hWaislamu wa Hamas wafanya ibada ya mazishi ya Kiongozi wao aliyeuawa Sinwar bila maiti yake kuwepo je kiislamu iko sawa? Kufanya ibada ya mazishi bila mwili kuwepo? Wanazika hewa au? Halafu cheki huyo imamu alivyochachamaa utafikiri anazika kweli
mu
View: https://youtu.be/pbK-wG0BtUQ?si=S2alI_a5UtX3l9r1
Inaitwa Swalaatul Ghaaib.
Inafaa. Na hilo waislamu wanalifanya
kwa kumuiga mtume Muhammad
صلى الله عليه وآله وسلم pale alipowaongoza waislamu wa Madina kumswalia mfalme Al Najaashiy wa Habasha (kwa sasa ni eneo zinapopatikana Ethiopia na Eritria ).
Mfalme huyu alikuwa mnaswara
( mkristo ) akasilimu lakini raia wake
wote walibaki kwenye dini yao ya unaswara.
Alipofariki hapakuwa na watu wa kumzika kiislamu katika nchi yake na mtume alipata wahyi (ufunuo kutoka kwa Allaah moja kwa moja au kupitia malaika Jibrilu ) Allaah akimjulisha kuwa mfalme Najaashiy amefariki ndipo mtume صلى الله عليه وآله وسلم akasema maneno maarufu kuwaambia maswahaba zake.
" إن أخاكم مات بأرض غيركم " = Hakika ndugu yenu ( muislamu mfalme Najaashiy ) amefia katika nchi ambayo siyo yenu ( Habasha au Ethiopia /Eritria haikuwa na waislamu zaidi ya mfalme Najaashiy peke yake ) basi mtume akawaongoza waislamu kumswalia mfalme Najaashiy Allaah amrehemu swala ya takbira nne maarufu ambayo ndiyo huswaliwa maiti wote wa kiislamu.
Kutokana na hadithi hiyo ndiyo wanachuoni wakafanya kuwa ni muongozo pale anapokufa mwislamu lakini ikashindikana kupata maiti yake kwa mfano kazama baharini na maiti haikupatikana, au kaungua moto, au kayeyuka kwenye tindikali au kafia katika nchi ambayo hakuna huko watu wa kumswalia , au kafa kwa magonjwa ya kuambukiza serikali ikaamrisha maiti hiyo izikwe na vyombo husika kwa taratibu zinazozuia kupeleka maambukizi kwa wengine basi waislamu watamswalia kwa utaratibu ule alioelekeza Mtume
صلى الله عليه وآله وسلم katika siku aliyokufa mfalme Najaashiy Allaah amrehemu.