafiri niwapongeze katika hili japo nao wanamajina mengine yakuudhi wanayowaita waislam,(sio mada yangu leo).
"KAFIRI" ni neno baya,ni tusi kubwa kiimani.
ndio maana hata katika vitabu vya dini si kila mtu asiyeamini aliitwa kafiri.Walioitwa makafiri ni wale tu waliokuwa wakipinga uwepo na uwezo wa Mungu kwa maneno na matendo.mfano farao Firauni wa misri ya zamani,yule ndio mfano wa kafiri.
Kwahiyo kumuita mtu kafiri,na mtu huyo anamuamini Mungu kisa tu mmetofautiana njia za kuamini, kisa tu Mungu huyo wewe umeamua kumuita kwa jina la lugha ya kiarabu,kisa tu Mungu huyo wao wamefundishwa jina lake kwa lugha ya kitaliano,sio sawa.sote Mungu wetu ni mmoja.
Dini zote zinahubiri upendo amani haki na uadilifu.
Mtume muhamad yeye aling'olewa hadi meno, lakini hakwaita waliomg'oa meno kuwa ni makafiri,lakini aliwaombea msamaha na akasema hakuja kulaani watu bali kuwaombea mema huenda kesho wakawa wema.
Sasa wewe hiyo chuki umeitoa wapi,kiasi cha kuwaita watu wasiompinga Mungu ni makafiri?
We muislam acha kuita watu makafiri,sio neno zuri kiimani,maana hata mama na baba wa mtume muhamad hawakuwa waislam,je walikuwa ni makafiri?
Tupendane na tuvumiliane katika imani zetu! Wote sisi Mungu wetu ni mmoja,
Sisemi kwamba makafiri hawapo,la wapo,tena wapo,ila sio kina kiranga,maana kuna tofauti kati ya kutokuamini na kupinga/kuzuia watu kuamini.
leo kuna vyama vingi vya wazi na vya siri vinavyozuia imani za watu kumuamini Mungu,.tena vinampinga Mungu kwa akili kubwa ila utavijua kwa kuwa vyenyewe vina promot sana yale yote ambayo Mungu amekataza.na humo wanajiunga watu watu wa dini zote.
Kwa hiyo unaweza kukuta kuna mashehe ni makafiri,kuna wachungaji ni makafiri,watu maarufu ndo hutumika sana na hivyo vyama(hili ni dodoso mada yake ni ndefu kidogo).
Si vema kumuita mtu kafiri,tukumbushane kutenda mema,tukatazane mabaya,yanayozuilika tuyazuie,ila kuhukumu imani ya mtu tumuachie Mungu mwenyewe.
Ramadhan na Kwaresma njema kwa wote.
Fungeni muwe wanyenyekevu,mchome mafuta ya kwenye matumbo, mpunguze sumu mboreshe afya,na mkumbuke kuwa kuna watu huwa wanahitaji misaada!