Waislamu na Wakatoliki mko wapi Askofu Gwajima ananyanyaswa?

Tumesahau kuwa ukimya wetu ni baraka kwa uovu kuendelea.

Leo ni Gwajima, kesho ni imamu, keshokutwa ni padre, hadi lini tutakaa kimya? Serikali inapofunga nyumba ya ibada bila sababu za msingi, it's not just a church being attacked,, it's our collective conscience being violated.
 
Mara hii umesahau mjadala wako? Hii nchi ina majitu ya hovyo sana, hovyo kabisa
Nimekuuliza hilo swali kwanza halafu tuanzie hapo? Alipigwa risasi Tundu Lissu, akatekwa Azory Gwanda, akatekwa Ben Saanane, ameuawa mzee Kibao na wengine wengi. Bado mnachunguza au uchunguzi umefika tamati?
 
Kweli kabisa mkuu. Lazima tukemee huu ushetani unaoendelea hapa nchini.
 
Hili si suala la Gwajima peke yake wala dhehebu fulani, bali ni suala la hatima ya uhuru wa kidini kwa wadanganyika. Na kama kuna udhalimu unaoendelea, basi tuungane wote—Wakristo, Waislamu, na hata siye tusioamini—kupinga kwa sauti moja kwa njia za amani na heshima.
 
Well said mkuu. An attack on one is an attack on all.
 
Tatizo huwa anawatukana Mamba halafu Kafika mtoni anataka Mamba walewale wategeshe migongo yao avuke..!
 
Dawa ni kukaa mbali na siasa au u-wanaharakati. Mbona watekaji wasikuteke wewe tpaul ? Unafikiri huyo Mdude_Nyagali walimchukua tu akiwa anafanya kazi zake?

Kama una familia na inakutegemea acahana na hizi mbanga, utaishia kuwasaidia akina Lissu ma Heche wapate fedha kutoka kwa wafadhili wao
 
Kweli kabisa, yaani watu wameshalewa na POWER halafu unataka kuwaingilia kukanyaga nyaya zao... lazima ukamsalimie Mdude
 
Yaani wewe kwa akili zako za kuzaliwa unaamini ile ufufuo ni nyumba ya ibada ? Yaani watanganyika mmevurugwa kweli kweli, Allah atawafanyia wepesi Inshallah .
 
Kwa hiyo mtu yeyote anayeipinga serikali ni halali kutekwa na kuuawa? Mahakama ni za kazi gani sasa?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…