Waislamu Mnafeli wapi?

Utasema vipi Mungu anatupa nafasi ya kuchagua hatima yetu ikiwa hata kuzaliwa hatuchagui, tunajikuta tu tumezaliwa?
 
Utasema vipi Mungu anatupa nafasi ya kuchagua hatima yetu ikiwa hata kuzaliwa hatuchagui, tunajikuta tu tumezaliwa?
Mkuu hii hoja yako nilishaijibu hapo awali

Lakini ngoja nirudie tena,
Huwezi kuchagua kuzaliwa wakati awali hukuwepo mkuu

Mfano rahisi ni Mimi na wewe sasa hivi tunatembea na mbegu za kizazi chetu katika suruali zetu,je hiki kizazi ambacho hakijatokea au sababu ya kutokea kwake bado haijafanyika Kwa maana bado hatujakutana na mwanamke,je huyu mtoto atachaguaje kuzaliwa wakati bado hajapatikana au hayupo kabisa?
 
Huoni kwamba ukishaanza hoja yako na "huwezi kuchagua kuzaliwa" unakubaliana nami kwamba watu hawapewi uchaguzi wa kuzaliwa au kutozaliwa, na hivyo hoja yote ya kwamba wana uhuru wa kuchagua inatoweka?

Uhuru wa kuchagua kuzaliwa au kutozaliwa ndiyo uhuru mkubwa kabisa katika maisha, sasa utasema vipi tuna uhuru wa kuchagua katika maisha ikiwa hata huko kuzaliwa kwenyewe hatuchagui?

Kwa nini Mungu hakutupa uhuru wa kuchagua kuzaliwa au kutozaliwa, katufanya tujikute tumezaliwa tu?

Unataka kusema Mungu wako muweza yote alishindwa kufanya namna ya kutupa uchaguzi wa kuamua tuzaliwe au tusizaliwe?

Zaidi ya hapo, hata kwenye kuzaliwa hatuna uhuru wa kuchagua tunazaliwa wapi, hatuna uhuru wa kuchagua tunazaliwa na wazazi gani, hatuna uhuru wa kuchagua vinasaba vyetu vikoje, hatuna uhuru wa kuchagua tunazaliwa mwaka gani, siku gani, saa ngapi, na haya ni mambo yanayokuja kuathiri sana maisha yetu, sasa hapo utasemaje tuna uhuru wa kuchagua?
 
Je, unakubali/unaamini dhana ya sayansi isemayo energy can neither be created nor destroyed ?
 
Je, unakubali/unaamini dhana ya sayansi isemayo energy can neither be created nor destroyed ?
Katika muktadha gani?

Sayansi hiyo hiyo inasema all energy was created at the Big Bang. Kwa hivyo, kusema kwamba sayansi inasema energy can neither be created nor destroyed bila kuweka muktadha si sawa.
 

Mkuu naona umekaza Sana kwenye hii hoja huenda ndio msumari wako wa mwisho au kete yako ya mwisho katika haya majadiliano.

Kama Mungu angeamua kutupa huo Uhuru unao sema wewe basi WA Kwanza kupewa angekuwa Adamu,maana yeye ndio original yetu na sie wengine ni copy yake Tu,yeye aliumbwa lakini Sisi tumepatikana Kwa kuzaliana.

Je iweje anaezaliwa akawa na uchaguzi wakati ameshatengenezewa formular tayar?
 
Unaelewa kwamba unakubaliana nami kwamba hatupewi uchaguzi wa kuzaliwa au kutozaliwa?

Hilo unalielewa?

Tukubaliane hapo kwanza tujue tunapatana sawa mpaka hapo.
 
Unaelewa kwamba unakubaliana nami kwamba hatupewi uchaguzi wa kuzaliwa au kutozaliwa?

Hilo unalielewa?

Naweza kusema ndio au hapana kutokana na sababu zifuatazo

Inaweza ikawa ndio endapo tuliomba kupewa Uhuru na hatujapewa,hapo ndio tutasema tulitaka Uhuru hatujapewa

Lakini pili huenda hakukuwa na mantiki yoyote ya kupewa huo uchaguzi
 
Naweza kusema ndio au hapana kutokana na sababu zifuatazo

Inaweza ikawa ndio endapo tuliomba kupewa Uhuru na hatujapewa,hapo ndio tutasema tulitaka Uhuru hatujapewa

Lakini pili huenda hakukuwa na mantiki yoyote ya kupewa huo uchaguzi
Mungu wako mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote ni dikteta?

Hataki kuwapa watu uhuru wa kuchagua?
 
Waislamu mnaamin mko sahii ilo ndo tatizo lenu
Mkuu hayo yote yanatoka wapi

Mimi na Kiranga katika majadiliano je umeona namlaumu yeye kwa kutomwamini Mungu au yeye Kwa kunilaumu Mimi kuwa muislamu?

Usipende kuongea mambo mepesi mepesi Tu mkuu!
 
Mkuu hayo yote yanatoka wapi

Mimi na Kiranga katika majadiliano je umeona namlaumu yeye kwa kutomwamini Mungu au yeye Kwa kunilaumu Mimi kuwa muislamu?

Usipende kuongea mambo mepesi mepesi Tu mkuu!
Wapi nimekulaumu ebu ntolee kicha chako hapa
 
Mungu wako mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote ni dikteta?

Hataki kuwapa watu uhuru wa kuchagua?
Let's say hajatupa Kwa mtazamo wako

Je hiyo ndo inakufanya uamini kuwa hakuna mungu
 
Let's say hajatupa Kwa mtazamo wako

Je hiyo ndo inakufanya uamini kuwa hakuna mungu
Siyo kwamba inanifanya niamini kwamba hakuna Mungu.

Hilo litaonesha habari nzima ya kwamba Mungu katupa uhuru wa kuchagua ina contradiction. Ni uongo.

Na kama hatuna uhuru wa kuchagua maana yake hizi habari za kwamba Mungu atatuhukumu kwa kuangalia tuliyochagua nayo ni uongo.

Na hapo tutajiuliza, kwa nini Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote asitupe uhuru wa kuchagua?

Na hapo litatokea swali, huyu Mungu yupo kweli? Au watu wamemtunga tu?

Mbona habari za kuwapo kwake zina contradiction kila sehemu tukizichunguza?
 
Mungu alivyompa Adam uhuru wa kuchagua kati ya mti wa uzima au uzima na ubaya alikua dikteta unajua mambo mengine ni ya ajabu sana
 
Kuhusu kupewa Uhuru WA kuchagua tumepewa katika mambo mengi Sana,mfano Adam na Hawa waliambiwa wasile mti Fulani WA matunda,lakini wao walichagua Kula na kuyapata waliyoyapata

Iblis aliambiwa amsujudie Adam sijida ya heshima lkn yeye alichagua kukataa kumsujudia

Mungu amesema yeye ni mmoja Tu lakini kuna binadamu wameamua kuchagua miungu Yao mbali mbali,mpaka hapo tunaona binadamu Wana Uhuru WA kuchagua.

Ila linapokuja swala la kuchagua kuzaliwa hapo hatukupewa uchaguzi

Sasa kama kuna baadhi ya mambo tumepewa uchaguzi basi yatosha kusema kuwa Mungu ametupa uchaguzi

Na

Kama tusingepewq kabisa Uhuru WA kuchagua japo Jambo moja Tu,basi hapo ingetosha kusema kuwa hakika Mungu hakutupa uchaguzi kabisa.

Umezungumzia kuwa uwepo wa Mungu kila sehemu Una contradiction,je waeza dhibitisha juu ya Hilo swala?
 
Nakwambia hivi, kama Adam na Hawa hawakuulizwa waumbwe au wasiumbwe, wakajikuta wameumbwa tu, baada ya hapo huwezi kusema wamepeea uhuru.

Kwa sababu, uhuru wowote watakaopewa umechorewa mistari, wameshazaliwa, hawakuwa na nafasi ya kukataa kuzaliwa.

Ni sawa na kauli ya kumtuhumu mtengeneza magari wa Marekani Ford. Ford aliulizwa kama watu wana uhuru wa kuchagua rangi yoyote wanayoitaka kwenye magari anayotengeneza ya Model T. Ford akasema watu wanaweza kuchagua rangi yoyote, ili mradi rangi wanayochagua iwe nyeusi.

Nikikwambia unaweza kuchagua gari la rangi yoyote, ilimradi hiyo rangi iwe nyeusi, hapo nimekupa uhuru wa kuchagua rangi au nimekuchagulia?

Mungu muweza yote, mjuzi wa yote na mwenye upendo wote anakuwa contradicted na ulimwengu unaoruhusu mabaya.

Ama ulimwengu unaoruhusu mabaya upo, na Mungu huyo hayupo.

Ama huyo Mungu yupo, na ulimwengu unaoruhusu mabaya haupo.

Viwili hivi haviwezi kuwapo pamoja vyote, that is a logical contradiction.

Tunaona ulimwengu unaoruhusu mabaya upo.

Hivyo, Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote hayupo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…