Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 34,256
- 44,597
Na. M. M. Mwanakijiji
Wanasifia "Katiba yetu nzuri"
Wanasema wameridhia EN ajiuzulu
Wakafanya kikao na kupendekeza mtu mwingine
Wakampitisha Bungeni
Wakaenda kumuapisha Ikulu
Wakahamisha vimulimuli, ving'ora na saluti
Wenye kupiga makofi na vigelegele wakapiga...
Siku tano baadaye...
Aliyesemwa kajiuzulu hajaonekana... Wanaosifia Katiba nzuri hawatuambii kama hiyo Katiba imemlinda aliye"jiuzulu"...
Hakuna aliyeonesha hadi leo EN akisema amejiuzulu kwa hiari yake au hata kuonekana akikabidhi barua au ofisi kwa makamu mpya! Sasa ikitokea wanatuonesha mwili wake marehemu... na kujitokeza kutoa poleee... si bado watatuambia "Bwana ametoa, Bwana ametwaa"?
Kama Katiba hii ni nzuri sana... kuna ubaya gani EN aelezee bila mtutu wa bunduki sikioni alivyojiuzulu?
Maana kama VP anaweza kuondolewa tukaletewa mwingine... itakuwaje tuone Rais anatoweka, hatujui aliko, siku chache baadaye tunaambiwa "inna illahi wa inna lillahi rajioun", mwingine anaapishwa....
Inakukumbusha kitu chochote?
Swali: Ikitokea Nchimbi anaibuka na kusema hajajiuzulu Umakamu je, Ndejembi atakuwa bado halali?