Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 5,383
- 18,776
Mbunge Mwita Waitara amesema suala la Katiba Mpya ni jambo muhimu kwa Tanzania, akieleza kuwa kuna mambo matatu ambayo wananchi wanayataka, likiwamo kuwepo kwa Tume Huru ya Uchaguzi ili kuhakikisha uchaguzi unakuwa wa haki kwa vyama vyote bila kujali upande wa kisiasa.
Waitara amesema Watanzania wanataka uchaguzi ambao kila mshiriki atatendewa haki, akisisitiza kuwa tofauti za kisiasa hazipaswi kuwafanya Watanzania kuonekana kama maadui. “Hata hao wapinzani ni Watanzania na walioko chama tawala ni Watanzania. Tukisigana mawazo kwa hoja na arguments, ndio maendeleo,” amesema.
Amesema jambo la pili ni kupunguza nguvu za dola na kuweka mfumo wa uongozi shirikishi, huku akitaka viongozi wateuliwe kwa kuzingatia sifa zilizoainishwa badala ya upendeleo. “Kuna mambo yanafanyika na mtu mmoja tu nchi nzima. Watu wanataka kuwe na uongozi shirikishi; mtu akipata nafasi tuone ana sifa zilizoainishwa na sio tu amependelewa,” amesema.
Kuhusu Katiba Mpya, Waitara amesema suala hilo si la mtu binafsi bali ni hitaji la Watanzania wengi, hivyo ameitaka Serikali kulifanyia kazi. “Tumesikia Rais ana ahadi yake, lakini tunamsihi jambo hili lifanyike kwa sababu hatuwezi kwenda kwenye uchaguzi kabla ya Katiba Mpya,” amesema