Waislamu wa Hamas wafanya ibada ya mazishi ya Kiongozi wao aliyeuawa Sinwar bila maiti yake kuwepo. Je, kiislamu iko sawa?

Waislamu wa Hamas wafanya ibada ya mazishi ya Kiongozi wao aliyeuawa Sinwar bila maiti yake kuwepo. Je, kiislamu iko sawa?

Kwanini Sinwar amekuwa habari zaidi ya yule aliyekuwa kabla yake?maana kapokea kijiti kwa mda mfupi lakini wengi wameumia zaidi kufa kwake kuliko yule wa kabla yake
Ndiye mastermind wa shambulio la oktoba
 
Huyu jamaa alikuwa ndio kama Moyo wa HAMAS na alikuwa anapanga mipango akiwa mbali....aliishi mpk Qatar kwa miaka kadhaa huku akitekeleza matukio ya kigaidi
Labda kuongezea huyo ndio alikuwa head of intelligence operation za hamas, kwa muda mrefu alikuwa akiwawezea israel, walimtafuta bila mafanikio.
Until alipochaguliwa kuongoza kundi hilo, niliwaambia watu hapa ilikuwa ni tactical mistake ya hamas kumu expose huyu bwana, now israel watajua mienendo yake

Na kweli haijachukua time
 
Ni kama wamechoka, wamekata tamaa, pengine wanajuta hata nchi yao kuwa hapo.
 
hWaislamu wa Hamas wafanya ibada ya mazishi ya Kiongozi wao aliyeuawa Sinwar bila maiti yake kuwepo je kiislamu iko sawa? Kufanya ibada ya mazishi bila mwili kuwepo? Wanazika hewa au? Halafu cheki huyo imamu alivyochachamaa utafikiri anazika kweli

mu
View: https://youtu.be/pbK-wG0BtUQ?si=S2alI_a5UtX3l9r1

Inaitwa Swalaatul Ghaaib.
Inafaa. Na hilo waislamu wanalifanya
kwa kumuiga mtume Muhammad
صلى الله عليه وآله وسلم pale alipowaongoza waislamu wa Madina kumswalia mfalme Al Najaashiy wa Habasha (kwa sasa ni eneo zinapopatikana Ethiopia na Eritria ).
Mfalme huyu alikuwa mnaswara
( mkristo ) akasilimu lakini raia wake
wote walibaki kwenye dini yao ya unaswara.
Alipofariki hapakuwa na watu wa kumzika kiislamu katika nchi yake na mtume alipata wahyi (ufunuo kutoka kwa Allaah moja kwa moja au kupitia malaika Jibrilu ) Allaah akimjulisha kuwa mfalme Najaashiy amefariki ndipo mtume صلى الله عليه وآله وسلم akasema maneno maarufu kuwaambia maswahaba zake.
" إن أخاكم مات بأرض غيركم " = Hakika ndugu yenu ( muislamu mfalme Najaashiy ) amefia katika nchi ambayo siyo yenu ( Habasha au Ethiopia /Eritria haikuwa na waislamu zaidi ya mfalme Najaashiy peke yake ) basi mtume akawaongoza waislamu kumswalia mfalme Najaashiy Allaah amrehemu swala ya takbira nne maarufu ambayo ndiyo huswaliwa maiti wote wa kiislamu.
Kutokana na hadithi hiyo ndiyo wanachuoni wakafanya kuwa ni muongozo pale anapokufa mwislamu lakini ikashindikana kupata maiti yake kwa mfano kazama baharini na maiti haikupatikana, au kaungua moto, au kayeyuka kwenye tindikali au kafia katika nchi ambayo hakuna huko watu wa kumswalia , au kafa kwa magonjwa ya kuambukiza serikali ikaamrisha maiti hiyo izikwe na vyombo husika kwa taratibu zinazozuia kupeleka maambukizi kwa wengine basi waislamu watamswalia kwa utaratibu ule alioelekeza Mtume
صلى الله عليه وآله وسلم katika siku aliyokufa mfalme Najaashiy Allaah amrehemu.
 
Nakukumbusha mpwa alipokaa kwenye kijisofa chake akataka kutungua drone na gongo ila Sina Wali kwa utapeli kiboko
Halafu ili nyumba na sofa sio vyake,mwenye nyumba na sofa alikimbia vita akaacha nyumba tupu Sunwar akaenda kuvamia,mwenye nyumba anataka nyumba na kochi lake.
 
Kwahiyo alikuwa na nguvu zaidi kuliko viongozi wake ndani ya Hamas?
Inasemakana alikuwa anapenda mabavu kuliko diplomacy ndio maana inner circle ya Hamas walikuwa wanamchukia,na kuna habari kuwa ni yeye mwenyewe kwa matakwa yake bila kushirikisha viongozi wenzake waliokuwa nje ndio aliamuru mashambulizi ya 7th October.
 
Labda kuongezea huyo ndio alikuwa head of intelligence operation za hamas, kwa muda mrefu alikuwa akiwawezea israel, walimtafuta bila mafanikio.
Until alipochaguliwa kuongoza kundi hilo, niliwaambia watu hapa ilikuwa ni tactical mistake ya hamas kumu expose huyu bwana, now israel watajua mienendo yake

Na kweli haijachukua time
Huyo Israel walikuwa wanamfahamu sana,alishafungwa jela za Israel almost 20yrs.
 
Back
Top Bottom