Mtutuwandei
JF-Expert Member
- Jun 28, 2022
- 2,153
- 3,140
Kamanda bhana... kwani katuga si anafanya kazi yake ya uwakili ndugu.Ila Lissu atakua huru tu muda ni mwalimuLissu sio raisi ila ni mwenyekiti wa chadema.... na amewekwa ndani kwa kesi ya uongo hata hao wakina katuga wanajua kabisa kuwa wanachofanya sio haki kabisa ....Lissu sio mchaga ndio tatizo
Kuna wakati utu ni bora zaidi na kwa muumini ni dhambi kumshuhudia mwenzio uongo.....Sawa na uwe polisi halafu upewe amri umuue mzazi wako tena bila kosa je utakubali?Kamanda bhana... kwani katuga si anafanya kazi yake ya uwakili ndugu.Ila Lissu atakua huru tu muda ni mwalimu
Unakumbuka kuna wabunge walivuliwa uanachama wa chama chao ila ubunge uliendelea?...au hiyo katiba inagusa vyeo vya Urais na Umakamu tu ?..kwa maandishi ya kwenye katiba ikitokea hivyo uraisi unaondoka makamu wake anarithi kiti cha urais
Suala lile la wabunge , sote tunajua serikali ilitumia mkono mrefu na ubabe kuwabakisha , ubunge ule kuendelea haukua halali kama ni kweli walivuliwa uanachama.Unakumbuka kuna wabunge walivuliwa uanachama wa chama chao ila ubunge uliendelea?...au hiyo katiba inagusa vyeo vya Urais na Umakamu tu ?..
Sawa sema mara zote tunatanguliza hisia na mihemko.. tutajua tu mbivuKuna wakati utu ni bora zaidi na kwa muumini ni dhambi kumshuhudia mwenzio uongo.....Sawa na uwe polisi halafu upewe amri umuue mzazi wako tena bila kosa je utakubali?
Kabisa ni muhimu,hasa mchakato wa wazi pindi mmoja akijiuzulu ama sheria na taratibu zikimbana na kuonekana hafai kuendelea na majukumu.Nakubaliana na wewe ss makamu kuwa mali ya rais na chama chake huoni umuhimu ya hicho kitu ndugu, Kwenye katiba mpya iwekwe
Chochote hakiwezi kupuuzwa, Ile meseji ya x aliandika Nani kwenye account ambayo haikuwa active toka 2023Na. M. M. Mwanakijiji
Wanasifia "Katiba yetu nzuri"
Wanasema wameridhia EN ajiuzulu
Wakafanya kikao na kupendekeza mtu mwingine
Wakampitisha Bungeni
Wakaenda kumuapisha Ikulu
Wakahamisha vimulimuli, ving'ora na saluti
Wenye kupiga makofi na vigelegele wakapiga...
Siku tano baadaye...
Aliyesemwa kajiuzulu hajaonekana... Wanaosifia Katiba nzuri hawatuambii kama hiyo Katiba imemlinda aliye"jiuzulu"...
Hakuna aliyeonesha hadi leo EN akisema amejiuzulu kwa hiari yake au hata kuonekana akikabidhi barua au ofisi kwa makamu mpya! Sasa ikitokea wanatuonesha mwili wake marehemu... na kujitokeza kutoa poleee... si bado watatuambia "Bwana ametoa, Bwana ametwaa"?
Kama Katiba hii ni nzuri sana... kuna ubaya gani EN aelezee bila mtutu wa bunduki sikioni alivyojiuzulu?
Maana kama VP anaweza kuondolewa tukaletewa mwingine... itakuwaje tuone Rais anatoweka, hatujui aliko, siku chache baadaye tunaambiwa "inna illahi wa inna lillahi rajioun", mwingine anaapishwa....
Inakukumbusha kitu chochote?
Swali: Ikitokea Nchimbi anaibuka na kusema hajajiuzulu Umakamu je, Ndejembi atakuwa bado halali?