Lax
JF-Expert Member
- Feb 10, 2022
- 4,740
- 7,179
Kuna mtu mmoja ile siku ya kwanza ilivofika kwenye maswali, alisema yeye hana swali ila ana ombi kwamba kwa lecture zinazofata next day kuwe na mkalimani ili watanzania wengi wanufaike maana english wengi imepita pembeni.Dr. Zakir Naik hakutenda haki, wengi walikosa kufaidika vilivyo na mihadhara yake kutokana na changamoto ya lugha za kimataifa inayoikabili umma mpana wa waTanzania.
ZAkir akauliza wangapi wanaelewa english watu wakanyoosha mikono wengi wengi akamwambia muuliza swali you see, watu wanaelewa na hawezi poteza muda wa mkalimani maana kama lecture ni ya masaa 3 maana yake itakua masaa 6.
NIkaona Zakir naik pamoja na waandaaji wote hawakujipanga. Maana naamini wale waloenda siku ya kwanza walishajichuja wanaoelewa lugha(English) ndo walienda.
Language ni mzozo.
Hapa hapa nichukue fursa ya kuchangia hoja ya Abu Miqdad
mimi sina tatizo na uyo yaeleza ila waumini wengi wanakubwa na tatizo la lugha na hasa katika uislam kwasababu ya kuibakisha katika kiarabu kama lugha kuu,Swala katufundisha Mtume (Swala na Salamu ziwe juu yake). Na tunaswali kama alivyotufundisha, nyinyi mnaojidai ni Quranists (Quranists ni makafiri) mko mbali mno na Quran. Quran imeamrisha kumfuata Mtume (Swala na Salamu ziwe juu yake) nyinyi mnakataa kabisa asifuatwe Mtume (Swala na Salamu ziwe juu yake).
Sisi tunamshukuru Allah kwa Neema tukufu mno kabisa ya Uislam na Sunnah, tunamshukuru Allah aliyeiteremsha 'Ibadah tukufu ya Swala na akmfunulia mafundisho ya Swala Mtume wake (Swala na Salamu ziwe juu yake) na Mtume akatufikishia. Na Waislam wote Duniani tukawajibika kuswali kama alivyoswali Mtume. Leo nikienda Upareni au Helsinki, Finland, nikakuta Waislam basi Swala ni ile ile, Muislam hata akitoka Switzerland au China anaweza kuja Tanzania na akawaswalisha ndugu zake hata kama hazijui lugha zao mama, Alhamdulillah.
Halafu maneno yanayofundishwa katika Swala maana yake hufundishwa, ni wewe ndio hujui. Na Dua zilizokuja kutoka kwa Mtume pia hufundishwa hata maana zake na watu wanazihifadhi na wanaelewa hata kama hawawezi kuzungumza kiarabu.
Na katika Sijda ambapo imehimizwa kukithirisha kuomba Dua wasiojua kiarabu wanaweza kuomba kwa lugha wanazozijua wao wakamuomba Allah haja zao mbalimbali kwa sababu mja anakuwa karibu zaidi na Mola wake akiwa katika Sijda.
Na nje ya Swala ndio kabisa mtu anaweza kumuomba Allah kwa lugha yoyote ile.
Namuomba Allah anifishe katika Uislam na Sunnah ya Mtume (Swala na Salamu ziwe juu yake).
Allah akuongoze.
Kama ilivo sifa kwamba muumini anaweza toka finland akaenda kuongoza ibada thailand. Yapasa kuasifa vilevile kua na mkakati wa waumini kufahamu kiarabu ili kuelewa kwa urahisi maandiko
Hata huyu Zakir Naik alienda kenya kama sio uganda alikua na topic hiyo ya waumini kujifunza kiarabu ( na faida za kufanya hivo)
Kwa imani zingine ambazo watu wamesha translate moja kwa moja kwenda lugha mbalimbali(yani mfano budhism ipo kwa kiswahili moja kwa moja full) hata huko walobobea katika imani hizo wanawashauri waumini kujifunza lugha original ya hiyo imani na kuisoma katika lugha original ilikuelewa kwa ufasaha zaidi misamiati pamoja na muktadha kwa ujumla
My opinion: viongozi pamoja na waumini wakae kuangalia wanatatuaje tatizo hilo