Waitaliano hawana kazi mbovu, Simba inaenda kuvaa pamba kali sana

DELETED ACCOUNT

JF-Expert Member
Joined
Mar 25, 2010
Posts
9,805
Reaction score
15,476
Linapokuja suala la fashion, hakuna taifa linaloipiku Italia kwenye ubunifu wa mavazi. Kidogo Mfaransa anajitahidi ila Muitaliano ni habari nyingine kabisa. Huko ndiyo wanapotoka kina Armani, Prada, Gucci, Versace, Fendi, Dolce & Gabbana, Cavalli, Valentino, nk.

Baada ya kusikia kuhusu mkataba wa mtengezaji na msambazaji mpya wa jezi za Simba JayRutty kuwa ana mahusiano ya kibiashara na Diadora ambaye ni designer wa Italy na ndiye anayeenda kubuni na kutengeneza bidhaa za mkataba huo, nikasema hapa sasa ndiyo patamu.

Kwa ufupi, design ya jezi za Simba inaenda kuwa ya uhakika zaidi. Tutegemee siyo tu jezi kali, ila pia mashati makali, kofia kali, mabegi makali, watuletee hata raba kali za Simba tutavaa.



Diadora pia wamewahi kuvalisha timu mbalimbali kama vile A.S Roma, Aston Villa, Sunderland na timu ya taifa ya Scotland.

Kwa wale wana Hip Hop, Diadora wametajwa sana kwenye mistari ya wasanii wakubwa kama Nas, Future, Young Thug, Meek Mill na wengine wengi. Pia wamewahi Δ·uwa na mikataba na wanamichezo wakubwa kama Boris Becker na Jennifer Capriati hawa ni wacheza tennis na wasanii kama Raekwon kutoka kundi la Wu-Tang Clan.



Nikitulia nitatoa mawazo yangu kwa upana zaidi kuhusiana na maelezo yote yaliyotolewa leo kuhusiana na mkataba huu.
 
Hebu cheki na Adidas chuma cha mjerumani afu urudi kucomment upya

Hahah! ati Diadora ni mbunifu mzuri.
Diadora amekuwa anatoa vitu vikali ila inabidi uwe mtu wa underground kujua. Ukiona hadi wahuni wanamkubali ujue anatoa vitu vya kueleweka.

Kwenye picha hapo ni Kim Kardashian. Huyu anaweza kuvaa na kupromote famba?
 

Hakuna mtengeneza jezi nchi hii anae enda kudisigniwa ulaya
Jezi zote zinatengenezwa China

Jezi ikitengenezwa Ulaya basi tarajia bei yake isipungue tsh 80k,
Sasa kwa uchumi wa mashabk wetu wataweza kumudu hizo bei...!???
 
Hakuna mtengeneza jezi nchi hii anae enda kudisigniwa ulaya
Jezi zote zinatengenezwa China

Jezi ikitengenezwa Ulaya basi tarajia bei yake isipungue tsh 80k,
Sasa kwa uchumi wa mashabk wetu wataweza kumudu hizo bei...!???
Kudesign na kutengeneza ni vitu viwili tofauti. Hata iPhone zinadizainiwa Marekani ila zinafyatuliwa China.
 
Umewahi kuvaa design yoyote ya diadora!?
Anyway najua huwa yuko sana na waendesha baiskel na wale waendesha vimitumbwi
Huku ndio anakuja sasa
 
Hakuna mtengeneza jezi nchi hii anae enda kudisigniwa ulaya
Jezi zote zinatengenezwa China

Jezi ikitengenezwa Ulaya basi tarajia bei yake isipungue tsh 80k,
Sasa kwa uchumi wa mashabk wetu wataweza kumudu hizo bei...!???

Haya rudi hapa ubishe tena!

 
Wakati unazaliwa madaktari walikutoa ubongo wakareplace na kinembe cha mama,shenzi kweli
 
Ndg topolo lete umbeya mwingine tena Maana huu tayari umedoda .
 
Huyu pichani ni mchezaji wa zamani wa Simba Selemani Matola akiwa kanyuka uzi chapa Diadora πŸ˜€

Haya mambo jamani yaangalieni tu kama yalivyo, kuna sanaa nyingi sana behind the scene
 

Attachments

  • IMG-20250425-WA0018.jpg
    47.1 KB · Views: 28
  • IMG-20250425-WA0018.jpg
    47.1 KB · Views: 22
Mkuu hii dunia tuna mengi ya kujifunza kwa kukaa kimya na kuruhusu muda uongee zaidi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…