Sheria inasemaje? hebu tusaidie tafadhali...
Maswala ya Mfuko wa Kuchochea maendeleo ya Jimbo la Uchaguzi yanaongozwa na sheria Sheria ya Mfuko wa Kuchochea Maendeleo ya Majimbo ya Uchaguzi, 2009 ambayo ni sheria Na. 16 ya 2009 ambayo pia inaweza kufanyiwa rejea kama Sura Na. 96 Toleo la 2015. Sheria hii kwa Kiingereza inaitwa
the Constituencies Development Catalyst Fund, 2009. Pia, maswala haya yanaongozwa na Kanuni za Mfuko wa Kuchochea Maendeleo ya Majimbo ya Uchaguzi, 2010 yaani
the Constituencies Citation Development Catalyst Fund Regulations, 2010 ambazo ni Tangazo la Serikali Na. 37 la 2010.
Masharti ya
Kifungu cha 7 na
11 cha Sheria ya Mfuko wa Kuchochea Maendeleo ya Majimbo ya Uchaguzi, 2009 yanaelekeza kuwa mamlaka ya kuidhinisha miradi ya maendeleo katika jimbo la uchaguzi na pesa za kuendesha miradi hiyo yako mikononi mwa Kamati ya Kuchochea Maendeleo ya Jimbo la Uchaguzi (
the Constituencies Development Catalyst Committee). Mbunge ndio mwenyekiti wa Kamati ya Kuchochea Maendeleo ya Jimbo la Uchaguzi kwa mujibu wa
Kifungu cha 10 cha Sheria Na. 16 ya 2009.
kwa mujibu wa
Kifungu cha 10 (1) cha Sheria Na. 16 ya 2009, Kamati ya Kuchochea Maendeleo ya Jimbo la Uchaguzi inaundwa na wajumbe wafuatao;
(a) Mbunge wa jimbo wa kuchaguliwa (Mwenyekiti)
(b) Afisa Mipango wa Wilaya (Katibu)
(c) Madiwani 2 (kutoka katika jimbo la uchaguzi husika)
(d) Makatibu Kata 2
(e) Mwakilishi wa Taasisi zisizokuwa za Kiserikali (NGO)
Hivyo basi, Mkuu wa Wilaya hausiki popote katika kufanya maamuzi ya kisera na wa kiuendeshaji wa Mfuko wa Kuchochea Maendeleo ya Majimbo ya Uchaguzi isipokuwa Mkurugunzi wa Halmashauri ambaye anahusika kama Afisa Masuhuli (Accounting Officer) wa mfumo na mtia saini (signatory) kwenye account za benki za mfuko kwa mujibu wa Kifungu cha 21 (2) na 22 (3) (a) (i) cha Sheria Na. 1 ya 2009 vikisomeka pamoja na Kanuni ya 4 (3) na 6 ya Tangazo la Serikali Na. 37 la 2010. Mkurugenzi wa Halmashauri pamoja na kuwa Accounting Officer na Signatory bado hana kabisa mamlaka ya kuidhinisha (approve) miradi na pesa za mfuko maendeleo tajwa bali mamlaka hayo yako mikononi mwa Kamati ya Kuchochea Maendeleo ya Jimbo la Uchaguzi.