Waislamu wazindua Jukwaa la KATIBA

Sasa hao baadhi wanakuwa zaidi ktk ukweli wa dini yao...

Pia ungechukua Muda kuusoma huo msahafu ungepata vifungu vingine vinavyowasupport hao uamsho....sijui utawakataza vipi kuvitumia hivyo vifungu hatari zaidi?Kwao vyote ni sehemu za ibada..nadhani hao walionukuu vifungu vya makatazo hawana vingi na vyenye Nguvu kuliko vya walifanya uharibifu.

Kwa taarifa yako haohao ukiwabana na kuwapa mistari watakuambia kitu tofauti....kuwa haya hizo ni kwa kazi maalumu na mazingira maalum...cha kujiuliza ni kuwa Hayo hayakuwa mazingira maulumu?Sasa shangaa watakavyowachomoa kwa sababu mbalimbali...kwani Basaleh..kashikwa mara ngapi na polisi kwa uchechezi na bado yupo mitaani anachochea bado?

Km unataka pata watu pious ktk dini yao nadhani mzee Mwinyi atakuwa ktk yao.Ila tazama challenges anazopata kupigwa makofi, km upo ktk meneo ya uswazi basi pitia vijiwe vya magazeti halafu usikie shutuma apatazo kila anapoandikwa akikemea hayo. Si viongozi wengi wanaweza kemea live bila kuogopa kuuwasha moto wa kidini.

Haiwezekani waislam dunia nzima wakafanana hivyo kitabia,hata sehemu walipobanwa na dola, km hakuna kitu kilichomo ktk kiini cha mafundisho yao.Uslam ni Dini, uamaduni, na mfumo wakisiasa(Mfumo mzima wa maisha).So lazima dini ipate power ili ianze kukimbizana na jitihada za kuunda taifa lake.Ni vigumu kuwa na uislam halafu ukainyima dini mamlaka.Maisha hayata kuwa as usual....
 



Mimi naona sio busara kuhitimisha hivyo kwa hisia bila kuwa na ushahidi kamili. Kwa kadili ninavyoujua uislamu hauungi mkono mambo hayo. Masuala ya vijiwe vya uswazi hayana uhusiano wowote na mambo ya dini. Sio ajabu stories zinazozungumziwa katika vijiwa vya uswasi Dar Es Salaam hayana tofauti na vijiwe vya uswazi vya majijiji na miji mikubwa mingine duniani. Kijana anapokaa kijiweni na wenzie hakai kama muislamu au mkristo bali ni kama kijana mwingine yeyote.

Kwamba uislamu ni utamaduni, siasa na jamii ni suala amablo linaenda zaidi katika falsafa ya dini. Ni suala ambalo linahusu dini karibu zote. Ukumbuke kabla hatujaingia katika mapinduzi ya kisiasa huko ulaya ya magharibi (political revolution) yaliyoendana na curcularazation dola huko ulaya magharibi zilikuwa ni dola za kidini chini ya kanisa katoliki wakati ulaya mashariki kulikuwa pia na dola za kidini chini ya kanisa la Orthodox na dola ya kiislamu kabla ya kuanguka kwa dola ya Otoman. Ndio maana baadhi ya masalia ya misingi ya dola ya kidini bado yapo katika baadhi ya nchi za ulaya magharibi.

Mimi naona tukienda katika mtizamo huo hatutafika. Kama masheikh wenyewe wamesema hadharani kwamba uislamu hauruhusu yaliyofanyika Zanzibar ni vizuri tukawaamini na kuwachukuliwa waliyofanya vurugu hizo kama wahalifu kama walivyo waharifu wengine
 
 
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…