Ukiamua kuingia JF uwe tayari kuwa wazi na usionekane mtu anayetafuta huruma ya watu hapa. Me binafsi sina ugomvi na kikundi cha watu wa imani fulani kutaka nini kiwemo kwenye katiba ili mambo yao yaweze kwenda. Lakini tukumbuke katiba siyo ya dini fulani wala ya kikundi kidogo cha watu wanaohitaji matakwa yao yaingizwe ili waishi vizuri. Tukiuchukulia mchakato wa katiba kwa mtazamo huu hatuwezi kupata katiba ambayo italijenga Taifa, ila makundi ya watu. Kwa mfano, CCM wana mambo yao ambayo wangelipenda yawemo kwenye katiba ili waendelee kubakia madarani milele daima, CHADEMA nao wana yao ambayo wanapenda yaingie ili washike dola, CUF tayari walishawasilisha mswada wa katiba, siyo mawazo...no mswada wa katiba kwenye wizara ya Sheria na Katiba. Vivyo hivyo NCCR, Tadea, TLP, ADC, Wakatoliki, Waanglikana, Wasabato, AIC, TAG, Full gospel bible fellowship, waalimu, madaktari, wabunge, Wakulima, Wafugaji, Machinga, Mama lishe na kila aina ya kundi ambalo unalifahamu.
Sasa fikiria tukigawanyika katika makundi haya na kila kundi likaainisha mahitaji yake na ndiyo kikawa kilio chao....tutapata katiba ya aina gani? Hapo kutakuwa na katiba kweli au utakuwa utani tunaleta. Maana kwenye madai ya waislamu haujasema kuwa UMILIKI WA ARDHI, MATUMIZI MAZURI YA RASILIMALI, MADARAKA YA RAIS, TUME HURU YA UCHAGUZI, MUUNDO WA MUUNGANO, MUUNDO WA SERIKALI, SERIKALI IWE NA WIZARA NGAPI ZA KUDUMU NA UKOMO UWE WIZARA NGAPI, KAMA NI MUHIMU KUWA NA WAKUU WA WILAYA, DAS, RAS, NA WAKURUGENZI KATIKA ENEO MOJA LA KUFANYIA KAZI, VIPI HAKI ZA WATOTO, na mengine mengi ya msingi. Haya hayahusiani na kundi lolote miongoni mwa makundi ambayo nimeyataja hapo juu. Tukisema kila mmoja alizungumzie kundi lake, nani atazungumzia masuala ya kitaifa kama ambayo nimeyaainidha kwa herufi kubwa hapo juu. Hauoni kuwa tutakuwa hatulitendea haki taifa letu?
Hivi waislamu mkipewa mahakama ya kadhi ndiyo kero zenu zitaisha? Tanzania ikijiunga na OIC, muislamu wa Kagera na Kigoma vijijini wananufaika nini na OIC? Au ni ulaji wa Mashekh tu? Na najiuliza kama mtaruhusiwa kupumzika na kutokufanya kazi siku ya ijumaa kero zinakuwa zimeisha? Mbona mimi mkristu Jumapili napiga kazi kama kawaida? Dini ni mapokeo tu...hapo awali kabla ya waarabu na wazungu hatukuwa na Ijumaa, Jumamosi wala Jumapili, tulikuwa tunafanya kazi kila siku za juma na mambo yetu yalikuwa safi kuliko hata sasa ambapo tunajifanya watu wa Mungu ilihali hatuzifuati amri zake...nini dini bwana? Angalia nchi ambazo zimejipambanua kuwa za kidini, Iraq, Iran, Libya, na sasa Sudan kaskazini, Yemen, Syria, Afghanstan na nyingine nyingi, mambo siyo shwari huko...kila siku watu wanakufa kama mbwa...!
Nashauri...tuangalie na tuchangie mambo ya msingi kwenye tume ya katiba. Tukileta mambo ya udini, wengine wataleta mambo ya ukanda, tutafika mbali na kuleta mambo ya ukabila ya Ukijiji, Hatutabaki salama. Tuzungumzie mambo ambayo yanatufanya kuwa wamoja kama watanzania. Dini kila mtu ana yake na wengine hawana kabisa na wanaishi, tena maisha mazuri bila stress, dini zenyewe za sasa, wachungaji, mapadri na mashehe wamekuwa wachumia tumbo...hakuna lolote...
Mwalimu Nyerere alisema, najua utapinga kwa sababu wewe Muislamu...."Hakuna dhambi mbaya kama dhambi ya ubaguzi. Haiishi tu kusema wewe ni mkristo na mimi ni muislamu. Ukimaliza kusema mimi Mtanganyika na wewe Mzanzibar, tukifika pemba tutasema wewe Mpemba na mimi Muunguja, huku bara tutasema wewe wa Kaskazini na mimi wa kusini, Hata kwenye dini, leo unajiita muislamu na kuwaorganize waislamu mambo yenu...siku yakitokea ya kutokea, utasema wewe mshiha...na mimi msuni...wewe muislamu wa tabora na mimi wa mwanza....hadi makanisani....wote ni wakristo...lakini tutasema wewe mkatoliki, na mimi mlutheri...tutabaguana hadi kwenye familia zetu, na tukicheza na dhambi hii, tutaanza kubagua hadi viungo vya miili yetu....wewe mkono wa kushoto na wewe wa kulia." Dhambi ya ubaguzi siyo nzuri...
Maji yanatuunganisha wote, Maliasili zetu kama misitu, wanyama, madini, gesi, mafuta na makaa ya mawe yanatuunganisha wote kama watanzania. Tukipata katiba nzuri yenye mgawanyo mzuri wa madaraka, kupunguza madaraka ya rais, kuunda tume huru ya uchaguzi kuondoa wakuu wa wilaya, kutengeneza serikalil za majimbo, wote waislamu na wakristo tutafaidika na haya mambo...siyo habari za mahakama za kadhi, kuvaa hijabu, kuabudu...haya nimapokeo tu, yajadiliwe misikitini yaishie huko...sasa tukifikia kuweka kwamba sasa kuvaa hijabu ruksa...kwenye katiba, inakuwa nchi ya Kiislamu sasa. Au tuseme sasa Mahakama ya kadhi hiyo, serikali itagharamia....na wakristo wakidai yao....? Nani atasema serikali haina dini tena? Tuache hii mambo....Asante, naamini utakuwa umenielewa vyema.
TOGETHER WE CAN BRING THE CHANGES WE NEED...YES WE CAN...TUACHE UDINI...TANZANIA MBELE KAMA TAI...MENGINE YANAFUATA.....