Uchaguzi 2020 Waitara: M/kiti CCM Mkoa Mara ana tumbo kama pipa, simuogopi

Uchaguzi 2020 Waitara: M/kiti CCM Mkoa Mara ana tumbo kama pipa, simuogopi

nokwenumuya

JF-Expert Member
Joined
Jun 29, 2019
Posts
820
Reaction score
2,896
Naibu Waziri wa TAMISEMI, Mh. Mwita Mwikwabe Waitara amesema hamuogopi mtu hata kama ana kitambi kama pipa, aliyasema hayo katika kikao na wajumbe wa CCM wilayani Tarime alipoendelea kusisitiza adhma yake ya kugombea ubunge wa Tarime Vijijini.

Alienda mbali na kusema hao wanaompinga yeye walikuwa wapi 2014 wakati CCM ikipoteza Uchaguzi wa Serikali za Mitaa?

Pia ameuliza walikuwa wapi wakati CCM ikipoteza majimbo yote mawili ma halmashauri zote? Kasema yeye amejitolea kuipa CCM uhai, na hakuna jiwe ambalo ataacha kuligeuza na haogopi na kutishwa na mtu ndani au nje ya CCM, lazima ashinde na kuwa mbunge wa Tarime Vijijini.

Isikilize video clip attached umsikilize moja kwa moja.

Zaidi soa: Mwita Waitara afikishwa mbele ya Kamati ya Maadili ya CCM mkoa wa Mara - JamiiForums
 
Siasa zetu raha sana, lengo la kwanza ni kumwondoa mpinzani wako alafu baadae sasa ndio inakuja kuhudumia wananchi
 
Hao wote pipa na mfuniko,yupo yule mwengine alimwita mwenzake makalio hao wote midomo yao imejaa laana.huwezi kuwa mtu unaishi kwa kusema sema uwongo kwa wananchi ukawa na kinywa kinachosema mazuri

Sent from my Redmi Note 5 using Tapatalk
 
Waitara ameshaigawa CCM Tarime!

Na hii ndio balaa litakaloletwa na wahamiaji wengi,........aliyebuni huu mradi hakufikiri sawasawa!
Hadi raha,ongezeni kuni huko
IMG-20191216-WA0001.jpeg
tapatalk_1575089448362.jpeg

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Naibu Waziri wa TAMISEMI, Mh. Mwita Mwikwabe Waitara amesema hamuogopi mtu hata kama ana kitambi kama pipa, aliyasema hayo katika kikao na wajumbe wa CCM wilayani Tarime alipoendelea kusisitiza adhma yake ya kugombea ubunge wa Tarime Vijijini.

Alienda mbali na kusema hao wanaompinga yeye walikuwa wapi 2014 wakati CCM ikipoteza Uchaguzi wa Serikali za Mitaa?

Pia ameuliza walikuwa wapi wakati CCM ikipoteza majimbo yote mawili ma halmashauri zote? Kasema yeye amejitolea kuipa CCM uhai, na hakuna jiwe ambalo ataacha kuligeuza na haogopi na kutishwa na mtu ndani au nje ya CCM, lazima ashinde na kuwa mbunge wa Tarime Vijijini.

Isikilize video clip attached umsikilize moja kwa moja.
View attachment 1374587
Kuna maswali mawili kabla sijachangia;
1. Kwa nini Waitara katika wabunge wote waliohama kutoka upinzani ndiyo mbunge wa upinzani pekee aliyepata nafasi ya u-Naibu Waziri ?
2. Kwa nini Waitara anajiamini kiasi hicho kuwa haogopi hata Mwenyekiti wa CCM-Mkoa kugombea na kushinda Jimbo la Tarıme ?

Jibu liko hapa:
Huyu Mwita Waitra amepata kuteuliwa kuwa Naibu Waziri kwenye Serikali ya Jiwe kama shukrani za Jiwe kwa kumsaliti Tundu Lissu. Akiwa Bungeni mnamo tarehe 7/ Septemba/ 2017 yeye ndiye alikuwa anawasiliana na Makonda kuhusu movement za Lissu toka Bungeni kwenda. nyumbani kwa Tundu Lissu. Hivyo kama malipo ya kazı aliyofanya alizawadiwa nafasi ya kuwa Naibu Waziri TAMISEMI. Na ni sababu hiyo hiyo inayomfanya ajiamini kuwa hata Mkutano Mkuu wa Mkoa wa Mara ukimpitisha mtu mwingine, itakapofika kwenye mchakato wa mwisho Jiwe atakata aliyeshinda na kurngiza jina la Waitara.
 
Back
Top Bottom