Wait a Minute: Hivi Tunajuaje kuwa kweli Nchimbi Alijiuzulu Umakamu wa Rais?

Wait a Minute: Hivi Tunajuaje kuwa kweli Nchimbi Alijiuzulu Umakamu wa Rais?

Ile tafsiri ya "katiba yetu ni nzuri" aliyoitoa bi Kidude tafsiri yake ni katiba nzuri kwa kufanya uhuni na maamuzi yoyote bila kuwa na wasiwasi wa kuhojiwa au kushtakiwa .
Ni taarifa rasmi aliyoitoa kwa kila mmoja anayejifanya kudai katiba mpya.
Maana yake ni kwamba, kama unataka katiba mpya, huwezi kuipata wakati hawa mashetani wakiwa kwenye madaraka.

Anawaambia waTanzania waziwazi, bila ya kificho; lakini bado kuna watu wanatamani kupata katiba mpya toka kwa hawa hawa maharamia.

Hata yale maneno ya ulaghai kayaweka pembeni, kaamua kuwa muwazi moja kwa moja juu ya uhitaji wa katiba mpya.
 
Nafikiri mazungumzo ya Mzee Warioba na VP Nchimbi ndio yanafanya tuamini ni yeye mwenyewe alijiuzuru. Tatizo kwasasa ni kusemekana hapatikani na wengi walitegemea angetokea kwenye uapisho wa mwenzake hajakwenda! Leo wengi wakajua atatokea Kanisani kama kawaida yake na hajaonekana! Sasa hii itazua wasiwasi mkubwa
Bado kuna 'option' nyingine iko wazi.
Ya utashi wake mwenyewe kutotaka kuonekana..

Hili ndilo lenye matumaini kwangu.
 
Ni taarifa rasmi aliyoitoa kwa kila mmoja anayejifanya kudai katiba mpya.
Maana yake ni kwamba, kama unataka katiba mpya, huwezi kuipata wakati hawa mashetani wakiwa kwenye madaraka.

Anawaambia waTanzania waziwazi, bila ya kificho; lakini bado kuna watu wanatamani kupata katiba mpya toka kwa hawa hawa maharamia.

Hata yale maneno ya ulaghai kayaweka pembeni, kaamua kuwa muwazi moja kwa moja juu ya uhitaji wa katiba mpya.


Sawia kabisa tafsiri yake yoyote anayedai katiba mpya nje ya hii anaingilia maslahi ya wahuni.
 
Nchimbi ni muhuni kama wahuni wengine.. Hana sababu ya kuwa habari ya mjini

Angekuwa mkweli na muaminifu hakutakiwa kutumia hata mwezi Baada ya ghasia kujiondosha

Wameona ligi ya nje imepamba moto wameamua kutengeneza ligi yao.!

Mabwege kabisa sijui wanatuchuliaje

Wanaona kila mtamzania ana asili ya Baba mnywa kahawa na kashata.! Makebo yao
 
Kwa mujibu wa AG kwa sasa hata uthibitisho wa kujouzulu wa makamo hauhitajiki kufuatia kuvuliwa uanachama
Alijiandaa(huyo msheria wa zilikale)kwa kutoa majibu kabisa ili asipate kigugumizi.Hata kama kajiuzulu kweli,kwa nini asionekane hadharani?Au alipovuliwa uanachama ndipo alipovuliwa na ujasiri na kuvalishwa aibu asiangaliane tena na watu?
 
Nchimbi ni muhuni kama wahuni wengine.. Hana sababu ya kuwa habari ya mjini

Angekuwa mkweli na muaminifu hakutakiwa kutumia hata mwezi Baada ya ghasia kujiondosha

Wameona ligi ya nje imepamba moto wameamua kutengeneza ligi yao.!

Mabwege kabisa sijui wanatuchuliaje

Wanaona kila mtamzania ana asili ya Baba mnywa kahawa na kashata.! Makebo yao
Kwamba wanamuandaa kimkakati?
 
Jasusi Chahali anasema ile barua inayosambaa hakuandika Nchimbi, ila kuna nyingine ambayo kaandika haijatolewa.

Ila uko sawa, bila kusikia Nchimbi mwenyewe anasemaje kila kitu ni suspect.

Tutajuaje hizo barua kaandika Nchimbi kweli wakati hata kwenye simu hapatikani?
Umeona sasa...yaani kama wanaamini "uzuri wa Katiba" wangeonesha kweli wanaiamini!!
 
Back
Top Bottom