Waislamu wazindua Jukwaa la KATIBA

Waislamu wazindua Jukwaa la KATIBA

JE HAYA YAKIPATIKANA NDIO UISLAMU UMEKAMILIKA?OIC NI KAMA BAKWATA LAKINI YA KIMATAIFA,JE MNAJUA NANI KIUNDA?
Malengo ya jukwaa la katiba.

[1] Tanzania ijiunge na OIC

[2] Tanzania ianzishe mahakama ya Kadhi.

[3] Tanzania ifunge ubalozi wa Vatican.

[4] Tanzania ianzishe mfumo wa kugawana madaraka nusu kwa nusu ie baraza la mawaziri likiwa na mawaziri 20 kumi wakristo kumi waislamu
 
Mimi nadhani jambo la msingi ambalo tungejikita nalo ni umhimu wa watanzania, zikiwemo na taasisi za dini, kutoa maoni juu ya Katiba mpya. Kwa tunaopenda mabadiliko, kuzinduliwa kwa jukwaa hilo ni mhimu na kumekuja katika wakati muafaka. Ila ni vizuri tungejiepusha na matamshi ambayo yanaweza kutonesha hisia za kidini miongoni mwetu na kutupeleka katika jazba na hatimaye tukaacha kujadili kiini cha hoja (mabadiliko ya katiba) na badala yake tukaishia kulumbana kwa kuegemea katika tofauti zetu za kidini.

Suala la Katiba mpya ni suala la kitaifa. Mafanikio yake yanategemea kuwepo maoni mapana zaidi yakihusisha watu wa jamii, vikundi na fikra tofauti. Tujifunze kustahimili fikra za wenzetu hata kama kwa uelewa na mtizamo wetu tunaona kuwa si sahihi. Tusaidiane kupanuana mawazo kwa lugha ya staha katika tofauti zetu. Tunapochangia hoja hata kama ni wazi imetolewa na jamii au kundi fulani la kijamii tujadili hoja kama hoja na sio mtu au kundi lililotoa hoaj. Tukifanya hivyo, FORUM yetu itakuwa na mchango mkubwa sana katika kuelimisha wananchi juu ya mabadiliko ya Katiba na kukusnya maoni ya watu
 
kwahili lakongamano kwa waislam kuhusukatiba mimi naunga mkono wasiwasi yangu ni matekelezo kwahayo watakayoyataka yawepo kwenyekatiba .isijeikawakamamiaka hamsini iliopita .
 
Hakutakuwa na jipya huko sana sana mfumoislamu,OIC na mahakama ya kadhi,jamani udini ushapitwa na wakati,katiba mpya iwe ya kuipeleka mbele TZ yetu.
 
sijui km tutaweza kwenda bila kuaminiana a kuwajibika.Kila kiongozi ajue kuwa anajukumu la kuhakikisha na haki za watu wa dini zingine,kabila zingine etc na hao watu wawe na ridhiko kuwa wanatendewa haki na kutoa ushirikiano.Imagine tuwe na wakristu nunu waislam nusu, then tanganyika nusu+zanzibar nusu.Then ptahitajika waislam wa bara wasiwepo ili kuweza beba zanzibar au zanzibar walazimishwe walete nao nusu waislam na nusu wakristu,Hapo hapo na dini nyingine nazo zipate wao kotekote.
 
Day dreaming!

Ndugu zangu, katika mjadala unaohusu suala zito kama hili hatutegemei kwamba watu wote watakuwa na mawazo sawa katika kila kitu. Pia hatutegemei kwamba kila kitakachosemwa kitakuwa sehemu ya hiyo Katiba mpya. Lazima kuna mahali tutafika kukubaliana kutokubaliana. Mhimu hapa ni kwamba kila mtu, maslahi ya kijamii, kisiasa na kidini wana haki sawa ya kuchangia katika mchakato wa Katiba mpya. Hamna haja ya kuzalauriana au kufikiriana vibaya. Sio kila mazo litakalotolewa litakuwa baya au zuri.

Kingine cha mhimu kuzingatia ni kwamba kuchangia katika uundwaji wa Katiba mpya hakutegemei sana ujuzi au umiliki wa taaluma katika fani fulani. Mkulima kule Kiponzelo Iringa, Mfugaji kule Meru Arusha, mfanyabiashara pale mtaa wa Kongo, padri, mchungaji, sheikh, imamu na manju wa dini ya Mrungu wa Kathanga wote wana haki sawa ya kuchangia japo mawazo yao kuna sehemu yatapingana.

Kwa kujua hilo ndio maana Sheria ya Mchakato wa Katiba imeweka mipaka baadhi ya masuala ambayo ni nguzo mhimu ya Taifa la Tanzania. Kwa mfano, haturuhusiwa kujadili kama Tanzania iwe dola ya kisekula au kidini. Haturuhusiwi kujadili kama tusiwe na haki za binaadamu katika Katiba au la. Haturuhusiwi kujadili uwepo wa Muungano wa Tanzania kama vile tusivyoruhusiwa kujadili kama Bunge, Mahakama na Serikali Kuu viwemo au visiwemo katika Katiba mpya.

Ningewashauri watanzania wenzangu tusianze kutiliana shaka na kukatishana tamaa kabla hata mjadala haujaanza. Muaje kila mtu na kila kikundi kitoe maoni. Kama waislamu wameanzisha chombo cha kuhamasisha mjadala wa Katiba ili kutoa maoni ya mambo yanayo wahusu kama watanzania wamefanya vema na wanapaswa kuungwa mkono na kupewa moyo badala ya kukatishwa tamaa. Nadhani na taasisi nyingine za kidini na kijamii zinautaratibu wake wa kujaribu kuingiza maslahi yao ya kijamii katika Katiba mpya
 
Malengo ya jukwaa la katiba.

[1] Tanzania ijiunge na OIC

[2] Tanzania ianzishe mahakama ya Kadhi.

[3] Tanzania ifunge ubalozi wa Vatican.

[4] Tanzania ianzishe mfumo wa kugawana madaraka nusu kwa nusu ie baraza la mawaziri likiwa na mawaziri 20 kumi wakristo kumi waislamu

usiliangalie hl kwa tanz bara tu bali ifanyike na tz zanzibar. Upo hapo" pia wakumbuke kufunga balozi nch kama oman, saudia n.k na si vatican pekee.
 
Nadhani hata JK alishawahi kuwahimiza viongozi wa dini pamoja na waumini wao kutoa mchango wao kwenye katiba mpya ila wasiingize mambo ya dini maana yataleta mafarakano...sasa wenzetu sijui wanatumia viungo gani vya mwili kufikiria!?

ndugu unaweza kuwa na macho kisha usitambue unachokitazama. Sasa hy mahakama ya kadhi wasifikiri ndio shuluhusho. Je watamudu uendeshaji wake? Wajaribu kufikiria tanzania sio saudia. TAFAKARI CHUKUA HATUA"
 
Haya masuala ya kuwepo au kutokuwepo mahakama za kadhi, kuwepo au kutokuwepo mahakama za kimila za kutatua migogoro iliyoratibiwa na sheria za kimila ni masuala yanayojadilika wala yasitupe tabu. Ndio maana yamekuwa yakijadiliwa Bungeni na mahala pengine hata kabla hatujaamua kuwa na Katiba mpya. Pia katika nchi nyingine zinazo fanana fanana na Tanzania suala la Mahakama ya Kadhi wameliingiza katika Katiba. Kama Tanzania litastahili pia kuwemo katika Katiba ni suala ambalo litaamuliwa na hoja mbali mbali zitakazojitokeza katika mjadala wa Katiba mpya.

Hata masuala ya nani atazigharamia mahakama hizo, nani ataziendesha, yanazungumzika na kujadilika hatuna haja ya kudhalau hoja bali tunaweza kupinga hoja kwa hoja na hatimaye wote tukasafiri na kufika pamoja. "Tusiogope mawimbi, ndio mwendo wa ngalawa". Mungu ametuumba tukiwa watanzania na akatuweka katika nchi ya Tanzania ambayo ina mchanganyiko na mkusanyiko wa imani, mila na itikadi mbalimbali zinazotofautiana. Inabidi tuheshimu ukweli huo wa kihistoria. Ungezaliwa Uingereza au Saudi Arabia tofauti kama hizi hazingekuwa na maana yoyote.

Tujifunze kuishi katika imani kwamba watanzania wote ni sawa na tuna haki sawa ya kuishi pamoja licha ya tofauti zetu.
 
.....

Kwa hakika hasa hii ni picha ndogo ya picha kubwa ya kazi ambazo bakwata ilitakiwa kufanya. Wengi wanawasiwasi kua waislam kama wataachiwa kupanga mambo yao wanaweza kua tishio kwa jamii nyingine ingawaje hawaelezi hasa kwanini wana wasiwasi huo.
....Kuchoma makanisa na kutisha wabara waishio visiwani , kulazimisha nchi iwape nguvu ya dola ktk Mahakama ya kadhi(ili kumbana muislam aliyeamua kutokuwa mmoja wa mabo hayo, mjane asiye mmoja wao) ni zaidi ya mambo yao...unless una reverse logic hutaona nini kinaleta shida hapa.

By the way,hakuna mahali muislam nashindwa kamilisha nguzo 5 za dini yake,+sunna.hayo mengine ni mafunzo ya dini yawe convincing enough kwa mfuasi kufuata sheria bila shuruti, na itakapofikia kahitaji shuruti basi si muuni tena.Kuendelea tumia dola mdhibiti ni makosa ambayo hata religious police wa Saudi Arabia wameanza kuwa embarassing to the community,that has always tried to perfect their life by more religious adherence with no avail.

Nature ya uislam haihamaisishi kumfanyia uadui mtu mwengine yoyote. Lakin mpaka waislam watakapopewa nafasi na wao wenyewe watakapo jipanga na kupuuza tofauti zao ndogondogo ambazo hazina msingi watakua ktk position ya kulionyesha hilo kama reality.
......
 
very true ndo wanachotaka

-Mbona haijaanzia zanzibar kuwa na hiyo ratio 20/20?

-Mbona kufunga ubalozi wa Vatican then wao watakosa kisingizio cha kuhimiza kujiunga na OIC km wanavyotumia?

-Sasa serikali itaweza anzisha hiyo mahakama kwa staili ya kiisalama, mbona itakuwa km kuiomba serikali kuchinja mnyaka atakayeliwa na muislam.Itakuwa halai kweli?

>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>.
-then kuna wataodai kuwa pawe na ubalozi kwa dalai lama-buddhist

-india watahitaji special kwa ajili ya jimbo linalobeba mto wao.

-wayahudi na wakristu wa madhehebu kilokole nao watadai ubalozi wa taifa la kiyahudi na wana ushahidi wa ushirikiano wenye faida kubwa kiulinzi, kisayansi na kijensi, tofauti na upande wa pili.

-kuna watakotaka ubalozi na uanachama na wachawi wakuu wa Nigeria na ubalozi maalumu.

-Wala mirungi watapenda kuwa na ubalozi maalumu na somalia namombasa....etc....teh teh.

-washia watapenda ubalozi wa 2 kwa iran.
 
At least hiyo ni hatua moja sahihi ya kuelekea right direction. Hili lilitakiwa lifanyike mapema na sio ktk kujadili katiba tu ispokua kujadili mengi ambayo waislam yanawahusu kama waislam na yanayowahusu kama raia wa kawaida.

Kwa hakika hasa hii ni picha ndogo ya picha kubwa ya kazi ambazo bakwata ilitakiwa kufanya. Wengi wanawasiwasi kua waislam kama wataachiwa kupanga mambo yao wanaweza kua tishio kwa jamii nyingine ingawaje hawaelezi hasa kwanini wana wasiwasi huo.

Nature ya uislam haihamaisishi kumfanyia uadui mtu mwengine yoyote. Lakin mpaka waislam watakapopewa nafasi na wao wenyewe watakapo jipanga na kupuuza tofauti zao ndogondogo ambazo hazina msingi watakua ktk position ya kulionyesha hilo kama reality.

Wakati umefika Bakwata ifanye kazi zake kwa ufanisi na kila mtu apewe jukumu linalostahili na vigezo vinavyostahili. Kwa mfano ni muhimu ktk kujadili swala la katiba wakapatikana wataalam ambao wanaifahamu vizuri sheria ya nchi na wanafahamu vizuri sheria let say ya kiislam. Hapo wataweza kufanya balance kua kitu wanachojaribu kukiproposal kinaweza kweli kikafanyiwa kazi ktk secular government?
Vinginevyo busara itumike ktk kuyaadress marekibisho yanaykusudiwa ktk njia ambazo yanaweza kupatiwa ufumbuzi. Hao yote ni magumu kufanyika bila ya elimu ya kutosha. Jaribuni kuwahusisha wataalam mbalimbali ili juhudi hizi muhimu zisipotee bure. Good luck

May be!
Lakini katika uzoefu wangu katika mambo ya aina hii nimeona makongamano haya na midahalo hii ikiishia kuzindua matamko ya ajabu ajabu ambayo yanapandikiza chuki katika jamii. Sitegemei jipya. Vinginevyo natarajia yaleyale ya "Tunaonewa, hatupewi haki, mbona wenzetu pale.......Hapa tu nimeshasoma mwingine anataka waende ikulu ili wawe wamefanya kama walivyofanya wale....ligi zisizo na msingi kabisa.... ukisikia wamesema a wewe sema aaaaaaaaaaaaaa!... mashindano ya ajabu kabisa.
Ningefurahi Kama this time angalau nitasikia nguvu ya hoja. Hoja zinazoonyesha watu wenye uchungu na mabadiliko ya nchi. Na siyo uimarishaji wa matengano ya kidini! Tayari naona watatoka na tamko la waislamu wanataka nini kwenye katiba mpya!.... wataelimisha jamii ya waislamu kuhusu elimu ya katiba ya sasa!......Nilitegemea watatoka na kuelimisha wananchi juu ya katiba wao wamekumbuka waislamu!

Labda tungoje tuone...lakini on my side sitegemei mpya. Ila nitafurahi kuona mwamko unaoonyesha ukomavu wa kifikra na hoja za msingi bila kusahau madai yenye mashiko (data).That is the way the grown ups handles matters in concern! Thanks Folks.
 
....Kuchoma makanisa na kutisha wabara waishio visiwani , kulazimisha nchi iwape nguvu ya dola ktk Mahakama ya kadhi(ili kumbana muislam aliyeamua kutokuwa mmoja wa mabo hayo, mjane asiye mmoja wao) ni zaidi ya mambo yao...unless una reverse logic hutaona nini kinaleta shida hapa.

By the way,hakuna mahali muislam nashindwa kamilisha nguzo 5 za dini yake,+sunna.hayo mengine ni mafunzo ya dini yawe convincing enough kwa mfuasi kufuata sheria bila shuruti, na itakapofikia kahitaji shuruti basi si muuni tena.Kuendelea tumia dola mdhibiti ni makosa ambayo hata religious police wa Saudi Arabia wameanza kuwa embarassing to the community,that has always tried to perfect their life by more religious adherence with no avail.

Japo mimi si mtaalamu wa dini, ninaamini kabisa hamna dini yoyote inayofundisha waumini wake kwenda kubomoa nyumba za inada wa waumini wa dini nyingine. Waliohusika na ubomoaji wa makanisa wamefanya hivyo kwa kusukumwa na misukumo mingine nje ya imani ya dini ya kiislamu. Yaweza kuwa msukumo wa kisiasa, kikabila, kidini au ubinafsi kwa ujuma.

Makanisa Zanzibar yamekuwepo kwa miaka na waislamu wamekuwepo kwa miaka iweje leo hii tabia ya kujoma makanisa izuke. Nimewasikia wasomi mbalimbali wa kiislamu wakinukuliwa na vyombo mbalimabli vya habari wakibainisha kwamba Kuraani inakataza kufanya uharibifu katika misikiti, makanisa na masinagogi ambamo jina la mungu linatamkwa kwa wingi.

Mimi ningependa kuona vyombo vya dola vinachunguza kwa kina waliohusika katika uharibifu huo mkubwa na kuwachukulia hatua inayostahili.
 
Japo mimi si mtaalamu wa dini, ninaamini kabisa hamna dini yoyote inayofundisha waumini wake kwenda kubomoa nyumba za inada wa waumini wa dini nyingine. Waliohusika na ubomoaji wa makanisa wamefanya hivyo kwa kusukumwa na misukumo mingine nje ya imani ya dini ya kiislamu.

si suala alinalohitaji mtu kuwa na elimu kubwa ili aone.Makanisa yanachomwa dunia nzima na waislam kila wakipandisha hasira.Ni njia imetumika ubana Ukristu kwa miaka.Huwa nchi za kiiislam km Egypt wana sheria zinahitaji kibali ,kwa ujenzi au hata kufany marekebisho ktk kanisa....sasa whats happen hawa jamaa wakipandisha hasira, huwa wanachoma halafu upelelezi unafanyika na hao wahalifu wa kidini huwa hawapewi adhabu kabisa au awanapata kidogo sana,kutokana na watu kuja na sababu kuwa walikuwa ni wahuni ,na mara nyingine mashinikizo ya wenye siasa kali kuwa watu wao waachiwe huru otherwise watafanya mauaji na vitisho vingine vya namna hiyo.

Pia ,ujue kuwa uislam una mafundisho mengi yanayohimiza kuangamiza wasio waislam,sasa njia za kunagamiza ni nyingi.Na usitegemee kukuta mambo yote yakawa yameandikwa specifically.Km mabomu wanayotumia hayakuandikwa ila mauaji yameandikwa.
Yaweza kuwa msukumo wa kisiasa, kikabila, kidini au ubinafsi kwa ujuma.

Sasa mbona unakubali tena, kuwa ni sababuza kidini...Pia uje wanauamsho wamesajiliwa km taasisi ya kidini.
Makanisa Zanzibar yamekuwepo kwa miaka na waislamu wamekuwepo kwa miaka iweje leo hii tabia ya kujoma makanisa izuke. Nimewasikia wasomi mbalimbali wa kiislamu wakinukuliwa na vyombo mbalimabli vya habari wakibainisha kwamba Kuraani inakataza kufanya uharibifu katika misikiti, makanisa na masinagogi ambamo jina la mungu linatamkwa kwa wingi.

Mimi ningependa kuona vyombo vya dola vinachunguza kwa kina waliohusika katika uharibifu huo mkubwa na kuwachukulia hatua inayostahili.

Utasikia hizo story for years na bado haitoisha sikia uchomaji ,mauaji etc...Waislam hawaruhusiwi shuhudia against muislam mwenzao.Uliona pakistan kwa nini walimhifadhi osama na sasa wanawahukumu waliosaidia kuuwa kwake.Si walikuwa wakijifanya wanasaidia war on terror?

Hao wanaosema hivyo, wana maeneo at least wakiwa wenyewe wanapogeza hilo na kuwatakia mwendo mwema.

Sidhani km sehemu litajwapo jina la Mungu kunazuia muislam kupaharibu,haiwezekani dunia nzima waislam wasiwe wanajua hayo wanayosema hao wasomi.Wao wapo kulinda dini kwa loloto...ama kwa uongo mtakatifu() au hata mauaji ...
{unaopoozea makafir}.

Pia mafundisho yanayopuuza maandiko na mafundisho ya dini nyingine yanapunguzia wafuasi wao,heshima mbele ya wengine, wakiongezewa na mahubiri km yajulikanavyo juu ya dini nyingine si haba kuona waislam wakiwa waaribifu wa maisha ya wengine.

Pia ukiweza soma Quran, na hadith kwa lugha uijuayo halafu uone kama wakuambiacho ni kweli au hata hao wachomaji uone ni kwanini wanjiamini kufanya wafanyalo.
 
si suala alinalohitaji mtu kuwa na elimu kubwa ili aone.Makanisa yanachomwa dunia nzima na waislam kila wakipandisha hasira.Ni njia imetumika ubana Ukristu kwa miaka.Huwa nchi za kiiislam km Egypt wana sheria zinahitaji kibali ,kwa ujenzi au hata kufany marekebisho ktk kanisa....sasa whats happen hawa jamaa wakipandisha hasira, huwa wanachoma halafu upelelezi unafanyika na hao wahalifu wa kidini huwa hawapewi adhabu kabisa au awanapata kidogo sana,kutokana na watu kuja na sababu kuwa walikuwa ni wahuni ,na mara nyingine mashinikizo ya wenye siasa kali kuwa watu wao waachiwe huru otherwise watafanya mauaji na vitisho vingine vya namna hiyo.

Pia ,ujue kuwa uislam una mafundisho mengi yanayohimiza kuangamiza wasio waislam,sasa njia za kunagamiza ni nyingi.Na usitegemee kukuta mambo yote yakawa yameandikwa specifically.Km mabomu wanayotumia hayakuandikwa ila mauaji yameandikwa.

Sasa mbona unakubali tena, kuwa ni sababuza kidini...Pia uje wanauamsho wamesajiliwa km taasisi ya kidini.

Utasikia hizo story for years na bado haitoisha sikia uchomaji ,mauaji etc...Waislam hawaruhusiwi shuhudia against muislam mwenzao.Uliona pakistan kwa nini walimhifadhi osama na sasa wanawahukumu waliosaidia kuuwa kwake.Si walikuwa wakijifanya wanasaidia war on terror?

Hao wanaosema hivyo, wana maeneo at least wakiwa wenyewe wanapogeza hilo na kuwatakia mwendo mwema.

Sidhani km sehemu litajwapo jina la Mungu kunazuia muislam kupaharibu,haiwezekani dunia nzima waislam wasiwe wanajua hayo wanayosema hao wasomi.Wao wapo kulinda dini kwa loloto...ama kwa uongo mtakatifu() au hata mauaji ...
{unaopoozea makafir}.

Pia mafundisho yanayopuuza maandiko na mafundisho ya dini nyingine yanapunguzia wafuasi wao,heshima mbele ya wengine, wakiongezewa na mahubiri km yajulikanavyo juu ya dini nyingine si haba kuona waislam wakiwa waaribifu wa maisha ya wengine.

Pia ukiweza soma Quran, na hadith kwa lugha uijuayo halafu uone kama wakuambiacho ni kweli au hata hao wachomaji uone ni kwanini wanjiamini kufanya wafanyalo.

Ndugu yangu najua umekereka na yaliyofanyika Zanzibar kama mimi na watu wengine walivyokerwa. Pamoja na hivyo, jaribu kushuka chini kidogo na kupunguza hasira ili tujadili sote tukiwa neutral.

Kuna haja ya kutofautisha uislamu na waislamu kama ilivyo kwa ukristo na wakristo. Sina haja ya kutoa mifano ya namna dini hizi zilivyotumika ndivyo sivyo katika kuhalalisha maslahi fulani ya kiuchumi au kisiasa. Nikupe mfano wa namna wafanyabiashara ya utumwa walivyotumia ndivyo sivyo mafundisho ya ukristo kuhalalisha biashara ya utumwa. Walitumia habari ya watoto wa nabii Nuhu kuhalalisha utumwa wa milele wa waafrika kwa wazungu na waasia. Walisema kwamba yule Hamu aliyemchungulia baba yake akiwa uchi na kulaaniwa ni chanzo cha kizazi cha waafrika na Shamu waasia wakati yule mmoja aliyebaki wazungu. Wakahitimisha kwa kusema kwamba kuna uhalali wa kihistoria wa waafrika kuwa watumwa wa wazungu na waasia kutokana na laana ya Mungu. Mtu akilitizama hili kwa hasira tu anaweza kuhusisha mafundisho ya biblia na utumwa kitu ambacho hakiwezi kupikika pamoja. Ni hivyo hivyo waarabu walitumia mafundisho ya kiislamu isivyo kuhalalisha utumwa wa waafrika kwa dhana kwamba ni makafiri.

Tunachoweza kujifunza hapo ni kwamba kuwepo kwa watu wanaotumia uislamu au ukristo wao kufanya uhalifu hakumaanishi kwamba hayo ndiyo mafundisho ya dini husika.

Suala la kuchunguza ni la msingi maana misingi ya haki na uadilifu inataka mtu asihesabiwe mkosaji mpaka mahakama imuone hivyo. Tumewasikia waislamu Zanzibar wakikanusha kuhusika na uchomaji wa makanisa na kusisitiza kwamba hilo lilifanywa na watu wengine kwa maslahi yao. Inapotokea kama hivyo tutajuaje nani anasema ukweli bila uchunguzi huru kufanyika na hatimaye wahusika kufikishwa katika vyombo vinavyo husika? Kuna njia gani ya mkato tunayoweza kutumia bila kuathiri haki za wengine?

Jambo la msingi ambalo lingejadiliwa sambamba na kufanya uchunguzi na kuchukua hatua zinazostahili ni kuweka mikakati ya kuzuia tatizo kama hilo kutokea tena maana kinga no bora kuliko tiba.
 
Issue ni kwamba unachojaribu sema hapa ndicho wao wanchokielewa na kukiamini?Ingekuwa ndivyo basi pasingekuwa na pattern moja, ambayo inatuweka njia panda ktk kuwaamini,kimatendo, kwa maneno na hata kifikra.
 
Ni vigumu kuingia katika imani yao, lakini pia ni ukweli kwamba japo wanaweza kuwepo baadhi yao ambao waka tayari kupotosha mafundisho ya dini kwa maslahi yao, msimamo mzima wa dini zetu haungi mkono vurugu na uharibifu mkubwa uliofanyika. Nimepata kuwasikia viongozi wa dini ya kiislamu wakinukuu vifungu katika msahafu vinavyokataza kwa wazi vitendo kama hivyo. Sioni kwa hali hiyo ni kwa nini tusiwaamini na kuruhusu uchunguzi huru ufanyike ili watakaobainika kuhusika waadhibiwe sio kama waislamu bali kama wahalifu wa kawaida. Maana, uhalifu haina dini hata kama utafanyika kwa mwanvuli wa dini.
 
Back
Top Bottom