Waislamu hawawezi jibu swali hili : Quran 15 :26 "Trinity"

Hakuna biblia inayo sema > Mungu ni nafsi 3 wala inayo sema mungu ana nafsi 3 kwa sababu hayo mafundisho ni ya shetani ...MKITAKA KUJUA INJILI YA KWELI NA FAFANUZI YAKE NIULIZENI MIMI..TU
 
Siyo makanisa tu hata madhehebu yote ni miliki ya shetani ...Mungu wa kweli hana madhehebu hata siku moja ...mafundisho ya makanisani ni potovu kwa asilimia 90% tofauti na injili ya kweli .... nikitaka naweza kupnyesha hapa

Sawa, kama unasema makanisa na madhehebu yote ni ya Shetani na 90% ya mafundisho yao ni potovu, basi usitupe kauli tu, Lete ushahidi wa Biblia .

Lakini kuna swali muhimu: “Injili ya kweli” uliyo nayo umeipata wapi, na kwa mamlaka gani umeamua kwamba tafsiri yako ndiyo sahihi?

Biblia yenyewe inatuonya tusiamini kila anayesema ana ukweli:

“Wapenzi, msiamini kila roho, bali zijaribuni hizo roho kwamba zimetokana na Mungu.” 1 Yohana 4:1

Na Yesu alisema:

“Mtawatambua kwa matunda yao.” Mathayo 7:16

Lete hayo mafundisho unayosema ni potovu, moja baada ya jingine, uonyeshe aya ya Biblia inayopingana nayo, halafu tuchambue kwa muktadha.

Usiseme tu “90% ni potovu.” Taja hizo 90% na uthibitishe kwa Biblia. Tuanze mjadala wa maandiko hapo.
 
Hakuna biblia inayo sema > Mungu ni nafsi 3 wala inayo sema mungu ana nafsi 3 kwa sababu hayo mafundisho ni ya shetani ...MKITAKA KUJUA INJILI YA KWELI NA FAFANUZI YAKE NIULIZENI MIMI..TU

😄 Unasema Biblia haisemi “Mungu ni nafsi 3”, lakini unadai fafanuzi ya Injili ya kweli ni wewe! Swali ni: Biblia imekupa wewe mamlaka gani kuwa mwamuzi wa mwisho?

Paulo alisema: “Msizidi kusema, kila mmoja wenu, kinyume cha yaliyoandikwa.” (1 Kor. 4:6)

Basi lete hiyo “Injili ya kweli” yako aya kwa aya, tuiweke mezani na tuipime kwa Biblia. Si kwa maoni yako binafsi.
 
Mimi ni mtu mwenye uwezo mkubwa wa kilogic na kiakili na nilipo soma biblia (injili) niligundua tatizo siyo injili ni potovu... tatizo wakristo ndiyo wamepotosha injili ...ila nilipo somq msahafu nimegundua tatizo ni msahafu wenyewe ndiyo potovu nq waislamu wanajaribu kuupamba tu
 

Kuwa na akili na logic si uthibitisho kwamba unachosema ni kweli. Ushahidi ndio kipimo.

Umesema Wakristo wamepotosha Injili, lakini Qur’an inasema:

“Na watu wa Injili wahukumu kwa yale aliyoyateremsha Mwenyezi Mungu ndani yake.” Qur’an 5:47

Basi kama Injili ilikuwa imepotoshwa, kwa nini Qur’an iwambie watu wa Injili wahukumu kwa yaliyomo ndani yake?

Na ukidai Qur’an imepotoshwa, lete ushahidi, si madai.
 
Fafanuzi zangu zinatokana na uelewa ambao unaupima kwa kujibu hoja mbalimbali .... waulize waislamu wenzio walio kuja hapa kupinga fafanuzi zangu .....waislamu waliuliza hapa je YESU ALIWAHI KUINGIA KWENYE NYUMBA YA IBADA INAYOITWA KANISA ? Niliwajibu hapa wakakubali majibu niliyo wapa.
 

😄 Hiyo si hoja ya kujivunia. Mtu kukubaliana na jibu lako hakuthibitishi kwamba wewe una tafsiri sahihi ya Injili. Ukweli haupimwi kwa kura.

Unasema una “uelewa mkubwa” na Waislamu wamekubali majibu yako , basi acha kujisifu, lete ushahidi wa Biblia.

Na kuhusu swali la Yesu kuingia “kanisani”: Biblia inasema aliingia sinagogini (Luka 4:16), si kanisa la Kikristo. Usichanganye maneno ili ujenge hoja ambayo Biblia haisemi.

Sasa acha “niliwajibu wakakubali”; lete aya, muktadha na ushahidi. Tutaangalia kama tafsiri yako inatoka kwenye Biblia au kichwani mwako.
 
Huu ni ushahidi kuwa kuran ilidukua biblia na lao ni moja kama ilvyo asili yao. Ni ngano za kijinga za kale zinazoaminiwa na mwazwazwa na malimbukeni. Period.
 
Huu ni ushahidi kuwa kuran ilidukua biblia na lao ni moja kama ilvyo asili yao. Ni ngano za kijinga za kale zinazoaminiwa na mwazwazwa na malimbukeni. Period.

“Tu/We” katika Qur’an haimaanishi Utatu, bali ni mtindo wa lugha wa ukuu. Qur’an pia inasema wazi: “Hakika Mimi ni Mwenyezi Mungu; hakuna mungu ila Mimi.” (20:14)

Na Biblia yenyewe inasema “tumfanye mtu kwa mfano wetu” (Mwanzo 1:26), lakini mstari unaofuata unasema “Mungu akaumba mtu” (Mwanzo 1:27)—si “miungu wakaumba.”

Kwa hiyo “We = Trinity” ni tafsiri aliyoibuni, si ushahidi. Kama anadai Qur’an iliiga Biblia, alete au leteni ushahidi wa kihistoria badala ya matusi.
 
Hakuna cha mtindo bali ushirikina mtupu. Unaweza kusema uwili basi. Maana, mtu haiwi muislam bila kuwataja allah na moody. Unaona?
 
Leo umemuweza Lwiva 😁😁
 
Leo umemuweza Lwiva 😁😁
Kaniweza nini ...neno utatu halina shida tumia akili ....kwani muislamu akisema kwenye uislamu kuna utano kwa maana ya nguzo 5 za uislamu utabisha au utasema amekosea ? Pia hiyo comment akunijibu mimi ...mimi sikuwai kusema utatu wa makanisani ni sahihi ...
 

Hapo ndipo unachanganya neno na dhana. 😄

Muislamu akisema “utatu wa nguzo” anamaanisha vitu vitatu vinavyohusiana, si kusema Mungu mmoja ana nafsi tatu.

Lakini unaposema Utatu wa Mungu, unadai Mungu mmoja yupo kama Baba, Mwana na Roho Mtakatifu. Hiyo ni dhana tofauti kabisa.

Kwa hiyo usitumie “utatu wa nguzo” kuthibitisha “Utatu wa Mungu.” Maneno yanaweza kufanana, lakini maana si moja.
 
Hizo fafanuzi ninazo kupa mo zipo kwenye injili na biblia kwa ujumla ...tatizo ni uelewa wa mtu ....

FAFANUZI NINAZO TOA MIMI NI SAHIHI KWA SABABU UKIZIPIMA NA NENO LA INJILI LINALANDANA NA KULETA MAANA SAHIHI NA ILIYO NYOOKA NA KUONDOA MIGONGANO YOTE ....TAFSIRI NINAZO KUPENI MNAWEZA KUZIFANYIA PROOF KWA KUZIPIMA NA NENO..
 

Sawa, kama tafsiri zako zinaendana na Injili na zinaondoa migongano yote, basi zithibitishe kwa maandiko.

Usiseme tu “uelewa wa mtu ndio tatizo” au “tafsiri yangu ni sahihi.” Huo ni msimamo wako binafsi, si ushahidi.

Lete tafsiri zako moja baada ya nyingine, pamoja na aya zinazozithibitisha, tuzipime kwa Biblia. Kama kweli ni sahihi, maandiko yatajitetea yenyewe bila kuhitaji kujitangaza kuwa wewe ndiye mwenye tafsiri sahihi.
 
Utatu wa Mungu mmoja mwenye nafsi 3 ni upotovu nimesha kuambia ..mbona unanisumbua na mafundisho potovu wa wahuni ....hayo hayanihusu mimi ...ungeniuliza kuhusu usahihi wa mafundisho ningekueleza ..siyo kunilisha dhana potovu za wakristo wasio na akili.
 

Kama unasema Utatu ni upotovu, usitukane, uthibitishe kwa Biblia. Umesema tafsiri zako ni sahihi; basi lete aya zinazozithibitisha. Hoja hupimwa kwa maandiko, si kwa kujitangaza kuwa wewe ndiye mwenye uelewa sahihi.
 
Kama unasema Utatu ni upotovu, usitukane, uthibitishe kwa Biblia. Umesema tafsiri zako ni sahihi; basi lete aya zinazozithibitisha. Hoja hupimwa kwa maandiko, si kwa kujitangaza kuwa wewe ndiye mwenye uelewa sahihi.
Nilisha leta hapa fafanuzi chungu mzima ..wewe ulikuwa wapi ...mfano kama ..baba ni nafsi moja na mwana(yesu) ni nafsi ya pili , kwanini roho mtakatifu iwe ni nafsi moja ? Kwanini zisiwe nyingi maana imeandikwa wote wakajazwa ROHO MTAKATIFU ...Hivyo Roho mtakatifu ukaandani yq wachamungu wengi sasa kwa mantiki vipi iwe ni nafsi moja tu na si nyingi ?
 
Umechanganya kujawa na Roho Mtakatifu na kuwa na nafsi nyingi za Roho. (Matendo 2:4) Watu wengi kujazwa na Roho mmoja hakumaanishi kuna Roho wengi. Lete aya inayosema Roho Mtakatifu ni nafsi nyingi; “wote wakajazwa” haitoshi kuthibitisha hilo.. Kila nikikuambia ulete aya unakimbia na kuzusha jipya . Bora kakojowe ukalale
 
Mungu alikuwa anapiga story na Malaika!

Mfano wa kibinadamu kabisa Boss wa kampuni binafsi anaweza kuwaambia tu kesho "Tupumzike" sio kwamba nyinyi wote sasa ni wamiliki wa ile kampuni!

Mifano ya Mungu ni halisia kwa mazingira yetu haya haya

TUMEAGIZWA UPENDO
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…