Waislam Pemba Waandamana Kanisa Lisijengwe Pemba

Waislam Pemba Waandamana Kanisa Lisijengwe Pemba

Hawa watu wamejiuliza Wakristo wakianza kupinga misikiti kujengwa maeneo yao mambo yatafikia wapi? Haya ni matokeo ya uongozi unaoonwa kuwa bora wa Raisi Samia nchini. Kuna mambo umeyaendekeza hadi kuleta vitu kama hivi.

Kwa kuwa hili ni suala la kitaifa linalotishia sana amani, nasubiri kuona Raisi Samia atasema nini au kuchukua hatua gani - huenda akaona Zanzibar haimhusu!
 
Mbona Pemba kuna makanisa mengi sana, Anglican na Catholic? Au hii ilikua nini
 
😂😂😂Wavaa kobazi akili zenu bn sasa wimbo wa taifa kuwa na neno mungu ndo inaifanya nchi kuwa ya kidini!? Unashndwa kutofautisha dini na mungu!? Au kwenye wimbo wa taifa umeskia kuna sehemu wamemtaja alah au jehova!? Muwage mnajifunza kuficha ujinga....

tofauti kati ya dini na Mungu ni ipi? kipi kinaweza kuwepo bila ya kingine? au inawezekana unachanganya kati ya Mungu na miungu labda ? …
 
Dini za kikristo na waislamu zenyewe kama dini hazina shida ila zinazalisha watu wa hovyo sana. Yaani unakuta mtu huyo huyo anaenda kutangaza dini yake sehemu ambayo haijafika na akifanikiwa kupata waumini na kuqnzisha nyumba ya ibada huko anashangilia mafanikio.

Mtu huyo huyo akiona mtu wa dini nyingine anatangaza dini asiyoiamini yeye anafura kama koboko. Na wajinga wengine ndio hao wa kuandamana. Sasa dini haikuhusu unaandamana ili iweje. Waache waje wajenge halafu washawishi wajiunge na dini yako waiache hiyo ambayo unaona sio sawa. Sasa hao unaoona wamepotea utawafikia lini iwapo wanajileta wenyewe kwako unaandamana🤣🤣🤣🤣🤣🤣.
 
kujenga Kanisa au Msikiti mahali maana yake ni kueneza Ukristo au uislamu ktk hilo eneo kwa gharama ya Wakristo au Waislamu wa hilo eneo, haijawahi kuwa tofauti na hivyo kihistoria tangia uwepo wa dini, mimi kama ninaishi kwenye kata au tarafa ambayo >98% ya wakazi ni Christians na wanapractice Christian way of life ujenzi wa Msikiti kwenye hiyo tarafa au kata yangu nitaona kama tishio la Ukristo moja kwa moja na nina haki ya kupinga …
Wewe naye ni mpuuzi sana... Makanisa na Misikiti vinajengwa hili waumini wao wapate sehemu za kuabudia

Kwa karne hii yenye muingiliano wa watu, lazima makanisa au Misikiti ijengwe kila mahali... Dini haiwezi kuwa tishio kupitia kujengwa kwa majumba ya kuabudia, kwa sababu hakuna anayeshikiwa panga kwenda kuabudu humo.... kila mtu akihesmu imani ya mwenzake hakuna shida... Ukija bara Waislamu wamejenga Misikiti maeneo ambayo awali yalikuwa ya Wakristo, na uwezi kukuta mkristo anaumia kuhusu hilo... labda wewe uwe mkristo ubwabwa, sisi Ukristo unatufundisha upendo hata kwa yule hasiye ndugu yako au wa dini yako
 
Unamjengea nani hilo kanisa huko Pemba. Waumini wa kanisa ni zero labda huyo kasisi peke yake ?
Na kanisa la madhehebu gani ? kama haya ya kitapeli ndio hayatakiwi kabisaaa.
Waacheni wapemba
Nani kakwambia kuwa Zanzibar hakuna Wakristo... Wakoloni walijenga makanisa mengi tu Zanzibar kama Waaarabu walivyojenga misikiti huko... Zanzibar Wakristo ni wa kucheba sana na makanisa yapo japo ni ya kuhesabika, kuhusu utapeli hiyo ni mambo ya kimamlaka na kisheria, lakini nchi haizuii mkristo kusali hata kama kanisa lake limewahi kutapeli... Tanzania kila mtu ana uhuru wa kuabudu cha msingi hasivunje sheria
 
Uwezo wako wa kufikiri ni kama wa Samaki aina ya Kambale kukaa kwenye matope tu wakati samaki wengine wakiishi Kwenye maeneo yenye maji mengi

Nikirudi kwenye kukuadabisha kimoja, Tanzania sio Nchi ya kidini... ukifanya hivyo kusema eneo moja Dini fulani iseme ni eneo lao tu hapo ndipo tutachochea vita vya wenyewe kwa wenyewe, umesema Zanzibar kwa asilimia 98% ni Waislamu, ukisema Zanzibar yote iwe ni Waislamu tu hakuna shughuli yoyote ya Wakristo kufanyika maeneo hayo huoni kama hao 2% wanaweza kuanza kuleta fujo kwa sababu ya kuzulumiwa haki yao ya msingi... hapo ndipo waasi au makundi yanayopigania dini uanza kutengenezwa.... Wakristo wataanza kutengeneza makundi ya kutaka haki yao, na watakapokuwa na Wakristo wa mataifa ya nje.

Vilevile Waislamu wengi wako Tanzania Bara, na mikoani ambayo kimsingi ni maeneo ya Wakristo wengi, utafanya Waislamu wanaoishi maeneo ya Wakristo wachomewe misikiti yao au wafukuzwe katika maeneo hayo kwa sababu ni maeneo ya Wakristo. Na hapo napo Waislamu wataanza uasi wa kutaka haki yao.

Itafika mahali hata Barabara au mitaa hatakiwi kukatiza mtu wa Dini fulani, hiyo itaenda mpaka kwenye ajira, chakula na mambo mengine

Kabla ya kutoa maoni fikiria athari zitakazotokea, sio kutoa maoni tu bila kufikiria.... Ogopa sana vita vya kidini au kikabila, angalia kule India Wahindu wanavyouwa Waislamu na kuwafukuza kwenye maeneo yao, vita mpaka imepelekea Nchi ya Pakistan na India kuchukiana na kutaka kuleta vita ya 3 ya Dunia. Sudan walipigana vita kiasi kwamba mpaka Nchi ikagawanyika kwa sababu ya Udini, leo tuna Sudani kusini na Sudani Kaskazini.

Dini zenyewe zimeletwa na Meli alafu unataka kuzipigania kuliko kupigania umoja wa Taifa letu, Utaifa kwanza Udini badae, Nchi hii ni mali ya Watanzania wote, kila mtanzania anayo haki ya kuabudu popote cha msingi hasivunje sheria au kumdhihaki mwingine.
Wafuasi wa mudi.
 
Aisee! Kwani kuna ubaya gani hilo Kanisa likijengwa huko Pemba..
 
Back
Top Bottom