Pascal Mayalla
Platinum Member
- Sep 22, 2008
- 53,857
- 121,995
Wanabodi,
Watanzania wote waliosoma enzi za mkoloni mpaka tunapata uhuru, tumekuwa na elimu ya aina 3. Shule za serikali, Government Schools, Shule za Mission, na elimu ya madras kwa ndugu zetu Waislamu.
Shule za serikali zilikuwa chache na zilichukua wanafunzi wachache tena vichwa kweli kweli, hivyo Watanzania wengi waliemika kupitia Shule za Mission.
Elimu ya madrasa iliwahusu Waislamu pekee, lakini shule za serikali na shule za Mission zilichukua watu wa dini zote bila ubaguzi wowote.
Hivyo Watanzania wengi wa zamani waliobahatika kusoma elimu ya secondary, walisoma shule za misheni.
Kilichofanya Wakristo wengi zaidi kuwa ni wasomi kuliko Waislamu, ni changamoto ya ada za shule.
Watoto wa mikoa yenye mazao ya biashara, waliweza kusoma zaidi kwasababu wazazi wao waliweza kulipa ada, kutokana na kupata kipato, lakini watoto wa mikoa ambayo haikuwa na mazao ya biashara ikiwemo mikoa yote yenye Waislamu wengi, hawakubahatika kupata elimu ya kisasa.
Hali hii ilipelekea hata uendeshaji wa harakati za uhuru, kuongozwa na wasomi Wakristo, mfano vyama vyote vya siasa vilivyopigania uhuru, kuanzia AA kiliongozwa na Mkristo, Cecil Matola, TAA ikaongozwa na Dr. Vedastus Kyaruzi na TANU ikaongozwa na Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.
Kitu kizuri sana Shule za Mission zilichowafanyia Watanzania, akitokea Mwanafunzi very bright, akafanya vizuri mitihani yake na kufaulu vizuri, wale waalimu wa shule za Mission, usually makasisi, waliwachukua watoto hao na kuwasomesha bure, hivyo ndio wengi wa wasomi wa Kiislamu walivyopatikana, hivyo watu kama Juma Mwapachu na nduguye Bakari, kina Hamza Aziz, Inspector Rashid na Waislamu wengi wa enzi hizo, walisoma sekondari kwa hisani ya Shule za Mission.
Hisani hii, sio kwa ndugu zetu Waislamu pekee, hata Wakristo kutoka maeneo ambayo hawana mazao ya biashara, hivyo umasikini wa kipato unasababisha watoto wao hawezi kulipiwa ada, na kutosoma sana.
Hivyo wasomi wa mikoa ya Singida na Dodoma, kama kina John Samwel Malecela na nduguye Job Lusinde, washukuru sana Mission, vinginevyo bila hisani ya Shule za Mission, kuna watu wangeishia kuchunga mbuzi au kupiga dufu au kuadhini tuu lakini sasa ni wasomi wazuri na waandishi mahiri kwa hisani ya Shule za Mission.
Hivyo hili ni bandiko la kuwakumbusha ndugu zetu Waislamu waliofaidika na hisani ya kusomeshwa shule za Mission, wakumbuke fadhila, wawe ni watu wa shukrani, wawashukuru sana Wakristo, wazishukuru shule za Mission walizosomea, na kuwashukuru wale Makasisi waliowaokoa.
Ukifadhiliwa, usiwe mtovu wa fadhila, haiwezekani mtu ufadhiliwe shule za Mission, usome bure, halafu kila uchao ni kuwabeza tuu hao Wakristo waliokusomesha elimu yao hadi unaweza kuandika kwa kuwadogosha na kuwatukuza na kuwakweza Waislamu, mara kulalamikia mfumo Kristo, mara kulalamika, Waislamu wanabaguliwa kielimu, mara hivi mara vile...
Baada ya uhuru, Mwalimu Nyerere akataifisha shule zote za mission na Hospital zote za mission na kuigeuza za serikali, akatoa elimu bure kwa wote tangu darasa la kwanza hadi la chuo kikuu ili Watanzania wote wa dini zote na makabila yote wapate haki sawa ya elimu ya juu.
Wakati huo tukitumia mitaala ya Cambridge na mitihani ya Cambridge, bado walioingia sekondari ni watoto wa makabila yale yale, Wachagga, Wahaya, Wanyakyusa, Wasukuma, Wahehe, na watu wa dini ile ile!.
Nyerere akafuta mitihani Cambridge, tukaanzisha Baraza letu la mitihani na mitaala yetu, mitihani tukatunga wenyewe, bado wanaopasi ni makabila yale yale na dini ile ile.
Ndipo tukakubali ukweli mchungu kumbe kiwango cha IQ hakifanani kwa dini zote na makabila yote, ikakawa sasa inafanyika affirmative action ili ndugu zetu hawa nao wasome na makabila yote wasome, kwa kuweka different cut off points maeneo tofauti tofauti. The highest ni Bukoba cut off point ni 90, Kilimanjaro 80, Mbeya 70, Iringa, Kanda ya Ziwa 60. Muslim dominated areas 40, primitive tribes ikashushwa mpaka 0 kwa Hadzabe, na wakasomeshwa kwa nguvu mpaka form 4 na wote wakapata zero!.
Utaratibu huu ulisaidia sana Watanzania wote kupata fursa za elimu ya juu. Bakwata na taasisi za Kiislamu pia zikaanzisha sekondari za elimu dunia, japo performance ya Shule ya Islamic Seminary ilikuwa... niliwahi kuuliza humu Inawezekana Vipi Zanzibar Kuna Div I, Div II, na Div III Chache, Ila Div IV na Div Zero Nyingi?!. pia niliwahi kuuliza Je, kuna tofauti ya IQ za Watanzania kutokana na dini zao? Kuna dini wanapasi sana, wanafeli sana, huwa wanabaguliwa na kudhulumiwa?
Na hata baada ya Waislamu kusoma Shule za Mission by default, lakini sasa, nina rafiki zangu wengi ambao ni Waislamu, lakini wanasomesha watoto wao Shule za Mission, by choice, kutokana na ubora wa elimu unaotolewa na Shule za Mission, hawa wana appreciate sana Wakristo na Shule zetu, ila baadhi ya wale waliosomeshwa na Mission, badala ya shukrani ni kuwabeza tuu kila uchao!, jambo hili halina karma njema!, badilikeni shukuruni!
Hitimisho,
Tanzania ni circular state, haina dini, ila watu wake wana dini zao, ni muhimu sana watu humu tukawa na religious tolerance ya kuzivumilia dini na imani za wengine bila kuzibeza na kuzichokoa from time to time.
Kuwa appreciative ni pamoja na Wakristo kuwa na shukrani kwa Waislamu na mfono mzuri ni mimi mwenyewe nilipopandisha bandiko hili Je, kuna uhusiano kati ya IQ, Dini ya mtu na Longevity? Naomba kuwatumia Marais wa Tanzania kama Sampling hapa nilieleza jinsi viongozi Waislamu walivyo waungwana. Uungwana huu haupo kwa viongozi Wakristo hivyo unaweza kuwa umechangiwa na ile elimu ya madrasa.
Ndugu zetu Waislamu mliofaidika na shule za Mission, kuweni na shukrani kwa aliyewafikisha hapo nikitolea mfano mmoja wa Wanazuoni wasomi wa Kiislamu waliosomeshwa Shule za Mission, ambaye angalau ana shukrani, Mkuu Maalim Mohamed Said kama anavyoeleza mwenyewe
Paskali
Rejea ya Nyuzi nyingine za mwandishi kuhusu kuwa na shukrani, appreciation

Pascal,
Mbona hapa na mimi kushukuru shule za misheni?
Nimeanza darasa la kwanza Lutheran Primary School Moshi na nashukuru shule ilikuwa nzuri sana.
wakati alichangia uzi wangu huu Kwa Simulizi za Mwana JF, Maalim Mohammed Said, Sio Mtu wa Kubezwa, Mengine ni Ukweli Mchungu!, Ila Pia Sio Mtu wa Kupuuzwa!Asiyewashukuru watu hawezi hata kumshukuru Mungu.
Nawashukuru wamishionari ambao shule zao nimesoma.
Siwezi kuwa mwizi wa fadhila.
Paskali
Rejea ya Nyuzi nyingine za mwandishi kuhusu kuwa na shukrani, appreciation
- Waraka wa Pascal Mayalla - Asanteni Sana!
- CHADEMA kuweni na shukrani, punguzeni kulalamika, shukuruni kwa yote. Ile kesi mbaya! Shukuruni mahakama, Mashinji, CCM, Magufuli na Watanzania
- Asante Rais kuruhusu mikutano, tunakuomba uruhusu haki nyingine ambayo imeporwa ya Watanzania wote kuchagua na kuchaguliwa
- Asante Rais Samia kwa kuwasisitiza watendaji wa vyombo vya haki kuwa haki sio hisani, bali ni stahiki. Watende haki, tubadili Katiba kurudisha haki
- Asante Mungu kwa Rais Samia: Ni Msema Kweli na Mtenda Kweli, Ni Msema Haki na Mtenda Haki. Je, Ataruhusu Ubatili Huu Kuendelea Ndani ya Katiba Yetu?
- Wito kwa wanahabari: If you can't get what you want, just take what you get!