Waislam tunapaswa kuondokana na upofu wa dini la sivyo tutaonekana wote hatuna akili

Waislam tunapaswa kuondokana na upofu wa dini la sivyo tutaonekana wote hatuna akili

Ewe kijana umejaribu kuelezea jambo kwa hoja ila embu rudi kwanza nyuma hili jambo lilipo anza na mpaka lilipofika umewasikia BAKWATA wakitoa neno lao au kuchangia

JE,umemsikia mufti Zuber au Balaza la ulamaa likitia neno

Unasema wew ni muislam sikatai,unaweza ukawa n kwel muslim ila wajina n sio vitendo
Naomba nikukumbushe kitu viongoz wa Dini waliungna na kutoa mapendokezo yao na wakapewa Ahad ya kuwa yatafanyiwa kaz

Je, TEC wao walishindwa nin kuwa na subra mpak hapo muda waliopewa

Je TEC kutoa walak na kusema kuwa watanzania hawautaki mkataba wa bandar ni haki kuwasemea wtz wote

Kama kwel TEC,walikuwa wanawasemea wtz ni kwel sisi sote ni wakatolik kwa maaan walaka umeenda kusomwa katika makanisa yao na sio kwa wasiokuwa wao

Tafuta nukuu za mwambusi,mbowe na yule mtumish wao na zunguka huko mitandaoni uone kila pande inapotoa hisia zao badala za hoja zen rudi hap unipe nukuu japo moja wa shekh wakat kuhusu bandar

Natoa rai kuwa sio muumini wa BAKWATA ila kweny hil naona wametumia hekima na busara kwa kukaa kimyaa mpka muda utakapo fika

Mwisho kabisa kwako wew mwandish Rudi kasome tena QURAN maana inaweza kuwa sio kwa ajili yako na hao walio tanguliza hisia zao,

Baadhi ya vipengele katik IGA kwa upande wa bandar vina matatizo na vimejadiliwa na mawaziri pamoja na wabunge ambao 95% sio waislamu na kuvipittisha kam ambavyo vilipitishwa huko nyuma na wasomi weny PhD

..kwenye suala mkataba na Dpw huenda Mama Abduli na genge lake wanataka kupiga danadana kama walivyofanya kwenye maridhiano na Chadema au suala la katiba mpya.

..nawaunga mkono Tec kujitokeza na kueleza madukuduku yao kuhusiana na mkataba wa Dp ili Mama Abduli apate pressure na kuchukua hatua za haraka kurekebisha kasoro.
 
JokaKuu upo sahihi kabisa na mtazamo wako, tuache ushabiki wa udini katika mambo yenye maslahi ya taifa, nina uhakika kwamba hoja kama unazozileta ndiyo zingekuwa hoja za msingi halisi wa kupinga huu mkataba, nina uhakika kwa asilimia mia tusingefika katika haya malumbano yasiyo na tija, kuwacha mada husika na kuanza kushambuliana kwenye mtazamo wa udini.
Sisi sote ni watanzania na nia yetu ni kuona nchi yetu inapiga hatua kimandeleo bila ya kujali imani zetu, kwani kuna wangapi walikuwa waislamu huko nyuma wakawa wakristo na kuna wangapi wakristo wamekuwa waislamu, mambo ya imani yabaki kwenye mioyo yetu.
Tanzania tumetoka mbali mpaka kufika hapa tulipo, na tuna safari ndefu mpaka tufike mahali ambapo kila mtanzania atafurahia maisha mazuri kwa utanzania wake. Ulimwengu upo kwenye vita vya kiuchumi, jana tumeona BRICS inavyozidi kukuwa, lazima tusome alama za nyakati. Sisi kama waafrika wengine ambao tumebarikiwa kuwa na rasilimali nyingi lakini hatufaidki nazo, sidhani kama sababu ni viongozi wetu, na haiwezekani Afrika nzima hatujielwi. Tatizo lipo kwa hao wakoloni wa kisasa wanaondelea kutupelekesha.
Naomba kwanza kama watanzania tujifunze diplomasia ya kiuchumi, tusome sheria zetu tuangalie vipi tunaweza kuzirekebisha ili tuendane na wakati. Tatizo letu tunakosa elimu ya mambo ndiyo maana tunatumia muda mwingi kulumbana katika mambo yasiyo na tija, na kuna mataifa yanafurahia hivi tunavyofarakana.
Tuwe na forums zitakazojadili mambo ya msingi kielimu na si kimihemko.
Tanzania itajengwa na watanzania wenyewe na si vinginevyo.
Elimu,elimu,elimu
 
Sioni mahusiano yoyote ya haya uyasemayo na dini. Kwenye huo mfano wako hapo tatizo ni kutokushika dini ama kutojua kuna kifo? Sioni mahusiano yoyote kati ya kifo na dini.
Unasau sana kunasehemu umesema mwenyedini anaishi kwa tabu kuliko mwenye pesa kukiwa namaana masikini ni mwenyedini ndio nikakujibu mtu aishi kwa mkate............
 
Unasau sana kunasehemu umesema mwenyedini anaishi kwa tabu kuliko mwenye pesa kukiwa namaana masikini ni mwenyedini ndio nikakujibu mtu aishi kwa mkate............
Sio lazima aishi kwa shida, bali mwenye pesa kwa vyovyote mambo yake yatakuwa mazuri lazima.
 
Rais mstaafu Mwinyi alipowaambia pelekeni watoto shule wakamlamba kibao cha uso hadharani. Sidhani kama ndugu katika imani watakuelewa mtoa mada
 
Kwa ufupi unataka tuwe murtad ..maana uislamu ni Dini so tuachane na uislam
 
Pale mlango wa kuingia Ofisi ya Rais (Ikulu) kuna maandishi yanasomeka hivi (ادْخُلُوهَا بِسَلَامٍ آمِنِينَ), maandishi haya yanatoka katika Aya ya Quran Surat Al HIJR Aya Ya 46 inayosema
ادْخُلُوهَا بِسَلَامٍ آمِنِينَ
Wataambiwa "Wacha Mungu" Ingieni kwa salama na amani. Ikisomeka (Udkulu_Ha_Bi_Salamin_Aminina)

Jina Hili la (Dare Salaam) lilibadilishwa na Wajerumani Kutoka katika jina la Asili la (DARU SALAAM) baada ya Wajerumani kuwatoa Waislamu kimabavu katika eneo hilo na kuiweka Ikulu mwaka 1870.

Ikumbukwe kwamba Ikulu hii ilikuwa msikiti uliojengwa na Sultan Majid kutokea Zanzibar Mwaka 1865 kwa ajili ya watu kujifunzia Quran na kusoma elimu ya Dini ya kiislam (leo tungesema ulikuwa msikiti wenye chuo cha Madrasa ) ambako watu mbalimbali kutoka Congo, Malawi, walifika kusoma hapa. Jengo hili likaitwa #DAR_U_SALAAM (Dar es salaam) kama walivyo zoea wengi. Neno hilo ni neno la Kiarabu lenye maana ya NYUMBA YA AMANI. Neno hili sio geni Duniani, ukienda LEBANON utakuta Dar Salaam..

Kwa hiyo katika mambo tunayoweza kuyafundisha kama historia ni haya lakini sio huku tunakotaka kwenda.
Ahsante sana kwa hii elimu.
 
Imani haina evidence.
Kwako wewe hautoamini .tunajuwa ushahidi upo mfano kilakilicho gunduliwa kimeandikwa katika vitabu vyadini yesu aliishi duniani lakini vitabu vyote vinatambua alipaa unaweza kubisha lakini hakuna kitu kipo tu mfano wewe apo umevaa hiyo nguo yupo aliotengeneza hapo najuwa utaamini japo hukumuona kwanini ukatae hakuna alioanzisha mwili wako japohukumuona?
 
Elimu,elimu,elimu
FM Tantawi hujakosea, sisi tumesomeshwa kuwa elimu ina shibri 3, mtu akifikia shibri ya kwanza anakuwa na kiburi, na akifikia shibri ya pili anakuwa mnyenyekevu, na akifikia shibri ya tatu anasema yeye hajui kitu.
Angalizo.
Shibri ni upimaji wa zamani mtu anapima kutoka kwenye ncha ya kidole gumba mpaka mwisho wa ncha ya kidole kidogo wakati vidole vyako umevitanua.
 
yani unakuta mtu anapinga tu wakati hata shughuli za Bandari hazielewi.Mnakali uislamu na ukristo wenu wakati hakuna mnacho kipata, Hii nchi sijui imelogwa na nani
Kwa wanao jishughulisha na Bandari ndio wanaelewa ubovu uko wapi, jinsi mali zinaingizwa utasema bandari ni mali binafsi, mitambo ya kupima mafuta kila siku mibovu, wizi bandarini na Lazima uwalipe baadhi ya watu ndio mizigo itoke haraka. Ni usumbufu ambao wafanya biashara ndio wanao upata. Halafu anakuja fala asie hata na kibanda cha kuuza sigara anapinga Mkataba humu.
 
Kama kuna kitu Waislamu tunapaswa kukifanya katika kuandika HISTORIA yetu na ikasomwa kila baada ya sala ni hii ya Ikulu ya Magogoni hapa Dar es salaam maana ni historia yetu na ni halali kwetu kufanya hivyo ila sio kwenye suala la Mkataba wa Bandari; huko tunahitaji kuwa na ufahamu wa kutosha kuhusu mikataba ya kimataifa.

Viongozi wetu hasa Ma-Imamu wetu na wengine wanaokaribishwa kutoa neno, wakumbuke kwamba suala la Bandari linahitaji udadavuzi wa SHERIA na SIO SHARIA. Hili la Bandari halihitaji MUAZINI kulisimamia, linahitaji wataalamu wa sheria kulichambua nando maana hatua yakwanza kabisa kupinga ilipelekwa mahakamani kupata ufafanuzi wa kisheria, hukumu ikatoka kwamba mkataba unazo dosari unatakiwa kurekebishwa. Kitaalamu hii ilishindikana mahakama kutengua maamuzi ya Bunge bali ilishauri Bunge lipitie sheria hizo litekebishe huo mkataba. Kwa kifupi ni kwamba MKATABA hauna faida kwa taifa.

Katika eneo ambalo Waislam tunapaswa kuliellewa ni kwamba tunapaswa kulizingatia ni hili viongozi wetu kuweka maneno ya chuki dhidi ya imani zingine, tukishindwa kuwahoji misikitini basi tutoke tuwaache waendelee na SOGA zao baada ya IBADA.

Kuna ujinga unasambazwa kwamba UJIO wa DP World utalifanya KANISA lisiingize makontena yao kwa msamaha wa kodi. Innalillah Wainalillah rajiun; kwanza tutambue masuala yote ya kikodi yanapangwa na serikali yetu, ni suala la DP World kukabidhiwa list ya misamaha ya KODI kwa taasisi husika. Na hapo hakuna atakaepinga. DP World hawaji kupanga masuala ya kodi ama tozo za bandarini; bei elekezi za bandari zitaendelea kusimamiwa na TPA na TRA. Hili Waislam tulielewe; tusipuyange.

Yaani kwa kifupi ile misamaha ambayotuliipeleka ya kuomba kuondolewa kodi ya TENDE, msamaha wa kodi ya MAJI ya ZAMZAM na mengineyo DP WORLD watayakuta mezani. Halafu pia wataikuta list ya misamaha ya kodi ya VIFAA TIBA, VIFAA VYA KUJIFUNZIA WANAFUNZI SUNDAY SCHOOLS, SECONDARY, COLLEGES nk wataikuta pale. Kwa hiyo hakuna kitu KANISA watapoteza bali wenzetu wameenda mbali zaidi kwa kuangalia uhalali wa mkataba na sio kuhusu misamaha ya kikodi au kwa sababu mwekezaji ni kampuni kutoka taifa la kiarabu. Mataifa mangapi ya kiarabu yamewekeza hapa? Ukienda pale Ngorongoro kuna kampuni ngapi za kiarabu? Ukienda Loliondo pale kuna maeneo ukifika unakaribishwa UAE [emoji1256], umewahi kuona kanisa linaongelea hayo?

Hawa akina Arab contractors wanaojenga Bwawa la Mwalimu Nyerere si wanatoka Misri? Au wale mnawachukulia kuwa ni wajukuu wa FARAO? Na hawa wanaojenga SGR si ni waarabu wa Uturuki [emoji1250] ? Au wale mnawachukulia ni ndugu zake Ottoman? Jikiteni katika kuzijadili hojaza TEC na sio kuwajadili waliokaa kuzichambua hizo hoja.

Anyway; ngoja niwarudisheni kwenye historia kidogo kuhusu Ikulu ya Magogoni na hili mkalikalie vikao mlijadili pengine mnaweza kulidai iwe mali yetu Waislam maana kihistoria ni mali ya Waislam na hata Magufuli aliamua kuhamisha makao makuu Dodoma ili ikulu hii iwe sehemu ya historia mkapate kuijua hii Ikulu vema.

Pale mlango wa kuingia Ofisi ya Rais (Ikulu) kuna maandishi yanasomeka hivi (ادْخُلُوهَا بِسَلَامٍ آمِنِينَ), maandishi haya yanatoka katika Aya ya Quran Surat Al HIJR Aya Ya 46 inayosema
ادْخُلُوهَا بِسَلَامٍ آمِنِينَ
Wataambiwa "Wacha Mungu" Ingieni kwa salama na amani. Ikisomeka (Udkulu_Ha_Bi_Salamin_Aminina)

Jina Hili la (Dare Salaam) lilibadilishwa na Wajerumani Kutoka katika jina la Asili la (DARU SALAAM) baada ya Wajerumani kuwatoa Waislamu kimabavu katika eneo hilo na kuiweka Ikulu mwaka 1870.

Ikumbukwe kwamba Ikulu hii ilikuwa msikiti uliojengwa na Sultan Majid kutokea Zanzibar Mwaka 1865 kwa ajili ya watu kujifunzia Quran na kusoma elimu ya Dini ya kiislam (leo tungesema ulikuwa msikiti wenye chuo cha Madrasa ) ambako watu mbalimbali kutoka Congo, Malawi, walifika kusoma hapa. Jengo hili likaitwa #DAR_U_SALAAM (Dar es salaam) kama walivyo zoea wengi. Neno hilo ni neno la Kiarabu lenye maana ya NYUMBA YA AMANI. Neno hili sio geni Duniani, ukienda LEBANON utakuta Dar Salaam..

Kwa hiyo katika mambo tunayoweza kuyafundisha kama historia ni haya lakini sio huku tunakotaka kwenda.


Tujisahihishe
Mengi yao yangekuwa na elimu kama wewe TANZANIA yetu ingekuwa salama.
Ogopa sana kushindana ama kubishana na mtu mtumia mihemko badala ya akili.
 
Back
Top Bottom