Waitara: Mwenye mamlaka na fedha za mfuko wa Jimbo ni DC pamoja na DED na si Mbunge

grudges kwa mtu usiyemtaka isiwe sababu ya kukiuka sheria zilizowekwa.Mfuko wa jimbo una wanakamati hao walikwenda wapi DC afuate utaratibu huo.
 
Waitara ukimaliza ziara Hai utulie na kupanga karata zako wapi utagombea ubunge October inayokuja.

Kwa ushauri Tu, weka akiba ya maneno na matendo yako. Muombe Mungu Sana na wekeza juhudi kwenye chama chako wakupitishe. Ukicheza vibaya jua Una miezi 10 Tu ya kutumia VX hilo na kuandikwa kwenye magazeti.

Mungu akupe hekima na busara

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kama DC na mkurugenzi ndo wenye mamlaka na fedha hizo, kwa nini uitwe mfuko wa jimbo?
Mimi naona uitwe mfuko wa wilaya/DC


Siku zote walikuwa wapi kuzigawa?

Ina maana hawajui mipaka ya kazi zao?

Hii ni AIBU KUBWA.
 
Kule tkwa watani zangu uwa kuna zao Fulani likitumiwa na hasa ukalipozea na kichui mambo huwa kama hivi
 
Ukiwa unapendwa na bwana mkubwa unaweza kufanya chochote bila shida yoyote
 
Kuna KAMATI inayohusika na UGAWAJI WA FEDHA ZA JIMBO, Mbunge ni mmoja wa Wanakamati hiyo, huko HAI hiyo kamati haipo? Kama haipo, wajumbe wengine mbali na Mh. Mbowe walienda wapi?

WAITARA UWE MKWELI.
Umeambiwa Mbunge haudhurii jimboni kwake kushughulika na matatizo ya wananchi. Kwa kifupi ni mtoro sugu jimboni ndio maana miaka 2 yote fedha za jimbo hazijapelekwa kwenye shughuli za maendeleo.

Msaidieni Mbowe kwa kumwambia aende jimboni kwake kwani amewatelekeza wananchi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hai mbugani. Awatampigia Kura tena chadema mara hii. Lyamungp nako ni shida Kwa chadema. Mh Mbowe atakuwa na kazi Sana kumshawishi. Machame kati kuna Afadhali kwake. Masama nusu kwa nusu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Anampango wa kugombea Tarime,wewe kanywe bia, barabara haitakusaidia kitu
 
Unavunja sheria alafu unashangilia Kama zuzu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hahaha huyo Waitara kasahau kwamba Ukonga ni jimbo lake, yeye huko jimboni kwake nani ilisimamiwa ugawaji wa pesa za mfuko wa jimbo,au alifyala zote.
 
Wabunge m sikanyage sheria mlizotunga. Wewe hayo yakifanyika jimboni kwako utafurahi? Jambo lililotakiwa ni Kamati kuitishwa na kama Mwenyekiti yaani Mbunge hayupo wajumbe wamteue mmoja wao aongoze kikao..
Mhe.,Waziri hapo unavunja Katiba uliyoapa kuilinda, kuidumisha na kuitetea.
 
Pale iseni jijini mwanza Rais alimhoji mbunge wa nyamagana mh Mabula kwamba anachangia shi ngapi kwa ajili ya ujenzi madarasa na vyoo? Mbunge akajibu laki mbili, Rais akasema "unachangia laki mbili tu wakati una mfuko wa jimbo?!" ndo baadae mabula akasema atachangia milioni mbili kupitia mfuko wa jimbo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuna KAMATI inayohusika na UGAWAJI WA FEDHA ZA JIMBO, Mbunge ni mmoja wa Wanakamati hiyo, huko HAI hiyo kamati haipo? Kama haipo, wajumbe wengine mbali na Mh. Mbowe walienda wapi?

WAITARA UWE MKWELI.
Huyo ni mlevi tuu, huenda hata wakati anaongea hayo alikuwa kalewa.
Kwa hiyo wilaya ya Hai tuu ndio DC ana mamlaka ya kupanga fedha za mfuko was jimbo?
Waitara acha kujipendekeza ccm wakuone unawafaa sana kumkabili Mbowe, humuwezi huyo utaishia kukamatia mpini.
 

Shida yao kubwa wanataka kuhodhi kila kitu. Wamedhoofisha Serikali za Mitaa kwa sababu ya ulafi wa kuhodhi madaraka. Hata hili la Mbunge kuwa na sauti kubwa kwenye matumizi ys mfuko wa jimbo linawakera sana hasa kwa sababu linawajumuisha wabunge wa upinzani! Wanatamani sana kurekebisha sheria lakini wanawaonea haya wabunge wa chama chao. Badala yake wanaamua kutumia mabavu. Very primitive and sadistic people.
 
Mkuu wa Wilaya ni Kiongozi Mkuu na Maimamizi Mkuu wa rasilimali Watu, Rasilimali Fedha, Rasilimali Madini na Ardhi, Ni Mwakilishi Mkuu ngazi ya wilaya. Hata Mbowe ni rasilimali ya Mkuu wa wilaya na akishindwa ku perform ajiandae kisaikolojia kusaidiwa. Ila Mbowe yuko busy na Mambo mengine naona ameelemewa na Majukumu, itabidi apumzike ubunge tu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…