DELETED ACCOUNT
JF-Expert Member
- Mar 25, 2010
- 9,805
- 15,476
Linapokuja suala la fashion, hakuna taifa linaloipiku Italia kwenye ubunifu wa mavazi. Kidogo Mfaransa anajitahidi ila Muitaliano ni habari nyingine kabisa. Huko ndiyo wanapotoka kina Armani, Prada, Gucci, Versace, Fendi, Dolce & Gabbana, Cavalli, Valentino, nk.
Baada ya kusikia kuhusu mkataba wa mtengezaji na msambazaji mpya wa jezi za Simba JayRutty kuwa ana mahusiano ya kibiashara na Diadora ambaye ni designer wa Italy na ndiye anayeenda kubuni na kutengeneza bidhaa za mkataba huo, nikasema hapa sasa ndiyo patamu.
Kwa ufupi, design ya jezi za Simba inaenda kuwa ya uhakika zaidi. Tutegemee siyo tu jezi kali, ila pia mashati makali, kofia kali, mabegi makali, watuletee hata raba kali za Simba tutavaa.
Diadora pia wamewahi kuvalisha timu mbalimbali kama vile A.S Roma, Aston Villa, Sunderland na timu ya taifa ya Scotland.
Kwa wale wana Hip Hop, Diadora wametajwa sana kwenye mistari ya wasanii wakubwa kama Nas, Future, Young Thug, Meek Mill na wengine wengi. Pia wamewahi ķuwa na mikataba na wanamichezo wakubwa kama Boris Becker na Jennifer Capriati hawa ni wacheza tennis na wasanii kama Raekwon kutoka kundi la Wu-Tang Clan.
Nikitulia nitatoa mawazo yangu kwa upana zaidi kuhusiana na maelezo yote yaliyotolewa leo kuhusiana na mkataba huu.