Waislam tunakuomba Rais Samia umshauri mkuu wa Wilaya ya Kisarawe, Petro Magoti aache kebehi dhidi ya Waislam

Waislam tunakuomba Rais Samia umshauri mkuu wa Wilaya ya Kisarawe, Petro Magoti aache kebehi dhidi ya Waislam

Mimi sio DC, TISS, Polisi, wala Mkazi wa kisarawe...nikuletee aushahidi kama nani kutoka wapi?

Wewe umeweka Ushahidi kuwa wale wote sio watoto na wamezidi miaka 18 ili wajitegemee?

Jibu kinagaubaga
Waislam tunawasomesha watoto wetu elimu ya dini wangali wadogo tu...mtoto wa miaka 3 anakwenda madrasa/markaz kusoma dini ili amjue mola wake na dini yake kwa ujumla.
 
Acha ujinga, dharura gani inawafanya watoto wakalale msikitini wasilale makwao??
Watoto wako pale kuhifadhi Quran. Maneno ya Mungu ili uyahifadhi huwa hayataki distractions za kidunia. Ndio maana hata nyinyi mna seminaries na vyuo vya biblia ambapo wachungaji,mapadri na masista huenda kukaa kulisoma neno la mungu wenu.
 
Utamwelewa DC ikiwa tu utaweka udini pembeni na kuangalia fact. Wale ni watoto wanastahili kusoma na kukaa kwenye mazingira mazuri . Labda kama utalaumu kwa yeye kwenda na wanahabari na macamera kwamba anedeal nalo kimyakimya of which pia inafanyika hivyo ili wengine waone na wajifunze na kujirekebisa. Ni suala la wahusika kuchukua hatua kutengeneza mazingira watoto warudi huko
Nani kakwambia mkuu wa wilaya anatunga sera za elimu nchini?
Kanukuu kifungu gani cha sheria katika agizo lake hilo?
Sera za elimu? Kwahiyo hiyo elimu ya dini nayo ipo kwenye sera?
 
Sifuri tupu...walimu tunajua...mtoto unamfundisha kuandika kutoka kushoto kwenda kulia...lakin kichwan amekaririshwa kuandika kutoka kulia kwenda kushoto...serikali ituongezee posho...tunateseka..yaan mpaka ajae kwenye mfumo mwalimu ushakunywa doz kazaa na masindano kibao
Mbona wayahudi na lugha yao ya Hebrew huandika kutoka kulia kwenda kushoto na hatukuoni ukiwabeza we kichwa maji?
 
Waislam tunawasomesha watoto wetu elimu ya dini wangali wadogo tu...mtoto wa miaka 3 anakwenda madrasa/markaz kusoma dini ili amjue mola wake na dini yake kwa ujumla.
Sio Waislam tu, Wakristo tunaanza kuwafundisha na kuwapeleka Sunday School hata wakiwa na mwaka mmoja

Hilo sio tatizo, lakini je wanapata malezi wa Wazazi? Wanapata elimu ya awali ya kutoka kwa mama na Baba? Wanapikiwa chakula kinachowastahili? Au ndio kujipikia na kutopata joto la wazazi
 
Utamwelewa DC ikiwa tu utaweka udini pembeni na kuangalia fact. Wale ni watoto wanastahili kusoma na kukaa kwenye mazingira mazuri . Labda kama utalaumu kwa yeye kwenda na wanahabari na macamera kwamba anedeal nalo kimyakimya of which pia inafanyika hivyo ili wengine waone na wajifunze na kujirekebisa. Ni suala la wahusika kuchukua hatua kutengeneza mazingira watoto warudi huko

Sera za elimu? Kwahiyo hiyo elimu ya dini nayo ipo kwenye sera?

Hujui kuwa kuna mkono wa serikali kwenye kila kitu?

Ukitaka kujua kuwa serikali ina miongozo yake hadi kwenye sita kwa sita mkeo akupeleke kwenye mamlaka kuwa unamuomba tigo ndo utajua kuwa hata hilo kumbe serikali ina sheria zake!
 
Sio Waislam tu, Wakristo tunaanza kuwafundisha na kuwapeleka Sunday School hata wakiwa na mwaka mmoja

Hilo sio tatizo, lakini je wanapata malezi wa Wazazi? Wanapata elimu ya awali ya kutoka kwa mama na Baba? Wanapikiwa chakula kinachowastahili? Au ndio kujipikia na kutopata joto la wazazi
Mnapoeapeleka watoto boarding schools huwa wanapata malezo yenu saa ngapi? Je huko boarding wanapata joto lenu?

Hapo wapo msikitini , ni safest place on earth. Msikitini hakuna masuala yoyote ya kipuuzi unayoyajua wewe. Wanalelewa katika tabia njema ya Uislam.
 
Hujui kuwa kuna mkono wa serikali kwenye kila kitu?

Ukitaka kujua kuwa serikali ina miongozo yake hadi kwenye sita kwa sita mkeo akupeleke kwenye mamlaka kuwa unamuomba tigo ndo utajua kuwa hata hilo kumbe serikali ina sheria zake!
Sawa sasa kama ndivyo shida iko wapi? Wanaangalia palipo na shida wanataka kurekebisa
 
Sheikh kamuonesha huyo DC kuwa wapo kwenye michakato ya ujenzi...kuna Cement,matofali,nondo mchanga na kila kitu...bado wanafatilia vibali waanze ujenzi huku watoto wakiendelea na masomo hapo msikitini kwa dharura. Elimu inaendelea na ujenzi unaendelea.
Eneo la ujenzi ndio hatari zaidi kwa hao watoto, unajengaje mahali huku umezungukwa na watoto wa darasa la nne??
 
Hapaa ndio inatudhibitishia kwamba Uislamu ni dini ya Kimasikini sanaa usiojali utu,check shule zote za kikristo kama utawai kukutana na jambo la aibu na ajabu kama hili na sio ajabu wanategeshea WAPATE UFADHILI KUTOKA UARABUNI.MAANA HAKUNA MWISLAMU MWENYE IWEZO WA KUTO SADAKA KWA AJILI YA MAENDELEO NI MALALAMIKO TUU NA KUTOA NYAMA YA KONDOO SIKU YA IDD YA KUCHINJAA
HATA HIVYO BADO NI MSAADA FLANI HIVI

Any way nisiseme sanaa tusubiri Hajaty wenu aseme awatetee

Sema mfumo haitoruhusu hicho kituu

POVU RUKSAA
Kwamba hizi taasisi zenu hazipati misaada kutoka USA, Vatican na Rome?
 
Mnapoeapeleka watoto boarding schools huwa wanapata malezo yenu saa ngapi? Je huko boarding wanapata joto lenu?

Hapo wapo msikitini , ni safest place on earth. Msikitini hakuna masuala yoyote ya kipuuzi unayoyajua wewe. Wanalelewa katika tabia njema ya Uislam.
Hakuna Mtu aliyesema Msikitini hakufai au kuna mambo ya kipuuzi...naona unaanza kujaa jazba badala ya kujibu kwa hoja.

Boarding hapelekwi mtoto wa miaka mitatu, na hao waliowapeleka wengi wanajutia.

Aidha, Mazingira hayo ya International School, Daycare n.k yapo bayana...yanajulikana na wanayapost kupitia Brochures n.k tofauti na Masjid
 
Hao watoto wanajifunza Quran pekee au Kuna kazi nyingine za kiuchumi wanafanya kama kilimo na ufundi!!?
Kwasababu Quran sio chakula pekee Cha mtu kula ,lazima kuwe na kazi za kiuchumi ambazo kijana anajifunza kujitegemea baadae!!

Kujifunza Quran pekee hakutoshi kumuandaa kijana kujitegemea badala ya kija kuwa mzigo Kwa taifa!!

Mimi kama kiongozi ajaye,nadhani shule iboreshwe zaidi ya kusoma Quran kuwe na elimu ya mtaala was kawaida na ufundi stadi plus kilimo Ili tupate complete package ya kijana sio kuhifadhi tu Quran pekee huyu mtoto hatokula Quran asipojifunza kazi!!
Kwani wanafunzi wanaosomea ualimu pale UDSM main campus na DUCE huwa wanafundishwa fani gani za ufundi? Ulishawahi kuwaona wakifundishwa welding,kushika majembe, uashi n.k?

Markaz wanafunzi wanasoma kwa muda fulani wakishahitimu hurudi makwao kuendelea na maisha yao mengine kama kawaida.
 
Msikiti, Kanisa ni sehemu ya kusali na kuondoka. Kama ni kulala au hiyo kula, kuhifadhi wakimbizi, hospital n.k hizo kwa mujibu wa sheria na taratibu za nchi ni huduma tofauti ambazo kila moja ina taratibu zake, sheria zake, vibali vyake na haya mamlala zake.
Dini zinatakiwa ku comply na Sheria za nchi, siyo vinginevyo. Haitakiwi nchi kufuata sheria na taratibu za dini.
Hiyo ni definition yako ya kanisa ila kwa waislam msikiti ni taasisi kubwa ndio sehemu waislam wanapata elimu yao ya kiroho n.k
 
Amani iwe nanyi.

Hivi karibuni, Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe amezua taharuki na sintofahamu kwa Waislamu wa Wilaya ya Kisarawe na Tanzania kwa ujumla baada ya kuvamia msikiti huko Kiluvya na kufungia kituo cha kuhifadhisha Quran. Alitoa amri kuwa wanafunzi warudi makwao na akasema kuwa kitendo cha wanafunzi wa Kiislamu kukusanyika na kusoma dini yao ni udhalilishaji.

Hii ni chokochoko dhidi ya Uislamu na Waislamu. Jamii ambayo kwa miaka mingi imekuwa ikijenga amani na maadili mema katika nchi hii. Masuala ya imani sio masuala ya kuyafanyia mzaha kwa kuwa yanagusa mioyo ya watu wengi na ni rahisi sana kuivuruga amani endapo mtu ataichezea ama kuidhihaki dini ya watu fulani.

Leo hii, Mkuu mpya wa Wilaya ya Kisarawe aje kuwafundisha Waislamu tafsiri na kazi ya msikiti. Ni jambo la ajabu na aibu sana.

Alilofanya Petro Magoti ni kutafuta "kiki" tu, na kuleta kebehi na kudhalilisha Waislamu na Uislamu kwa ujumla. Jambo la hatari sana.
Hili andiko ni ishara ya hasira ya kuzuia mafunzo ya kigaidi yaliyokuwa yakitolewa.
Tena usijaribu kutumia neno uslamu na waislamu kama namna ya kupata kuungwa mkono na wenzio wengi.

kaa ukijua zama zimebadilika,
ukibeba jambia sitakimbia, nitabeba panga.
ukibeba mawe nitabeba mawe
ukibeba bomu, nitavaa mabomu.
ukibeba bunduki, nitakuja nazo
ukituma majini nitakutumia mapepo (au unabisha?)

ZAMA ZA KUOGOA UISLAMU NA WAISLAMU ZIMEKWISHA!
 
Uliyewasilisha mada ombi langu kwako.
Naona unaipenda dini na haupendi mabaya yatokee.
Naomba miwe mnashiriki viongozi wa kiislam wanapoitisha michango kwa ajili ya maendeleo ya dini kama ujenzi wa madarasa.
Naomba anzisha harambee hapahapa tuwachangie watoto wa kisarawe wapate elimu ya dini kwa kuwajengea madarasa au kununulia vitanda
Unaweza kuuona uongozi wa msikiti wa salafi kiluvya wakakupa taratibu za kuwasilisha michango yako.

Shukrani
 
Hiyo ni definition yako ya kanisa ila kwa waislam msikiti ni taasisi kubwa ndio sehemu waislam wanapata elimu yao ya kiroho n.k
Msikiti unasajiriwa kwa mujibu wa Sheria za Tanzania siyo kwa mujubu wa Sheria za Yemen wala Oman.
Msikiti ukitaka kutoa huduma za afya huo ni utarayibu mwingine chini ya sheria na mamlaka nyingine, na haitaitwa Msikiti tena, ndivyo ilivyo kama Msikiti utataka kutoa huduma za malazi, n.k
Mbina mnakuwa wazito sana kuelewa
 
mimi kilichonikera ni pale anasema, kama isingekuwa nyumba ya ibada ningekuweka ndani leo. who is he? mkuu wa wilaya mbona mtu mdogo sana, anatishia watu kuwaweka ndani?
Kwani hana mamlaka hayo?
 
Watoto wenye umri wa kwenda shule wawe shuleni acheni mbambamba baadae mnatuletea watu wa hovyo mitaani huku tufanye mambo kama Dunia ilivyo mbona mnataka kujifanya vyura viziwi?kila siku watu wanasisitizwa kusoma wewe unafungia watoto wa watu eti wasome dini ukijua wazi Mbeleni maisha yao yatakua magumu watakosa Ajira watakosa maisha mazuri hapa Duniani na Ahera waislamu badilikeni
Kuna muislam alishakuja kukulilia umpe pesa ya kula? Unajuaje kuwa mbele maisha yao yatakuwa magumu? Unaijua kesho yako utaamkaje?
 
Amani iwe nanyi.

Hivi karibuni, Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe amezua taharuki na sintofahamu kwa Waislamu wa Wilaya ya Kisarawe na Tanzania kwa ujumla baada ya kuvamia msikiti huko Kiluvya na kufungia kituo cha kuhifadhisha Quran. Alitoa amri kuwa wanafunzi warudi makwao na akasema kuwa kitendo cha wanafunzi wa Kiislamu kukusanyika na kusoma dini yao ni udhalilishaji.

Hii ni chokochoko dhidi ya Uislamu na Waislamu. Jamii ambayo kwa miaka mingi imekuwa ikijenga amani na maadili mema katika nchi hii. Masuala ya imani sio masuala ya kuyafanyia mzaha kwa kuwa yanagusa mioyo ya watu wengi na ni rahisi sana kuivuruga amani endapo mtu ataichezea ama kuidhihaki dini ya watu fulani.

Watanzania tumelelewa katika misingi ya amani, upendo, umoja na mshikamano. Hii ni mizizi iliyoasisiwa na wapigania uhuru wa nchi hii na tumeweza kudumu katika misingi hiyo kwa miongo kadhaa sasa.

Anapotokea mtu, awe kiongozi ama yoyote yule, akafanya dhihaka, kukashifu, kubeza na kuingilia imani za dini fulani basi bila shaka anapaswa kukemewa kwa nguvu zote.

Serikali ya Rais Mama Samia ni serikali sikivu na yenye weledi inayosimamia misingi iliyowekwa na waasisi wa taifa hili. Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe hakupaswa kuzua taharuki kwenye vyombo vya habari kwa kufanya ziara ya kushtukiza usiku wa manane msikitini, ambayo Waislamu wameitafsiri kama uvamizi dhidi ya msikiti huko Kisarawe na kuamuru kituo cha kuhifadhisha Quran kifungiwe huku akiita kuwa ni udhalilishaji.

Pia, alidai kuwa misikiti ni sehemu ya watu kuswali na kuondoka tu huku akitumia kauli za kebehi na dharau kwamba watoto wanalala kama nyanya, wamepangwa kama tofali za block, hata nguruwe hawezi kulala katika mazingira hayo. Mara aseme watoto hao walipaswa wachapwe viboko wote na wazazi wao wawekwe gerezani kwa kuwa wameshindwa kuwalea! Hizi ni dharau kwa wazazi wa Kiislamu! Mzazi anayempeleka mwanae kuisoma dini yake ili awe na maadili mema katika jamii yake aonekane ameshindwa kumlea mwanae!

Leo hii, Mkuu mpya wa Wilaya ya Kisarawe aje kuwafundisha Waislamu tafsiri na kazi ya msikiti. Ni jambo la ajabu na aibu sana.

Waislamu nchini Tanzania wana taasisi yao ya BAKWATA, ambayo inashirikiana na taasisi nyingine ndogondogo kusimamia masuala ya Waislamu kwa ujumla. Petro Magoti alishindwa nini kuongea na uongozi wa BAKWATA unaoongozwa na Mufti Abubakar bin Zuber kuwa waboreshe kituo hicho cha msikiti wa Kiluvya ili kuweka mazingira rafiki ya vijana wa Kiislamu kuisoma dini yao na jambo hilo lisifike kwenye mitandao na kuzua sintofahamu kama alivyofanya yeye?

Msimamizi wa kituo cha msikiti wa Kiluvya alionekana akimueleza Mkuu huyo wa wilaya kuwa wanafunzi wanaishi katika hali hiyo kwa dharura tu huku jitihada mbalimbali za kuanzisha ujenzi wa mabweni zikiendelea. Nondo, mchanga, cement na matofali tayari vimeshakusanywa na jitihada za kuomba vibali vya ujenzi zikiendelea kufanyika ili kuhakikisha wanafunzi wanaishi katika mazingira rafiki.

Wito wangu kwa Rais ni kuhakikisha kuwa wateule wake kama Petro Magoti hawaingilii masuala ya kidini moja kwa moja kwa sababu ni eneo nyeti linaloweza kuvunja amani ya nchi hii kwa haraka sana. Awashauri wateule wake wawe na busara katika masuala ya utawala.

Alilofanya Petro Magoti ni kutafuta "kiki" tu, na kuleta kebehi na kudhalilisha Waislamu na Uislamu kwa ujumla. Jambo la hatari sana.

Video ya Sheikh akitoa mapendekezo kwa serikali nini kilipaswa kufanyika.

Pia soma:Kisarawe: DC Petro Magoti ameutaka Msikiti unaotoa elimu ya dini kwa watoto 96, kuwarudisha walipowatoa sababu ya Mazingira Mabovu ya malazi
Kisaikolojia tu kwa alivyo huyo DC hawezi kuwa sawa sawa hivyo labda ungeanza Kwanza kumuombe akatibiwe vizuri.
 
Back
Top Bottom