Waitara: Mwenye mamlaka na fedha za mfuko wa Jimbo ni DC pamoja na DED na si Mbunge

Waitara: Mwenye mamlaka na fedha za mfuko wa Jimbo ni DC pamoja na DED na si Mbunge

Pesa ya jimbo ipo kisheria, DC hakuna sehemu ambayo inampa room ya kugawa fedha ya jimbo. DED ndo mwenyeuwezo wa kumwomba katibu mkuu wizara ya fedha kibali cha kugawa au kuhamisha fedha yoyote ya serikali iliyo chini yake. Mwita naye anatoa maagizo nje ya sheria ya Budget. DC kaanza lini kuwa accounting officer wa Halmashauri

Ngoija CAG apite
 
Mkuu wa Wilaya ni Kiongozi Mkuu na Maimamizi Mkuu wa rasilimali Watu, Rasilimali Fedha, Rasilimali Madini na Ardhi, Ni Mwakilishi Mkuu ngazi ya wilaya. Hata Mbowe ni rasilimali ya Mkuu wa wilaya na akishindwa ku perform ajiandae kisaikolojia kusaidiwa. Ila Mbowe yuko busy na Mambo mengine naona ameelemewa na Majukumu, itabidi apumzike ubunge tu



Madudu ya sabaya hamuyaoni, au ndivo mnavyomtuma?

Mwananzila kuutaka ubunge. eti anatamaa ya madaraka,

Vyeti feki, kuvamia clouds, kuvamia wafanya biashara ni UTUMISHI ULIOTUKUKA?
 
Sheria inasemaje? hebu tusaidie tafadhali...
Huyu hajielewi
Screenshot_20200109_172000.jpeg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Serikali inaongozwa na wanasiasa vichaa waliohitimu.
 
Naibu waziri wa Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Mwita Waitara amemwagiza Mkuu wa Wilaya (DC) ya Hai mkoani Kilimanjaro, Lengai Ole Sabaya kutumia Sh42 milioni za mfuko wa jimbo hilo ambazo zimekaa kwa miaka miwili bila kutumika.

Waitara amesema fedha hizo zilitolewa mwaka wa fedha 2018/19 ambazo hadi sasa hazijapangiwa matumizi yoyote kinyume na taratibu za matumizi ya fedha hizo.

Maagizo hayo aliyatoa jana Jumatano Januari 8, 2020 wakati akizungumza na watumishi wa halmashauri ya wilaya ya Hai pamoja na wananchi wa kijiji cha Longoi alipokwenda kutembelea ujenzi wa kituo cha afya.

Alisema fedha hizo ni kwaajili ya kuchochea miradi ya maendeleo. Jimbo la Hai linaongozwa na Freeman Mbowe ambaye pia ni Mwenyekiti wa chama kikuu cha upinzani nchini Tanzania.

Katika mazungumzo yake, Waitara alisema, "mwenye mamlaka ya kupangia fedha za mfuko ni DC na mkurugenzi na sio mbunge kama anavyofanya mbuge wa Jimbo hili Freeman Mbowe."

Alisema fedha hizo zilitakiwa zitumike tangu mwaka 2019 hadi sasa hazijatumika hivyo ni kosa na kwamba kwa kutumia mamlaka aliyonayo amemtaka Mkuu wa Wilaya na Mkurugenzi kutawanya fedha hizo kwenye miradi ya maendeleo vijijini.

"DC mwagize mkurugenzi atawanye fedha hizo, wananchi watume maombi na DC uzisimamie zitumike kwenye matumizi yanayotakiwa," alisema Waitara.

Aidha alisema Mbowe hana mamlaka ya kupanga matumizi ya fedha hizo bali anatakiwa kuchukua matatizo ya wananchi na kuyawasilisha bungeni.

Alisema Mbowe ambaye ni Mwenyekiti wa Chadema amekuwa mtoro wa kufanya kazi za wananchi na badala yake amekuwa akifanya matumizi ya fedha hizo kwa njia ya simu jambo ambalo sio sahihi.

"Sabaya ndie Mkuu wa Wilaya ya Hai na ndiyo mwenye mamlaka ya kuamua nini kifanyike ndani ya wilaya hii," alisema Waitara aliyewahi kuwa Chadema kabla ya kujiuzulu na kutimia CCM.

Naye Mkuu wa Wilaya ya Hai, Ole Sabaya alisema endapo mtu yoyote atafanya matumizi mabaya ya fedha za wananchi atamfyatua na kumtupilia mbali baada ya kupewa nguvu hiyo na naibu waziri huyo.

"Mheshimiwa naibu waziri kituo hiki cha afya ulicho kitembelea leo ni jitihada za kuhakikisha wananchi wa ukanda huu wa tambarare wanakumbukwa katika shughuli za maendeleo na tayari mpaka sasa kiasi cha Sh338 milioni zimechangwa kutoka vyama vya ushirika na wananchi na fedha hizo zipo katika akaunti iliyo funguliwa," alisema Sabaya.

Aidha Sabaya alimtaka mkurugenzi wa halmashauri hiyo kuhakikisha ndani ya wiki moja wananchi wanatuma maombi ya matumizi ya fedha hizo na zigawanywe kwa kufuata sheria za matumizi ya fedha hizo.

Sent using Jamii Forums mobile app
Si kweli. Mbona rais huwauliza wabunge wamechangia kiasi gani kutoka mfuko wa jimbo!! Kwa nini asiwaulize DED au DC. Kwa sheria ipi kitu kimoja kiamuliwe na watu wawili kwa wakati mmoja!?
 
Shida yao kubwa wanataka kuhodhi kila kitu. Wamedhoofisha Serikali za Mitaa kwa sababu ya ulafi wa kuhodhi madaraka. Hata hili la Mbunge kuwa na sauti kubwa kwenye matumizi ys mfuko wa jimbo linawakera sana hasa kwa sababu linawajumuisha wabunge wa upinzani! Wanatamani sana kurekebisha sheria lakini wanawaonea haya wabunge wa chama chao. Badala yake wanaamua kutumia mabavu. Very primitive and sadistic people.
Kuhusu mfuko wa bunge hata wapinzani wenyewe hawapo tayari kurekebishwa, sababu unawanufaisha wao pia kama wabunge; Yaani katika hili wabunge wote huungana na kuwa kitu kimoja sawa na pale wanapoungana yanapojadiliwa maslahi ya wabunge. Hakuna mbunge aliye tayari kukubali marekebisho ya sheria ya mfuko wa jimbo, sawa tu na majadiliano ya vyama vyote vya siasa kupewa ruzuku, hapa hata vyama vya upinzani vilivyopo bungeni huwezi kuviona vikileta hoja hiyo au kuunga mkono hoja kama ikiletwa na serikali.
 
Naibu waziri wa Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Mwita Waitara amemwagiza Mkuu wa Wilaya (DC) ya Hai mkoani Kilimanjaro, Lengai Ole Sabaya kutumia Sh42 milioni za mfuko wa jimbo hilo ambazo zimekaa kwa miaka miwili bila kutumika.

Waitara amesema fedha hizo zilitolewa mwaka wa fedha 2018/19 ambazo hadi sasa hazijapangiwa matumizi yoyote kinyume na taratibu za matumizi ya fedha hizo.

Maagizo hayo aliyatoa jana Jumatano Januari 8, 2020 wakati akizungumza na watumishi wa halmashauri ya wilaya ya Hai pamoja na wananchi wa kijiji cha Longoi alipokwenda kutembelea ujenzi wa kituo cha afya.

Alisema fedha hizo ni kwaajili ya kuchochea miradi ya maendeleo. Jimbo la Hai linaongozwa na Freeman Mbowe ambaye pia ni Mwenyekiti wa chama kikuu cha upinzani nchini Tanzania.

Katika mazungumzo yake, Waitara alisema, "mwenye mamlaka ya kupangia fedha za mfuko ni DC na mkurugenzi na sio mbunge kama anavyofanya mbuge wa Jimbo hili Freeman Mbowe."

Alisema fedha hizo zilitakiwa zitumike tangu mwaka 2019 hadi sasa hazijatumika hivyo ni kosa na kwamba kwa kutumia mamlaka aliyonayo amemtaka Mkuu wa Wilaya na Mkurugenzi kutawanya fedha hizo kwenye miradi ya maendeleo vijijini.

"DC mwagize mkurugenzi atawanye fedha hizo, wananchi watume maombi na DC uzisimamie zitumike kwenye matumizi yanayotakiwa," alisema Waitara.

Aidha alisema Mbowe hana mamlaka ya kupanga matumizi ya fedha hizo bali anatakiwa kuchukua matatizo ya wananchi na kuyawasilisha bungeni.

Alisema Mbowe ambaye ni Mwenyekiti wa Chadema amekuwa mtoro wa kufanya kazi za wananchi na badala yake amekuwa akifanya matumizi ya fedha hizo kwa njia ya simu jambo ambalo sio sahihi.

"Sabaya ndie Mkuu wa Wilaya ya Hai na ndiyo mwenye mamlaka ya kuamua nini kifanyike ndani ya wilaya hii," alisema Waitara aliyewahi kuwa Chadema kabla ya kujiuzulu na kutimia CCM.

Naye Mkuu wa Wilaya ya Hai, Ole Sabaya alisema endapo mtu yoyote atafanya matumizi mabaya ya fedha za wananchi atamfyatua na kumtupilia mbali baada ya kupewa nguvu hiyo na naibu waziri huyo.

"Mheshimiwa naibu waziri kituo hiki cha afya ulicho kitembelea leo ni jitihada za kuhakikisha wananchi wa ukanda huu wa tambarare wanakumbukwa katika shughuli za maendeleo na tayari mpaka sasa kiasi cha Sh338 milioni zimechangwa kutoka vyama vya ushirika na wananchi na fedha hizo zipo katika akaunti iliyo funguliwa," alisema Sabaya.

Aidha Sabaya alimtaka mkurugenzi wa halmashauri hiyo kuhakikisha ndani ya wiki moja wananchi wanatuma maombi ya matumizi ya fedha hizo na zigawanywe kwa kufuata sheria za matumizi ya fedha hizo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huyo naibu waziri angekuwa nchi zinazofuata sheria angeshafukuzwa kazi.Ni aibu sana.
 
Kuna KAMATI inayohusika na UGAWAJI WA FEDHA ZA JIMBO, Mbunge ni mmoja wa Wanakamati hiyo, huko HAI hiyo kamati haipo? Kama haipo, wajumbe wengine mbali na Mh. Mbowe walienda wapi?

WAITARA UWE MKWELI.
Wanasiasa wetu wanadanganya waziwazi na hawafanywi kitu.Huyu si alishasimama Bungeni na kuelezea kuwa wabunge ndo wana mamlaka nazo?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kama wenye mamlaka ya pesa ya mfuko wa jimbo ni Mkurugenzi na DC kwanini ziitwe pesa za mfuko wa jimbo? Hivi kabla ya kutoa hii kauli alikuwa bado hajapiga alcohol!!!
 
Hivi punde,
Kauli aliyoitoa mh Waziri ni nzuri na inatakiwa itumike kwa Halmashauri na wilaya zote za Tanzania.
Na itumike kwa miaka yote,usije ikatumika kwa Jimbo au wilaya Mija tu ya Hai. Huku Bukombe hiyo kauli haijatumika,tunaomba itumike wananchi tuletewe barabara,maji na umeme,tunateseka kumbe serikali yetu imetuma fedha muda mrefu zinaelekea tu hazitumiki.mh waitara hongera sana
Unahitajika uelewa mpana kuwaelewa wanasiasa wanafiki, waongo na wachonganishi, je unamfahamu vizuri waitara?

Waitara huyu anayeitumikia ccm sio yule aliyekua CHADEMA.
 
Madudu anayofanya Sabaya huko Hai, ni maelekezo ya ALIYEMTEUA,


Vinginevyo angekwisha WAJIBISHWA,


POLENI WANA HAI,


Kule Arusha alikuwa na kesi ya kijifanya TISS, Watu wakapiga kimya, Unyang'anyi aliouita makonda style mwenyewe, hadi clip mtandaoni, wakubwa zake kimya, hawasikii wala hawaoni, hili la pesa za jimbo Waitara katumwa kwenda kumwongezea nguvu.


HAI KAENI MACHO
Na huyu si ndio alikuwa na tuhuma za kumnyapianyapia msanii Nandy usiku na kutaka apewe papuchi kilazima?[emoji3]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom