- Source #1
- View Source #1
- Source #2
- View Source #2
Your browser is not able to display this video.
- Tunachokijua
- Kumekuwepo na video inayosambaa kwenye mitandao ya kijamii ikiwa imeambatana na ujumbe unaoeleza kuwa waisrael wanakikimbia nchi yao kuukwepa moto wa Iran.
Je, ni upi uhalisia wa video hiyo?
Ufuatiliaji wa kimtandao uliofanywa na JamiiCheck kupitia Google reverse image search kwa kutumia fremu muhimu kutoka kwenye video hiyo ulibainisha chapisho la Instagram lililo na kipande hicho cha video kilichochapishwa Juni 2, 2025, na ukurasa wa MadeInNepal.
Aidha kulingana na chapisho hilo, watu wa eneo la Dolpa walikusanyika kuvuna kuvu adimu yenye thamani kubwa ya tiba inayoitwa 'yarsagumba' Inayojulikana pia kama “Dhahabu ya Himalaya”, ambayo hukua kwenye urefu wa mita 3,000 hadi 5,000, na inathaminiwa kwa faida zake zinazodhaniwa kiafya.
Yarsagumba, inajulikana pia kama “Viagra ya Himalaya,” mmea adimu unaopatikana katika maeneo ya juu ya Milima ya Himalaya nchini Nepal. Hukua pale kuvu (fungus) inapomwambukiza kiwavi (caterpillar), na hukusanywa kati ya miezi ya Mei na Juni. Kwa karne nyingi imekuwa ikitumika katika tiba za jadi, ikiaminika kuongeza nguvu, stamina na afya ya uzazi, pamoja na kusaidia matatizo ya kupumua na figo. Katika miaka ya hivi karibuni, imekuwa chanzo kikubwa cha mapato kwa jamii za milimani kwa kuwa huuzwa kwa bei ya juu.
Wakazi wa Dolpa pamoja na wale kutoka wilaya jirani kama Rukum, Jajarkot hufanya safari ndefu na ngumu kuelekea katika malisho ya milimani ya juu. Huko hujenga makambi ya muda na kuvumilia hali ngumu za mazingira kwa wiki kadhaa ili kuvuna kuvu hiyo. Mapato yanayotokana na ukusanyaji wa yarsagumba ni muhimu sana, kwani mara nyingi huwezesha familia kujikimu kwa mwaka mzima.
Hata hivyo, shughuli hii ina changamoto nyingi, zikiwemo ugonjwa kutokana na hali ya mwinuko (altitude sickness) na mabadiliko yasiyotabirika ya hali ya hewa.