Waitara: Watanzania wanataka Katiba Mpya, na nguvu ya dola kupunguzwa

Tija yake nini,itaongeza nini katika kukuza uchumi?
 
Huyu si ni mboga mboga , sasa mboga mboga na katiba wapi na wapi
 
Nimesikiliza interview yote. Nikiwa very seriously curios kusikia watu wa CCM wenye ka rekodi ka kuwa na akili akili kidogo wanasemaje na haya yanayoendelea nchini, repression, mauaji nk. Nikagundua bado yuko primitive vibaya mno kama wenzie ndani ya CCM

Kasema tunapokosoa lazima tumlinde Rais. Rais asiguswe. Rais asibagazwe.

Mtu yeyote anaesema watu wote tumlinde Rais asibagazwe huyo bado anaishi medieval ages, ambayo dunia za Ulaya zilipita zikamaliza karne ya 15
 
Anayekwamisha kupatikana katiba mpya ni kimama kwa sababu yeye amesoma elimu mbalimbali anataka vilaza kama yeye ndio waendelee kutawala.
 
Kila mtu anasema "watanzania wanataka" hiki na kile. Ni watanzania nani hao ambao wako wangapi wanaoishi wapi?
 
Nguvu ya maamuzi irudi kwa wananchi si kikundi cha watu wachache, katiba itakayo muwajibisha kiongoz bila kujali nafasi yake pale atakapo vurunda
Wananchi hushiriki maamuzi ya serikali kupitia wawakilishi i.e madiwani,wabunge,rais,wewe unataka wananchi 70m+ washiriki vipi maamuzi?
Like seriosly? Kwamba matitizo ya nchi hii ni hela tu?
Nilianza na neno ufanisi,hayo matatizo mengine yanayosababishwa na katiba ni yapi?
 
Nguvu ya maamuzi irudi kwa wananchi si kikundi cha watu wachache, katiba itakayo muwajibisha kiongoz bila kujali nafasi yake pale atakapo vurunda
Nguvu ya maamuzi irudi kwa wananchi kivipi,ukizingatia kwa sasa tupo 70+m?
Unahitaji katiba mpya Ili tu kumuwajibisha kiongozi?..kwani katiba ya sasa haimuwajibishi kiongozi?
 
Hutaki tume huru ya uchaguzi, mahakamani huru, haki ya raia ya kufanya siasa, maandamano na kuongea kwa uhuru bila kuingiliwa na dola etc yapo mengi sana na acha ujinga
Tume huru ya uchaguzi ni kwa ajili ya wanasiasa,mimi hainihusu
Maandamano mbona mnafanya na kusindikizwa juu,kuongea Heche anaongea togwa zake kila siku
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…