Waitara ahamasisha wananchi kuigomea serikali Wilayani Tarime

Nasikia Heche ni kama ameshaanza kampeni! Hilo linamchanganya Waitara! Badala ya hawa jamaa kuungana kuwa na lengo moja ambalo ni wananchi wanaumizana kisiasa makusudi kwaajili ya 2025.

Waitara kama imeshaamuliwa Heche arudi hapo huna la kufanya zaidi acha legacy ya kupigania wananchi wasiporwe maeneo yao. Hii kuanza kupambana na Heche ni kupoteza muda na focus, pigania wananchi na andaa life after 2025.

Wakubwa wanakunywa kahawa huku vijana ambao future kwao bado ni kubwa wanatupiana mishale na mapanga. Siasa za Bongo

Sent from my SM-A315F using JamiiForums mobile app
 
Waitara anapotea siasani mapema sana. Hili pia litamkuta Mollel kule Siha
 
Nikajua sumu ka yake inatolewa na kongoro kumbe hata kulia?
 
Mgogoro wa hifadhi ya SENAPA na wananchi kule Serengeti na Tarime ni mkubwa na ni wa kihistoria.
Tatizo ni kuwa kila upande unavutia kwake! SENAPA inatumia mabavu. Wananchi nao wanahisi kuonewa, kudhulumiwa na kunyanyaswa!
 
Kilichoturoga ni kuruhusu walafi kuwaongoza wajinga!!!!!.

Walafi wakiiba wajinga wanapiga makofi, walafi wakilia wanawataka wajinga wawaunge mkono walie wote.
Siasa za kijinga sana.
 
Inaonyesha incompetence ya serikal8 ya Samia,poor communication kati ya viongozi wa kitaifa,mpaka inasababishi huyu anasema,"Wairege mliopo sehemu mbali mbali nchi,njooni hapa tufanye fujo."
Haha Mambo yanaweza kutokea serikal8 ya Marekani,watu wanabishana for no reason?
Unakumbuka wakati ule,Nape alifukuzwa(wanabishana kuhusu Clouds),na January alifukuzwa (wanabishana kuhusu mifuko ya plastic)for no reason at all?
 
Nipo mkoani Mara nimepewa dokezo na mtu wa uhakika kwamba kuna vita inaendelea huko Tarime kijijini cha Mrito kata ya Kemambo.

Sababu kubwa ikiwa ni migogoro ya ardhi huku mwenyekiti wa CCM wilaya ya Tarime akiwa na upande wake.
Hao wamezoea vita achana nao

USSR
 
Mgogoro wa hifadhi ya SENAPA na wananchi kule Serengeti na Tarime ni mkubwa na ni wa kihistoria.
Tatizo ni kuwa kila upande unavutia kwake! SENAPA inatumia mabavu. Wananchi nao wanahisi kuonewa, kudhulumiwa na kunyanyaswa!
HUU MGOGORO NI MWEPESI SANA, KWA BAHATI MBAYA WALE WANAODAI HAKI WAMESHINDWA KUDAI KWA UTARATIBU MZURI, WANATUMIA UBABE. WAITARA (MB) NA TIBOCHE RICHARD WALISHAWAHI KUULIZA MASWALI HAYA KWENYE MAMLAKA?
SHUKA NAYO MKUU SASA UONE:

1. Kwa Mujibu wa ramani, mpaka wa hifadhi ya Serengeti unaanzia na kunaishia wapi kwa upande wa Tarime? Hii hifadhi ilianza kutambuliwa mwaka gani kisheria?

2. Kijiji cha Nyanungu kilitambuliwa kisheria mwaka gani? Mpaka wake uliishia wapi kuelekea eneo la hifadhi?

3. Eneo lenye mgogoro wanalodai wananchi nani alikuwa wakwanza kuanza kulitumia? Wananchi au Hifadhi?

4. Nani anamwingilia mwenzake katika mgogoro huu? wananchi wanaingia kwenye hifadhi kwa ajili ya kulima na kufuga au wanyama wanaingia kwenye makazi ya wananchi?

IITWE IDRA YA ARDHI YA MKOA WA MARA WATUPE RAMANI YA NYANUNGU NA SERENGETI. WAITWE WAITARA NA TIBOCHE RICHARD, WAITWE WATAALAMU WA SHERIA ZA ARDHI..

#Famasiala
#Famzaha
#Famchezo

MGOGORO UNAISHA JIONI TU
 
Waitara aende taratibu asije akaupoteza huo Ubunge, Ccm wakimuamulia atalia kila siku.
 
Kamata sukuma Ndani
 
Hii sasa Rais Samia aingilie kati hii vita soon kuna mauaji yatatokea nasema sooner or soonest, vita ni vita muraaa.

Baada ya Baraza la Mawaziri la Serikali ya awamu ya tano kupitisha azimio la kuweka mipaka huko Mara kazi ikawekwa kwa mkuu wa mkoa Meja Jenerali Seleman Mzee na Kamati yake ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa na zile za Wilaya kuweka mipaka.

Mwita Waitara analijua hilo kuwa yale ni maagizo ya Serkali ya Baraza la Mawaziri ila anaona shida ni RC Mzee Mwita anashida gani?

Mwita yupo Bungeni sasa hasemi kabisa, yeye ameweka vijana wakaondoe bicon za serikali, ameunda genge na hapa RC Mzee amemuonya kuwa atapata anachostahili.

Hii vita ipo karibu.

USSR
 
Ndipo kamati ya maadili itakapoitwa na mwita kutemwa ubunge wake!!

Japo haieleweki mwita katumwa na Nani hasa!!

Maana hili la mwita ni neno kubwa nitashangaa sana kama kajiamulia mwenyewe!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…